Sikubaliani kabisa na hii Teua Teua ya Balozi kwa kila Mtu, kwani inatuaibisha na inadhalilisha pia Hadhi ya Neno Balozi kwa wenye Akili duniani

Ungekuwa physically na Mimi na Kuuliza hili Swali ningekupiga Bonge la Ndoo ( Kichwa ) kwani ni Swali ambalo kwa ninavyokujua na Kukuheshimu kwa IQ yako Jibu unalo.
Najaribu kuonesha ni aina ipi ya vichwa vinapaswa kuteuliwa kuwa balozi na sio kuzoa yeyote yule ilimradi kuonesha ushkaji na kulindana
 
Sasa USA ndio mbinguni kwamba wakikuzuia kuingia kwao basi wewe hufai?

Mangapi na wangapi wameuwawa na Marekani bila hatia mpaka leo?

Huko Mareham unaposifia na kuabudu wewe,si ndio wanachapana risasi mchana kweupe?

Acha kukariri utumwa wa kifikra!

Jaribu kujenga hoja vizuri kwa kuelezea kile unachokiona hakifai kutokana na ufahamu wako,ila sio kwa kuamuliwa na Marekani.

Na ndio maana Sirro amepelekwa Zimbabwe maana hata Marekani haikumkubali Mugabe.
 
Umeitukana ccm wazi wazi, hapo nakupongeza
 
Nakubaliana nawe mambo mengi isipokua kipengele cha JESHI kutawala kama Rais amefariki au shida nyingine imetokea,katiba mpya itatupa nini kifanyike, Jeshi kazi yao ni kulinda mipaka ya nchi tu, our borders zimekuwa very porous yaani unaweza ingiza containers 20 za wahamiaji haramu pale namanga na wakasafirishwa hadi kasumulu bila tatizo lolote hii ni human trafficking!,pls jeshi langu stay away from politics, Linda our porous borders
 
Nakubaliana nawe kabisa, ubalozi umekuwa cheo masihara sana. Nadhani hawa wa Unguja ni watu wenye masihara wakati wote we sikiliza kauli zao tu utaona.
 
Simaanishi kuingia Marekani ndio issue, kitendo cha muwakilishi wa nchi haruhusiwi kuingia nchi nyingine hiyo ni dosari. Sirro wakati wake matukio mengi ya uvunjaji wa haki za binadamu yalitokea na hakuna alilofanya. Ex. Kuzuia maandamano kwa vitisho ilhali maandamano yalikuwa ya amani, kupeleka polisi kwenye mikutano ya vyama vya siasa nk
 
Sema baba sema baba! Wape vidonge vyao! wakimeza wakitema, shauri yao!
 
Sikupingi, yaani balozi kwa nchi zetu hizi ni kama cheo cha kustaafia watu waliotoka kwenye nyadhifa flani serikalini, wazito kwenye chama walioshindwa uchaguzi au zawadi kwa watu waliofanya jambo flani..

Sijui kama kwa sasa tuna mfumo wa kutafuta cream za kuziendeleza ili zichukue nafasi hizo kwa siku za mbeleni

Ahhh siasa za nchi hii ni pasua kichwa bora nikawajadili kina p funk na salaam
 
Zamani ukiteuliwa, ukiitwa balozi heshima ni kubwa sana ila tunapoelekea ubalozi huu utakuwa sawa wa nyumba 10

R.I.P balozi Raphael lukindo(japan)

Ova
 
basi kama jina la ubalozi linakera ,tuaiye wajumbe au sio?.......yaaninkazi ya mjumbe wa nyumba 10 ni kusuluhisha migogoro ya ndoa,kuuza viwanja na kunywa gongo au?
 
baloz huteuliwa kwanza umahili wake na elimu,lakini pia huangaliwa lengo la nchi kwenye balozi husika ni Nini,lakini pia Hali halisi ya nchi aendayo .hivi hutumika kumpata mtu atakaye fiti kwenda kuwa baloz nchi husika. Ila Sina uhakika Kama kwa Sasa yanazingatiwa haya, siku hizi imekuwa Kama pia ni sehemu ya temporary punishment kwa top govt workers,au a loop hole for curling Mastermind politicians!!
 
Nikiwa kama ni mwana CCM Kiushabiki sikumbuki ni lini nimewahi Kutomuelewa au hata tu Kutompenda Mheshimiwa Freeman Mbowe.

IQ kubwa ya Mheshimiwa Freeman Mbowe unaweza kuitafuta kwa wana CCM Wenzangu Milioni Tano nchi nzima na bado usibahatike kuipata.

Yote aliyosema hapa Mbowe ni Kweli.
 
Tanzania kuna vitu vingi sana ambavyo vinahitaji marekebisho ya kufumua mfumo wetu wa utawala na kujenga upya mfumo wa uongozi. Ni mengi sana na yanahitaji umakini kweli kweli ili tuwe na katiba nzuri. Tatizo ni kuwa kila anayeupata urais anajisemea ''subiri kidogo nifaidi kabla sijabadilisha mambo''. Hili ndilo kosa alilofanya Magufuli. Alipoambiwa mambo ya katiba akakataa kata kata kwa sababu aliona kama hakuna kitakachoweza kumwondoa. Na rais Samia naye ameingia kwenye mkumbo ule ule. Na mbaya zaidi pembeni wanakuwepo wapambe ambao wanataka mambo yaendelee kubaki kama yalivyo kwani kukiwa na ushindani wa halali basi hawafui dafu.
 
Hao wapambe ndio aliowazungumzia Nyerere kipindi anataka kung'atuka wakawa wanamwambia mzee endelea bdo kumbe mitumbo yao ndio walitaka waendelee kushiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…