Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”

Anastahili sana ila Pascal umezidisha sifa .Una lako jambo.
Mkuu Senzighe, kama zipo ambazo hazistahili, sema nizipunguze, sina langu jambo lolote, ndio maana sijazungumza lolote kuhusu yale macho!.

Paskali
 
Pascal elevates Suluhu Samia to status of a demigoddess partly divine partly human. Maskhara mengine hayafai kabisa.
 
Wallah tena Wallah kisha tena Wallah Pascal una lako jambo.Una nini wewe mkuu na huyu mama yetu? Umemsifia mno na hii mara yako pili mpaka inaleta dhana.Naomba uache.
 
Pascal vipi tena na mama yetu huyu!!
Mbona unamsifia sana mpaka unazidi kipimo..
 
Kawaida yenu kutamani hivi hivi mwisho wa siku mnaanza kumgeuka na kumuita majina ya kejeli

Watanzania wanafiki sana.
 
Mhe makamu wa Rais siku ya wanawake hujaitendea haki!
Katika mazingira ambayo Tanzania ingesimama na Makamu wa Rais basi ni siku ya leo,siku ya wanawake.
Mama usoni unaonekana muungwana na mwenye huruma kiasi kwamba unanishawishi niamini kwamba moyoni huridhishwi na yanayoendelea nchini.
Mhe Makamu wa Rais,kuna sehemu nataka nikukumbushe kwamba wewe haupo ikulu kuunga mkono tu jitihada za Rais tu ila upo pia kudhihirisha uwezo wako wa kiuongozi Mungu aliokujalia,haupo kuunga mkono jitihada za wanaume tu, upo Ikulu ili kupishana kimawazo na Rais ili kujua jambo gani sahihi la kutekeleza kwa wananchi.
Inawezekana kabisa ulipendekezwa na kamati kuu ya CCM ugombee nafasi ya Makamu wa Rais kwa dhana ya kutoorefusha vikao kwasababu ya marumbano ya hoja kwa upeo wa wanaume!
Lakini unayo nafasi ya kuonyesha kwamba dhana hiyo ni mfilisi kwa wanaume,fanya sasa,amua sasa,amua kutoka nje na kueleza zuri na lile unaloona si sawa muda huu nchini halafu uone utakavyokua shujaa hata kuingizwa kwenye vitabu vya mashujaa!
Ukiachilia muda huu ambapo hata umaarufu wako unazidiwa na ule wa mbunge wa Kawe Halima Mdee na Yule Dada wa Mara aliyempiga Taison, Ester Bulaya,ukitoka nje ukanena kwa lugha utaingia kwenye vitabu vya mashujaa hata kwa kubebwa na cheo chako!
Mhe, makamu wa Rais nimeona EATV wameandika kwenye ukurasa wao wa Facebook kuwa umewaomba Watanzania wamuunge mkono Rais!
Nimechelea kuamini kama maneno hayo umeyasema,na kama umeyasema basi utakuwa umepitiwa!
Naamini unawajua Watanzania,na najua kabisa unajua kazi walioifanya tarehe 25/10/2015
Siku hiyo walimuunga mkono Mhe Rais kwa kumchagua,wakampatia Makamu wa Rais ambaye atamsaidia akichooka ama kumuunga mkono kwa yote mazuri na ikiwezekana kumkosoa hata kabla hajaja na makosa kwa Watanzania!
Kwahiyo mtu ambaye yupo kihalali ili kuunga mkono jitihada za Rais ni Makamu wa Rais.
Mhe,Makamu wa Rais waache Watanzania kuwasumbua maana wao walishamuunga mkono Rais kwa kumchagua kuwa Rais!
Mhe,Makamu wa Rais fanya wajibu wako,dhihirisha nguvu ya mwanamke ikulu kisha upambane na mfumo dume hapo ulipo,kemea utekaji,kemea mauaji,kemea MaRC na MaDC wabovu,hubiri utawala wa sheria hapo ulipo halafu usubiri uone namna utakavyoongeza thamani ya mwanamke.
Onyesha kwa mabinti walioko mtaani na wale waliopo shuleni na vyuo vikuu kwamba hukufika hapo kutokana na kutafuta usawa wa kijinsia isipokua uwezo wa kiuongozi uliojaaliwa na Mungu,Fanya hivyo tuwaone akina Samia Suluhu wengine baada yako.
Mhe Makamu wa Rais, sikulazimishi ila fanya kadri utakavyoona inakufaa.
Simama katika nafasi yako vizuri udhihirishie UMMA wa Watanzania kuwa unaweza kuwa mshauri wa Rais kama cheo chako kilivyo.
Heri ya siku ya wanawake.
Elia F Michael.
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa madiwani wa CHADEMA kanda ya Magharibi.
08/03/2018.
 
Mara kingereza mara kiswahili hata ulichoeleza kinakosa utamu, weka lugha moja tu, sasa mara tule pilau halafu unaleta ugali wapi na wapi.
 
How many do we have like her in Tanzania? In Africa? On earth? Mungi ibariki Tanzania.
 
Bro Pascal Mayala, napenda sana mada zako. Katika kusoma mada yako nimegundua kitu kikubwa kwamba huenda hujaridhika kabisa na hali ya sasa. Hizi sifa zinakufanya utamani awe Rais wa nchi. Rejea "I wish if Mungu angeamua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!. "

Hapa kwa kweli ungeweza pia kutoa madhaifu ya upande wa pili na pengine kupitia andiko lako, mambo yanaweza yakabadilika. Saa nyingine mtu habadiliki kwa sababu hajifahamu na kama anajifahamu basi mtu huyo anakuwa mpumbavu.

"Ambition Having a strong desire for success or achievement ndiko kuliko mfikisha hapo alipo, tungependa sana huyu awe, ile 2025 might be too little too late!, labda 2020 akampokee Shein au tuombe Mungu afanye mambo ili awe?." Hapa naomba kukuuliza, hivi akiwa Rais ataweza kutenda yeye kama yeye, au kuna misingi ya chama (ideology) itakayomwongoza badala yake. Hata yule mlimsifia sana kwa kweli na alipochukua form kila mmoja alifurahia sana. Nini kimetokea??? Jembe limegeuka mpini?? hata wewe kama mwandishi ulifurahi sana . Nakumbuka mara ya kwanza mlipohudhuria mahala fulani, ndipo tulipofahamu ya kwamba Mayala ni Njaa(hahhaha Samahani)
 
Maandalizi wa ACTING PRESIDENT OF THE INTERIM NATIONAL GOVERMENT
 
ukitaka kujua inside job is going on hakuna hata leak moja hata za hao wana usalama au wanasiasa na harakati zinazosema serikali ya mpito Mama Samia ,Majaliwa Au ccm ifutwe ...
Acha aendelee kupoteza muda kupambana na chadema wakati wanaomchezea ngoma wako ndani ,,,,,....wanamchekea tu
ahaahaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…