Sikubaliani na Profesa Janabi

Sikubaliani na Profesa Janabi

Mwili una mifumo imara ya kutambua mapungufu na mahitaji yake.

Kwahiyo jaribio lolote la kuuelekeza (to dictate) mwili nini cha kufanya ni kuharibu miitikio ya kimaumbile.

Mwili hutoa viashiria mbalimbali unapokuwa na mahitaji ama mapungufu;

1. Kiu.........maji.
2. Njaa....chakula.
3. Miayo....uchovu.
4. Usingizi... Mapumziko.
N.k.

Kwahiyo kula unaposikia njaa, kunywa maji unaposikia kiu, nenda haja kubwa unapobanwa na haja..

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.

Hujawahi kusikia madaktari wakishauri watoto walale masaa 8+, watu wazima masaa 6+, watu wasibane mkojo muda mrefu, watu wapumzike vya ktosha kupunguza uchovu, n.k?

Sasa kwann unapokuwa na uhitaji wa chakula iwe nongwa?

Sikubaliani na prof. Janabi kuhusu nadharia yake ya mahusiano ya kisukari na vyakula. Ninachokiona ni kwamba wazungu wanataka kutuhamishia kwenye mfumo mpya wa maisha. Ni hao hao wazungu ndiyo walikuja na nadharia ya milo 4 kwa siku, sasa wanaipiga vita. What a contradiction!

Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni
Ambacho anasema dr Janabi ni "kula kwa kiasi"......huitaji ufahamu mkubwa kuona busara kwenye huo ushauri.......
 
Uwezo wa kifedha
Ugumu wa kazi
Hivyo ndio vinafanya mtu ale chakula gan
 
kwa tafiti ipi uliyofanya unaposema bado?

Bila utafiti ndugu yangu, kila mtu anajua samaki wanaoliwa Tanzania, ngomb'e bado wanafugwa kiasili, watanzania hawali processed food nk.
Mbona hili jambo liko wazi
 
Kufupisha tu kauli za Janabi ni kama hivi...

1. Tule kulingana na uhitaji sahihi wa mwili, mwenye njaa ndiye ale. (Kula kwa kiasi)
Basi hujamsikiliza vizuri. Yeye anasema watu wale mara moja kwa siku kama yeye. Waanze kwa kuu-condition mwili kwa kufanya intermittent fasting. Eti afunge masaa 16, kisha 18 na hatimaye 24. Why mtu afnaye hivi?
 
Ipo siku utakubaliana naye bila shurti.

Hapa nilikuwa na kilo 96 five years passed

bp ikawa juu, ikalazimu niende hosp.

Nikaogopa kuanza dawa za bp.

Nikabadili mfumo wa ulaji kabisa sasa nina kilo 81 niko sawa moyo hausumbuii wala sukari.

Mazoezi pia ni muhimu.
Wewe utakuwa mgonjwa. Ushauri wa janabi ilipaswa kuwa specific kwa wenye matatizo ya michakato ya physiology.
 
Ulaji mbovu wa chakula unaua sana nguvu kazi hapa Tz
Hapana. Ulaji wa vyakula havina shida. Tatizo kubwa liko kwenye:-
*matumizi yasiyo sahihi ya madawa.
*madawa yalipita muda wake.
*utaalamu duni wa madaktari wetu.
*uhifadhi mbovu wa dawa.
*matumizi mabovu ya viwatilifu kwenye nafaka, mbogamboga na matunda.

Janabi asifiche uzembe wa wataalamu na serikali ktk kuhifadhi, kutumia madawa na ukosefu wa elimu dawa kwenye ulaji wa vyakula
 
Ambacho anasema dr Janabi ni "kula kwa kiasi"......huitaji ufahamu mkubwa kuona busara kwenye huo ushauri.......
Anashauri watu waaanze kufunga kidogo kidogo kwa masaa 16 kisha 18 , halafu hatimaye wale chakula mara moja kwa siku.
 
Mwili una mifumo imara ya kutambua mapungufu na mahitaji yake.

Kwa hiyo jaribio lolote la kuuelekeza (to dictate) mwili nini cha kufanya ni kuharibu miitikio ya kimaumbile.

Mwili hutoa viashiria mbalimbali unapokuwa na mahitaji ama mapungufu;

1. Kiu.........maji.
2. Njaa....chakula.
3. Miayo....uchovu.
4. Usingizi... Mapumziko.
N.k.

Kwahiyo kula unaposikia njaa, kunywa maji unaposikia kiu, nenda haja kubwa unapobanwa na haja..

Kama vile ilivyo kwenye haja kubwa kuwa unapobanwa na haja halafu ukajibanabana madhara hutokea mwilini, ndivyo hivyo hivyo hata kwenye njaa. Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea.

Hujawahi kusikia madaktari wakishauri watoto walale masaa 8+, watu wazima masaa 6+, watu wasibane mkojo muda mrefu, watu wapumzike vya ktosha kupunguza uchovu, n.k?

Sasa kwanini unapokuwa na uhitaji wa chakula iwe nongwa?

Sikubaliani na Prof. Janabi kuhusu nadharia yake ya mahusiano ya kisukari na vyakula. Ninachokiona ni kwamba wazungu wanataka kutuhamishia kwenye mfumo mpya wa maisha. Ni hao hao wazungu ndiyo walikuja na nadharia ya milo 4 kwa siku, sasa wanaipiga vita. What a contradiction!

Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni
' Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea'

'Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni'

Hizo point zako 2 hapo juu 👆 nina mashaka na vyanzo vyake...
 
Kuhusu point ya kwanza kasome concept ya autophagy.

Na point ya 2 ni kwamba kampuni ya Nike walipobuni raba za kukimbilia ndipo wakaja na promo ya jogging wakiihusisha na afya bora.

Lkn tafiti zinanesha kukimbia kiboya na kumalizia makilomita kibao kila siku kuna madhara zaidi kuliko faida
 
Basi hujamsikiliza vizuri. Yeye anasema watu wale mara moja kwa siku kama yeye. Waanze kwa kuu-condition mwili kwa kufanya intermittent fasting. Eti afunge masaa 16, kisha 18 na hatimaye 24. Why mtu afnaye hivi?

Mimi nilimsikiliza mke wake ambaye ndiye humuandalia chakula, alihoniwa wakati fulani...

Sophia alisema, mume wake anachomaanisha ni kula kwa kiasi na kwa wakati sahihi.

Mfano wao kama familia, dinner yao wakichelewa sana kula ni saa 1 jioni...
 
Nafikiri Janabi atakuwa kaona kuna tatizo kubwa la kulemewa kwa huduma za afya kwa wagonjwa wengi kufika kwenye mahospitali huku matatizo mengi yakiwa ni yale yatokanayo na mtindo hatarishi wa maisha ikiwemo ulaji mbovu, ndo maana anajaribu kuweka hizo concepts kuhusu vyakula na ulaji.​
 
Janabi anazungumza kulingana na uzoefu WA wagonjwa anaowatibu.

Overweight na obese based disease ni vitu serious.

Vyakula tunavyokula ni salama?
Ni natural?

Au mbegu za maabara zenye side effects tele.

Mbolea je ni natural?

Hakuna side effects za madawa?

Unasemaje ukisikia njaa Tu ule kumbe tunakula vyakula vyenye sumu nyingi?
Kwahiyo tusile?
 
Mimi nilimsikiliza mke wake ambaye ndiye humuandalia chakula, alihoniwa wakati fulani...

Sophia alisema, mume wake anachomaanisha ni kula kwa kiasi na kwa wakati sahihi.

Mfano wao kama familia, dinner yao wakichelewa sana kula ni saa 1 jioni...
Sasa saa moja jioni wengine ndiyo tumalizia kumwaga zege. Mpk tukamalize, hafai tumsubiri bosi aje akague kazi na kutupatia pesa tayari ni saa 3 usiku. Inafika nyumbani saa 5 usiku. Kwahiyo kula saa moja jioni mlo wa usiku haiwezekani.
 
Organic sana? Tafsiri yako ni ipi?

Tanzania haswa Dar es Salaam, vyakula wanavyokula vina sumu kwa kiwango kikubwa. Mboga mboga na viungo vinapigwa viua wadudu leo, kesho vinachumwa na kuuzwa sokoni.

Mbolea zinatumika zenye kushurutisha mmea ukue kwa haraka ili mkulima auze apate fedha.

Sijui ni nchi gani upo, ila nchi za Ulaya wapo serious sana katika kuzingatia afya za walaji. Mpaka kwenda kwa walaji chakula hupitia katika hatua kadhaa za uthibiti.

Mara kibao Watanzania wenzako unaodai bado wanakula vitu organic, wanaomba kusafirisha vyakula haswa mboga mboga kwenda nje. Ni wachache sana wanafaulu, why? Kwa sababu vyakula hivyo vinakosa sifa ya kuliwa na binadamu.
Ngoja nikuwekee vizuri hoja ya jamaa kwa maelezo ya darasa la tatu C huenda ukaelewa.

Nchi nyingi za ulaya asilimia kubwa hawali Chakula (Food) bali wanakula biadhaa za chakula (Food Products).

Mfano wa chakula (Food) ni ugari maharagwe, kisamvu, ubwabwa mbaazi, makande, makange, mtori nk watanzania wengi hula hivi.

Mfano wa bidhaa za chakula ni Pizza, Bugger, Cheese, Cheese Bugger, Cheese pizza, Hot dogs, Coca-Cola nk wazungu 80% wanakula vyakula hivi kama mlo kamili wa siku yaani mtu anakula Pizza kama Lunch na Dinner pia daily addiction kubwa hata kwenye movie unaona littoral linasusa mpaka Pizza zake ziletwe zikiletwa linakataa "Oooh Cheese Pizza I need Cheese Burger"

Jamaa haongelei sumu ya kwenye chakula dunia ya sasa chemicals kwenye chakula haiepukiki bali anaongelea Food and Food products hizo food products ndio ulaya zimekuwa addiction na zina madhara sana kwa Tz hakuna madhara ya Junks Food labda kwa wachache na Junk food pekee kwa Tz nk Chips Yai tu 90% wajawahi kula Pizza wala KFC
 
Hapo kwenye jogging ni pagumu, labda ukizidisha ndio itakuletea shida.

Je ina maana mtu kila ukisikia nyege kwa vile ni kiasharia cha hitaji la mwili ni lazima ufanye zinaa??
Ndio kila ukisikia inabidi ufanye kwanini usifanye mwili unataka unless kuwe na factors zinazokuzuia kwasababu sisi binadamu mbali na hapo fanya.

NB: usiseme zinaa sema tendo la ndoa, neno zinaa litumike pale inapostahili.
 
Back
Top Bottom