Sikubaliani na Tundu Lissu kuhusu Hayati Magufuli

Nampenda sana Mungu wangu na nitaendelea kumwabudu na kumtii na kumtumikia. Anajua sana kuwatetea wanadamu. Kwa wale wakristo wanatambua jinsi Mungu alivyowatetea wana wa Israel wakitoka Misri kwenye mateso ya Farao na jeshi lake. Wana wa Israel walipoondoka Misri Kuelekea nchini kwao Kanani (Israel) Farao kwa kunogewa kuumiza watu alituma jeshi lake liwafuate njiani ili kwenda kuwaua na kuwateketeza kabisa. Mungu akaona isiwe tabu, walipotaka kuvuka bahari ya shamu kuwafuata akawaangamiza wote baharini.

Watanzania wakiwa njia panda wasijue nini kinaendelea nchini kwa kushuhudia watu wakiwa kwenye viroba, wakipigwa risasi, wakipotezwa, n.k. Mungu akaona isiwe tabu, likafanyika lililofanyika na maisha yanaendelea. Ujumbe hapa ni kwamba, wewe waweza kuwa mbabe ukatuumiza sana. Sisi tukishindwa kujitetea, Mungu anatutetea. Kwa hiyo usifanye mabaya kwa watu eti kwa sababu unajisemea moyoni au hadharani "hawaniwezi". Yupo anayekuweza na huna ubavu kwake hata chembe! Atakushughulikia kama walivyoshughulikiwa akina Idd Amini na wote wanaofanana naye akiwemo huyu aliyekuwepo kwetu. Mungu ni kiboko. Ukimzingua anakuzingua, na unazinguka kweli kweli.

Au nasema uongo ndugu zangu!
 
..hii ni kweli...mwendazake alikuwa dhulumati mwenye roho mbaya na njaa ya kunufaika na watu wake wa karibu na pia kabila lake... Mungu aliliona hili..akatuondolea...maana huyu angeumiza wengi..labda kuliko hata madikteta wa ukweli.m
 
Hata kumsikiliza tu TL ni kumpa kiki asiyostahili. Yule bwana yuko kazini na wanaomlipa wanafahamika!
 
Umetumia nguvu nyiiingi ukilinganisha na ulichokiandika hapo!! Bule kabisa
 
Umetumia nguvu nyiiingi ukilinganisha na ulichokiandika hapo!! Bule kabisa
Nguvu kubwa au akili unajua watu wapumbavu hushindwa kutofautisha mambo,mfano kufuta vyama vya upinzani na kuvuruga chaguzi ndiyo kudhibiti ufisadi fara??
 
Wee jomba vp ni rahis san Ku crush mtu then inakua ngum sana kwako kutoa solutions dhid ya hao unaowa crush kwa kutoa facts kutokana na bandiko hapo juu. Jifunze kuelimisha bila kuita mtu mjinga, Once who arguing with idiot always is an idiot than who he think he is!!
 
Kwa asilimia kubwa viongozi walinyamaza kimya kwa kulinda matumbo yao na si kwa kumuogopa Mwendazake . Kikubwa walichokiogopa ni kutumbuliwa tu.
Waliogopa pia kutukanwa hadharani, kupotezwa, kupigwa marisasi, kubambikiwa kesi ......
 
Na vp waliopoteza maisha yao kwa kupotezwa?
 
Nguvu kubwa au akili unajua watu wapumbavu hushindwa kutofautisha mambo,mfano kufuta vyama vya upinzani na kuvuruga chaguzi ndiyo kudhibiti ufisadi fara??
Kiwango cha ufahamu hupimwa Kwa njia nyingi, Mtu anayeshindwa kutoa hoja, na kuanza kutoa matusi, ni kipimo tosha cha kuudhihirisha ujinga wake
 
Magufuli alikuwa kiboko wa mabeberu na vibaraka wao. Alikuwa kiboko ya wapigaji wote, wala rushwa na wabadhirifu. He is the best president.
Endelea kumpamba tu huyo dikteta wako mfu! Haisaidii chochote kwa sasa! Ameshakwenda zake. Na kama hamtaweza kuishi kwa jasho kama sisi, ni bora mkamfuata tu huko aliko.
 
Umeandika ushuzi gani tena
Lissu hawezi kuitwa "Ndugu Lissu" ataitwa Bw. Lissu. Ndugu enzi za awamu ya kwanza ilikuwa na maana haswa. Kwa mfano mwizi au msaliti au yeyote aliye likosea taifa hawi addressed kwa kutanguliza Ndugu.
Mfano Kambona baada ya kukimbilia Uingereza hakuitwa Ndugu Kambona tena!
 
Hebu pitia title yako hapo juu na soma kwa umakini content yako, then utagundua kama upo sahihi au la. Umempinga mtu lkn kwa maelezo yako bado una reflect yaleyale ya uliempinga.
Wewe ndio umeshindwa kung'amua Mwenzio katumia tafsida katika kuwasilisha maoni yake.

Ana maanisha Lissu hakumpa sifa aliyokuwa anaistahili mwendazake. Badala ya kumwita dikiteta kamili yeye alimwita dikiteta uchwara akimaanisha dikiteta mdogo(mchanga)
 
Binti tuliza kihere here hutulii unakuwa kama uko kwenye heat.
Unasemaje mke wangu mbona sikuelewi elewi leo,niko jirani kwa Mangi hapa namalizia John Walker yangu na kitimoto,sikawii maana nawe kwa kususa,usije kuninyima unyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…