Sikubaliani na mabadiliko ya Katiba yenye lengo la kumpunguzia madaraka Rais

Sikubaliani na mabadiliko ya Katiba yenye lengo la kumpunguzia madaraka Rais

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Ni siku nyingine Mwenyezi Mungu ametujalia kuiona, tukiwa wazima wa afya na amani ya kutosha. Mungu ni mwema nyakati zote.

Kama ilivyo kawaida, waona mbali huwa hawaeleweki kwa 'matomaso' na hawa ni mpaka waone ndio waamini na hivyo jukumu letu sisi waona mbali ni kuwasaidia 'matomaso' before it is too late to regret.

Katika mengi yanayohitaji Taifa kupata moja wapo ni katiba mpya , hata Kama ni hitaji la wachache lakini ni hitaji la Wananchi. Lakini kuna baadhi ya mambo yaliyopendekezwa kwenye Rasimu ya Katiba ya mzee Warioba ukiyaangalia kwa makini yatakuwa na madhara makubwa kuliko faida na mojawapo ni kupunguza madaraka ya Rais.

Ieleweke kwamba Urais ni madaraka, mamlaka na taasisi kuu katika Taifa lolote na Uimara wa Taasisi ya Urais ni kutokana na Uimara wa kiongozi mkuu wa Taasisi hiyo kwa maana ya Rais.

Kwa vyovyote vile taasisi haiwezi kuwa na nguvu Kama kiongozi wake hana nguvu hivyo kumpunguzia madaraka Rais ni kuipunguzia nguvu Taasisi ya Urais na hapa kwenye madhara makubwa baadaye.

Kwanza, baada ya kumpunguzia madaraka inawezekana yakapunguzwa madaraka yatakayoathiri utendaji wake na kufanya kwake maamuzi.

Pili, kutakuwa na majaribio mbalimbali ya kutaka kumpindua au kumuondoa madarakani. Majaribio yote ni hatari sana kwa usalama wa Taifa letu.

Tatu, Nchi itakosa mtu mwenye mamlaka ya kweli ya kusimama juu ya kila kitu na badala yake zitaibuka mamlaka nyingi zenye nguvu ya ku-challenge utawala wa nchi. Pia, kutakuwa na uwezekano wa nchi kuwa na watu wenye nguvu ya maamuzi kubwa kuliko au sawa na aliyo nayo Rais.

Nne, kunaweza kuwa na majaribio mengi ya kulazimisha tamaduni za kigeni nchi na zikakubalika ,kwa sababu hakutakuwa na Rais mwenye mamlaka ya kuamua.

Tujifunze kutoka Marekani. Marekani likiwa ndio Taifa imara kwenye demokrasia lakini wanalinda hadhi na madaraka ya Rais wao na zaidi kila leo wanawaza kuyaongeza zaidi. Mfano mwepesi, Marekani sio member wa ICC na hii yote ni kuwalinda viongozi wake wakuu kutoshtakiwa kwa maamuzi yoyote watakayochukua, wakiamini kwamba maslahi ya Marekani hayataweza kulindwa nje ya Marekani.

Tutoke nje ya box na tufikiri kwa undani, ni faida zipi Taifa itapata kwa kupunguza madaraka ya Rais? Je, ni vema kuwa na Rais ambaye sio mtendaji au mwenye maamuzi? Je, ni kweli kwamba changamoto na matatizo yote yanatokana na Rais?

Kwangu Mimi jibu ni HAPANA.
 
Maendeleo yatakuwa kwa haraka

Mikoa itaweza kutatua changanoto zao

Tanganyika itapata nguvu na kurudi upya

Muungano wenye usawa

Kuwajibishwa kwa wakuu wa mikoa, wakurugenzi na WANANCHI wa mikoa husika.

Kupunguza upendeleo wa upande mmoja wa Muungano.

Kujua vipaumbele vyetu kama nchi
 
Nakubaliana na wewe, kwa sababu kwanza wanaohamasisha uwepo wa katiba mpya wana mtazamo wa kumkomoa rais (hususan aliyepita) ni kama wana vita, pia wana chuki fulani moyoni ya kutaka kupambana na mamlaka. Hawana fair mind. Kwa hiyo kwa sasa wakianza kushughulikia katiba, hawatakuwa na balanced opinion.

Wana hasira. Acha kwanza hasira ipoe kama vile spika alivyosema mjadala wa taarifa ya CAG ufanyike mwezi wa nane. Ili kutoa nafasi ya kupitia kwa kina taarifa hiyo, pia kuwafanya wapoe ili wasije wakaongozwa na mihemko pindi wanajadili, halafu wakaharibu kazi.
 
Back
Top Bottom