Siku za mapumziko ya Siku ya Taifa zaonesha uhai wa China

Siku za mapumziko ya Siku ya Taifa zaonesha uhai wa China

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111672138877.jpg
Siku za mapumziko za Siku ya Taifa la China inajulikana kama “Wiki ya Dhahabu” nchini China. Wiki hiyo iliyomalizika hivi karibuni ilikuwa tena fursa muhimu kwa dunia kuielewa China. Vyombo vya habari vya kimataifa ikiwemo Reuters, Yahoo Finance, na Forbes vimefuatilia ongezeko kubwa la matumizi katika nyanja za utamaduni na utalii nchini China. Kupitia “Wiki ya Dhahabu”, dunia imeshuhudia China yenye uhai mkubwa, uvumbuzi, na nia ya kufungua mlango.

Hii ni China ni yenye uhai mkubwa. Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Uchukuzi ya China zinaonesha kuwa kati ya tarehe 1 na 7 Oktoba, jumla ya safari za abiria kati ya maeneo mbalimbali ilifikia bilioni 2.142, ikiwa ni wastani wa watu milioni 306 kwa siku. Usafiri wa reli ulihudumia safari za abiria milioni 151.87, ambalo ni ongezeko la asilimia 12.7 ikilinganishwa na mwaka uliopita wakati kama huu. Aidha, katika siku hizo za mapumziko, safari ndefu za ndege zinazozidi kilomita 2,000 ziliongezeka kwa zaidi ya asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

Wachina wengi wamefanya utalii katika nchi za nje. Takwimu zinaonesha kuwa katika siku hizo za mapumziko, watalii wa China walitembelea zaidi ya miji 2,000 duniani, na wanapokwenda nchi za nje, si kama tu wanaleta mapato kwa sekta kama vile usafiri wa anga, hoteli, migahawa, na biashara ya rejareja kwa nchi wanazotembelea, bali pia ni madaraja ya urafiki kwa ajili ya kubadilishana utamaduni kati ya China na dunia.

Hii ni China yenye soko kubwa la matumizi. Pale ambapo watu wanapokusanyika, masoko hustawi. Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China zinaonesha kuwa kuanzia tarehe 1 hadi 6 Oktoba, idadi ya watalii na mapato ya mauzo katika mitaa maarufu 78 ya watembea kwa miguu viliongezeka kwa asilimia 2.5 na 4.7 mtawalia ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

Sera za kuhimiza ubadilishaji wa bidhaa za zamani kwa mpya zilichochea mauzo yenye thamani ya yuan bilioni 33.48 na kunufaisha watumiaji milioni 6.392. Mapato ya sinema katika kipindi hicho yalizidi yuan bilioni 1.1, huku kukiwa na watazamaji zaidi ya milioni 31. Mauzo ya bidhaa za kijani na bidhaa za akili bandia pia yaliongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano mauzo ya roboti yaliongezeka kwa asilimia 130 ikilinganishwa na mwaka jana, huku mauzo ya miwani ya AI yakiongezeka maradufu.

Hii ni China inayofungua mlango. Takwimu zinaonesha kuwa wakati wa siku za mapumziko ya Siku ya Taifa, China ilipokea watalii 682,000 wa kigeni, ambalo ni ongezeko la asilimia 5.4 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki, na kati ya watalii hao, watalii kutoka nchi za Ulaya waliongezeka kwa asilimia 20.

Ustawi wa uchumi wa “Wiki ya Dhahabu” ni kielelezo kidogo cha uhai mkubwa wa uchumi wa China, na pia ni ushahidi wa China kunufaishana na dunia nzima kwa maendeleo yake ya kasi. Katika siku za baadaye, China itaendelea kupanua ushirikiano wake na nchi nyingine, ili kujenga dunia yenye ustawi wa pamoja
 
Back
Top Bottom