Sikubaliani na Profesa Janabi

Vyakula natural vinakuaje?
Mbolea natural zinakuaje?
Kuna kitu ambacho hakina side effects??
Google GMO foods...
Google non natural foods
Google organic fertiliser
Google organic food...

Google is your friend...
 
Ambacho anasema dr Janabi ni "kula kwa kiasi"......huitaji ufahamu mkubwa kuona busara kwenye huo ushauri.......
 
Uwezo wa kifedha
Ugumu wa kazi
Hivyo ndio vinafanya mtu ale chakula gan
 
kwa tafiti ipi uliyofanya unaposema bado?

Bila utafiti ndugu yangu, kila mtu anajua samaki wanaoliwa Tanzania, ngomb'e bado wanafugwa kiasili, watanzania hawali processed food nk.
Mbona hili jambo liko wazi
 
Kufupisha tu kauli za Janabi ni kama hivi...

1. Tule kulingana na uhitaji sahihi wa mwili, mwenye njaa ndiye ale. (Kula kwa kiasi)
Basi hujamsikiliza vizuri. Yeye anasema watu wale mara moja kwa siku kama yeye. Waanze kwa kuu-condition mwili kwa kufanya intermittent fasting. Eti afunge masaa 16, kisha 18 na hatimaye 24. Why mtu afnaye hivi?
 
Wewe utakuwa mgonjwa. Ushauri wa janabi ilipaswa kuwa specific kwa wenye matatizo ya michakato ya physiology.
 
Ulaji mbovu wa chakula unaua sana nguvu kazi hapa Tz
Hapana. Ulaji wa vyakula havina shida. Tatizo kubwa liko kwenye:-
*matumizi yasiyo sahihi ya madawa.
*madawa yalipita muda wake.
*utaalamu duni wa madaktari wetu.
*uhifadhi mbovu wa dawa.
*matumizi mabovu ya viwatilifu kwenye nafaka, mbogamboga na matunda.

Janabi asifiche uzembe wa wataalamu na serikali ktk kuhifadhi, kutumia madawa na ukosefu wa elimu dawa kwenye ulaji wa vyakula
 
Ambacho anasema dr Janabi ni "kula kwa kiasi"......huitaji ufahamu mkubwa kuona busara kwenye huo ushauri.......
Anashauri watu waaanze kufunga kidogo kidogo kwa masaa 16 kisha 18 , halafu hatimaye wale chakula mara moja kwa siku.
 
' Usipkula unaposikia njaa, mwili utakula baadhi ya cells ama tissues zake ambazo zilikuwa zikifanya kazi nyingine hivyo kupelekea madhara kutokea'

'Ni wao walioleta nadharia ya jogging, sasa wanasema jogging inaharibu mifupa ya miguu na inaleta matatizo uzeeni'

Hizo point zako 2 hapo juu 👆 nina mashaka na vyanzo vyake...
 
Kuhusu point ya kwanza kasome concept ya autophagy.

Na point ya 2 ni kwamba kampuni ya Nike walipobuni raba za kukimbilia ndipo wakaja na promo ya jogging wakiihusisha na afya bora.

Lkn tafiti zinanesha kukimbia kiboya na kumalizia makilomita kibao kila siku kuna madhara zaidi kuliko faida
 
Basi hujamsikiliza vizuri. Yeye anasema watu wale mara moja kwa siku kama yeye. Waanze kwa kuu-condition mwili kwa kufanya intermittent fasting. Eti afunge masaa 16, kisha 18 na hatimaye 24. Why mtu afnaye hivi?

Mimi nilimsikiliza mke wake ambaye ndiye humuandalia chakula, alihoniwa wakati fulani...

Sophia alisema, mume wake anachomaanisha ni kula kwa kiasi na kwa wakati sahihi.

Mfano wao kama familia, dinner yao wakichelewa sana kula ni saa 1 jioni...
 
Nafikiri Janabi atakuwa kaona kuna tatizo kubwa la kulemewa kwa huduma za afya kwa wagonjwa wengi kufika kwenye mahospitali huku matatizo mengi yakiwa ni yale yatokanayo na mtindo hatarishi wa maisha ikiwemo ulaji mbovu, ndo maana anajaribu kuweka hizo concepts kuhusu vyakula na ulaji.​
 
Kwahiyo tusile?
 
Mimi nilimsikiliza mke wake ambaye ndiye humuandalia chakula, alihoniwa wakati fulani...

Sophia alisema, mume wake anachomaanisha ni kula kwa kiasi na kwa wakati sahihi.

Mfano wao kama familia, dinner yao wakichelewa sana kula ni saa 1 jioni...
Sasa saa moja jioni wengine ndiyo tumalizia kumwaga zege. Mpk tukamalize, hafai tumsubiri bosi aje akague kazi na kutupatia pesa tayari ni saa 3 usiku. Inafika nyumbani saa 5 usiku. Kwahiyo kula saa moja jioni mlo wa usiku haiwezekani.
 
Ngoja nikuwekee vizuri hoja ya jamaa kwa maelezo ya darasa la tatu C huenda ukaelewa.

Nchi nyingi za ulaya asilimia kubwa hawali Chakula (Food) bali wanakula biadhaa za chakula (Food Products).

Mfano wa chakula (Food) ni ugari maharagwe, kisamvu, ubwabwa mbaazi, makande, makange, mtori nk watanzania wengi hula hivi.

Mfano wa bidhaa za chakula ni Pizza, Bugger, Cheese, Cheese Bugger, Cheese pizza, Hot dogs, Coca-Cola nk wazungu 80% wanakula vyakula hivi kama mlo kamili wa siku yaani mtu anakula Pizza kama Lunch na Dinner pia daily addiction kubwa hata kwenye movie unaona littoral linasusa mpaka Pizza zake ziletwe zikiletwa linakataa "Oooh Cheese Pizza I need Cheese Burger"

Jamaa haongelei sumu ya kwenye chakula dunia ya sasa chemicals kwenye chakula haiepukiki bali anaongelea Food and Food products hizo food products ndio ulaya zimekuwa addiction na zina madhara sana kwa Tz hakuna madhara ya Junks Food labda kwa wachache na Junk food pekee kwa Tz nk Chips Yai tu 90% wajawahi kula Pizza wala KFC
 
Hapo kwenye jogging ni pagumu, labda ukizidisha ndio itakuletea shida.

Je ina maana mtu kila ukisikia nyege kwa vile ni kiasharia cha hitaji la mwili ni lazima ufanye zinaa??
Ndio kila ukisikia inabidi ufanye kwanini usifanye mwili unataka unless kuwe na factors zinazokuzuia kwasababu sisi binadamu mbali na hapo fanya.

NB: usiseme zinaa sema tendo la ndoa, neno zinaa litumike pale inapostahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…