Sikubaliani na Tundu Lissu kuhusu Hayati Magufuli

Sikubaliani na Tundu Lissu kuhusu Hayati Magufuli

Kama anatumia kilicho chake wewe wivu unakupata ukiwa mtaa gani? Nawe tumia ya kwako utajirike!
Huyo hapo Chama Cha Maparachichi ni jamvi la wageni, kipindi kile alipelekwa Zanzibar ndiyo walikuja kumfumua marinda sasa kawa mzoefu,hela yako tu.
 
Ndugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.

Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.

Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.

Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!

Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.

Mambo yamekuwa mambo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
👏👏👏👏👏👌👌👌
 
Mbona kaeleweka mkuu..yeye anapingana na Lissu alipomuita Magufuli dikteta uchwara(dikteta lakini nusu nusu) ila yeye anasema Magufuli alikua dikteta kamili ndo maana hata watu hawakua huru kusema kuanzia raia hadi CCM wenyewe.
Hebu pitia title yako hapo juu na soma kwa umakini content yako, then utagundua kama upo sahihi au la. Umempinga mtu lkn kwa maelezo yako bado una reflect yaleyale ya uliempinga.
 
Ndugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.

Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.

Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.

Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!

Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.

Mambo yamekuwa mambo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
Nimekuelewa
 
Hata mimi nakubaliana na wewe kweli Magufuli alikua dictator kamili sio uchwara.
Lissu alimwita uchwara lini? Mwanzoni kabisa mwa utawala wake. Alipomaliza fungate la siku 100 akaanza zake. Hapangiwi wala hashauriki. Kila kitu anajua yeye. Kweli amekuja kuwa kamili mwishoni. Halima Mdee alishauri afungwe speed governor, hatukuelewa!
 
Wewe ndio umeshindwa kung'amua Mwenzio katumia tafsida katika kuwasilisha maoni yake.

Ana maanisha Lissu hakumpa sifa aliyokuwa anaistahili mwendazake. Badala ya kumwita dikiteta kamili yeye alimwita dikiteta uchwara akimaanisha dikiteta mdogo(mchanga)
Kwani
Mbona kaeleweka mkuu..yeye anapingana na Lissu alipomuita Magufuli dikteta uchwara(dikteta lakini nusu nusu) ila yeye anasema Magufuli alikua dikteta kamili ndo maana hata watu hawakua huru kusema kuanzia raia hadi CCM wenyewe.
Aisee 🤔🤔
 
Ilibidi awe hivyo kutokana na!

Kwanza ndilo lilikuwa hitaji kamili la nchi wakati huo, lakini pia lilikuwa hitaji la Upinzani Kwa kuwa walitaka apatikane kiongozi sio dhaifu, ni mwenye chembe ya udicteta, na wakati nchi ikingia ktk Hali ya kuombea, watu waliomba apatikane kuiongozi atakayezuia wizi na ufisadi uliokuwa umekithili

Kukithili Kwa uwizi, ufisadi, huduma mbovu, uuzaji madawa ya kulevya, ukwepaji Kodi, Uonevu na kila Aina ya ufisadi, ilikuwa ni cheni iliyokuwa imechukua watu weeengi mpaka ktk ngazi za juuu kabisa za viongozi wetu,

Kuondoa huo uozo, ilitakiwa awepo Mtu kama huyo, na ilimbidi awe mithili ya Dicteta Kwa sababu bila hivyo, isingewezekana kuondoa huo mfumo

Kipindi cha nyuma, watu wengi Sana walikuwa walipoteza Maisha Yao Kwa kukosa huduma nzuri mahospitalini, kwani dawa zoote za Serikali zilikuwa zikigawanwa ju Kwa ju, huku Masikini na wasiojiweza kabisa wakiathirika na mfumo huo mbovu

Kipindi cha nyuma, vijana wengi wa Kitanzania walikosa mwelekeo Kwa sababu ya kujiingiza katika mihadarati ambapo huduma hiyo ilikuwa IPO kila eneo na hakuna kizuizi, ilifikia mtu akitaka kutaja wauza madawa, anapewa masaa 24 apotee au apotezwe, Kwa sababu tu ya nguvu ya wauza madawa, na walikuwa hatari kuishinda hata serikali yenyewe

Nahitimisha kusema, JPM ambaye ni Hayati, udicteta wake tunaousema leo, tuliutengeneza Sisi, ama mazingira yaliyokuwepo ndio yaliyomtengeneza kuwa Dicteta!
Mimi naomba unieleweshe uhusihano wa kukokomesha ufisadi na kuthibiti upinzani. Je, wapinzani ndo walikuwa wanasababisha ufisadi?
 
Mimi naomba unieleweshe uhusihano wa kukokomesha ufisadi na kuthibiti upinzani. Je, wapinzani ndo walikuwa wanasababisha ufisadi?
nitakujibu vema Ikiwa unania ya kutaka kujua, maana karibu Kila mtu atakaye kuuliza hivi, ukimwambia ukweli, anakimbilia kutukana matusi utadhani ni chakula chake cha Asubuhi

Hapana mkuu!! Haikuwa hivyo,

Kwa nini JPM alionekana ni kama anagombana na Upinzani!!

Suala la Kwanza, kwanza tukubaliane wote kwamba, 2025, Vyama Vya Upinzani na wananchi wengi, walikuwa wamechoshwa na dhuruma, ukandamizaji, wizi na upolaji wa rasilimali za nchi, Matumizi mabovu ya pesa za serikali, Uonevu, mauwaji ya albino, ujambazi wa Asubuhi, mabenk kuporwa mchana kweupe, mikataba mibovu, rushwa njenje, biashara haramu na kila Aina ya uchafu ulikuwepo kipindi hicho, binafsi nilihama Chama changu CCM nilijiunga Kwa Dr Slaa!

Wapinzani walifanya kazi kubwa mno, na Mungu awabariki wapinzani wa kipindi hicho,

Wimbo ule wa Tunataka mabadiriko, ulieleweka Kwa kila Kona, mwishoni huko, kuelekea kampeni, ni ujanja tu uliozidiana, CCM, ilituzidi ujanja, badala ya CCM kumweka lowasa aliyekuwa amepakwa matope mwili mzima, ikamtupa, Upinzani wakamdaka, biashara ilianza kuharibikia hapo

Longo lilikuwa zuri, Ila kusudi likabadirika, badala ya Chama kwenda kupambana na ufisadi, Chama kikaamua kwenda kuupambania ufisadi, hicho ndicho kilibadiri upepo

Tokea hapo, mpaka leo, Chama kikuu cha Upinzani kikawa cha kutetea ufisadi,

Wale waliokuwa wamepigiwa kelele na Upinzani kwamba walitafuna pesa za EPA walipodakwa, Upinzani wakaanza kuwatetea, uwizi wa madini, Upinzani walizidisha nguvu kuutetea, ubadhirifu wa Mali za Umma, kila waliokuwa wakitumbuliwa, Upinzani walitetea, kila uovu, Upinzani walitetea, unadhani hata ungelikuwa wewe ungefanya nini,

Raisi aliyekuwepo, Kwa maono yangu, huyo alikuwa abeba agenda zoote za Upinzani, nilidhani Upinzani wangemuunga mkono, lakini badala yake walimpinga Kwa nguvu na Kwa dharau kubwa, Kwa kuwa na yeye ni binadamu, akaona, kumbe hata Upinzani wako nyuma ya maharamia hawa,

Sjui mara MIGA, sijui Bora Ndege Bora zishikwe, sjui mara matusi ya ajabu ajabu, nakwambia, Kwa namna hiyo, akawajumlisha Upinzani kwenye fungu la mafisadi ingawa siyo, Ila Kwa sababu ya kuutetea uharifu huo, hata angelikuwa Raisi kutoka Upinzani, uzalendo ungemshinda, angedili NAO wapingaji wote kutoka CCM

Mkuu, nadhani Kwa ufupi umeelewa, ni Kwa nini Rais alionekana kuwa adui wa Upinzani,
 
Kiwango cha ufahamu hupimwa Kwa njia nyingi, Mtu anayeshindwa kutoa hoja, na kuanza kutoa matusi, ni kipimo tosha cha kuudhihirisha ujinga wake
Hata Yesu aliwatukana Mafarisayo kwa unafiki wao(Soma Mathayo23:1-21) kama hufahamu kuwa tusi sehemu nyingine hutumika kuonya,kukaripia na kufundisha basi utakuwa mjinga tu.
 
Hata Yesu aliwatukana Mafarisayo kwa unafiki wao(Soma Mathayo23:1-21) kama hufahamu kuwa tusi sehemu nyingine hutumika kuonya,kukaripia na kufundisha basi utakuwa mjinga tu.
Mfano wako ni wa kijinga usioendana na ulichokusudia, na kiwango chako cha kufikiri kipo Chini mno, siwezi bishana na wewe!!
 
Back
Top Bottom