Siku zinavyozidi kwenda nazidi kuutilia Shaka uwepo wa Mungu

Hata ukawa tayari ni Atheist, haindoi uwepo wa Mungu...!!
Ulale njaa ama Ushibe, Mungu yeye ni Mungu tu.
Ufe na Cancer ama upone Cancer, Mungu yeye atabaki kuwa Mungu tu.

Mkuu Mungu ana kanuni zake....
Haiwezekani wewe Unazini, ni mwizi, ni Mchawi, unasengenya wenzako, Muongo, Huna Upendo na wenzako, una Kisasi, una Chuki, then unataka Mungu akuone kwenye Shida zako, ilhari huombi, husaidii Masikini, hutoi Sadaka.....!!
Fata kanuni zake Utakula Mema ya Nchi...!
Hutaki kufata Kanuni zake.... Then Mungu ana Roho Mbaya mno....!
Waswahili Wana msemo wao husema pale mmoja akifariki, kwamba "Mungu Mkali" oooooh Yessss ni Mkali kweli Kwa Watu wasiofata kanuni zake.

Hizi kelele za Watu hapa wasiotambua Uwepo wake Wala hazimshughurishi....!

Umekwama Mjaribu Mungu hata kwa miezi 3, mwambie Nakujaribu kujua kama unatenda, Mwambie ntaenenda kwenye Kanuni zako, then tupia Maombi Yako hapo....! Mungu atakushangaza.
 
Hakuna Mungu, Allah, Yesu, Jehovah, Jah, God anayetoa Afya wala uzima.
Allah anasema katika suurat al zzumar kuanzia aya ya 56 zisome vizur zitakusaidia kuikoa nafsi yako

أَن تَقُولَ نَفْسٌ يَا حَسْرَتَىٰ عَلَىٰ مَا فَرَّطتُ فِي جَنبِ اللَّـهِ وَإِن كُنتُ لَمِنَ السَّاخِرِينَ﴿٥٦﴾

56. Isije nafsi ikasema: Ee majuto yangu kwa yale niliyozembea katika upande wa Allaah! Na hakika nilikuwa miongoni mwa wenye kufanya masikhara.

أَوْ تَقُولَ لَوْ أَنَّ اللَّـهَ هَدَانِي لَكُنتُ مِنَ الْمُتَّقِينَ﴿٥٧﴾

57. Au iseme: Lau Allaah Angeniongoza, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye taqwa(kumcha yeye).

أَوْ تَقُولَ حِينَ تَرَى الْعَذَابَ لَوْ أَنَّ لِي كَرَّةً فَأَكُونَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ﴿٥٨﴾

58. Au iseme pale itakapoiona adhabu: Lau ningelikuwa na fursa ya kurudi (duniani) basi ningekuwa miongoni mwa wafanyao wema.

بَلَىٰ قَدْ جَاءَتْكَ آيَاتِي فَكَذَّبْتَ بِهَا وَاسْتَكْبَرْتَ وَكُنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ﴿٥٩﴾

59. (Ataambiwa) lakini Wapi! Kwa yakini zilikujia Aayaat (na Ishara, Dalili) Zangu ukazikadhibisha, na ukatakabari na ukawa miongoni mwa makafiri.

Rudi kwa mola wako aliekuumba kutokan na tone la manii lilitiwa kwenye mfuko wa uzazi wa mama yako hauna haja ya kufanya kibri wakati umetoka kwenye njia mbili za haja ndogo
 
Robo tatu ya dunia inaongozwa na shetani, hata hiyo robo iliyobaki itatekwa karibuni. Mungu yupo wapi?
Ni kweli usemalo ila haikupi wewe ruhusa ya kuwa katika hao waovu au ikawa sababu ya kukukinga na adhabu ya allah ukiwa pamoja nao kwasababu allah anasema katika Qur an Suurat Al Nahli Aya Ya 61

وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٦١﴾

61. Na kama Allaah Angeliwachukulia watu kwa dhulma zao, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote, lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao hawatoakhirisha saa na wala hawatotanguliza.
 
Logical fallacies.
 
Mimi nakuacha ubishane na dini yako mwenyewe Genttleman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…