SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 50,104
- 75,552
Huyo hapo Chama Cha Maparachichi ni jamvi la wageni, kipindi kile alipelekwa Zanzibar ndiyo walikuja kumfumua marinda sasa kawa mzoefu,hela yako tu.Kama anatumia kilicho chake wewe wivu unakupata ukiwa mtaa gani? Nawe tumia ya kwako utajirike!
Ukiona hivo wewe sio greti thinka. ..Mimi hata sijaelewa dhumuni/main point ya hili bandiko.
👏👏👏👏👏👌👌👌Ndugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.
Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.
Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.
Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!
Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.
Mambo yamekuwa mambo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
Hebu pitia title yako hapo juu na soma kwa umakini content yako, then utagundua kama upo sahihi au la. Umempinga mtu lkn kwa maelezo yako bado una reflect yaleyale ya uliempinga.
NimekuelewaNdugu Tundu Lissu, ingawa yuko CHADEMA na mimi CCM, ni zaidi ya rafiki kwangu. Nimemzidi umri na uzoefu katika siasa lakini amenizidi maarifa ya kisasa. Lissu nipo naye kwenye shida na raha kisiasa na kimaisha. Ni zaidi ya ndugu yangu. Tunafurahi wote na kuhuzunika pamoja.
Lissu, mwanzoni kabisa mwa utawala wa Mwendazake, aliwahi kumuita Mwendazake kuwa ni DIKTETA UCHWARA. Yaani, Mwendazake hakuwa DIKTETA KAMILI. Sikubaliani na Lissu katika hili. Namkatalia kwa nguvu, uwezo, upeo na ninachokiona.
Watu sasa wanazungumza 'ukweli'; CAG ameuanika 'ukweli'; wanaCCM wanaambiana 'ukweli' na hata wanasiasa wanaanza kurejea kwenye 'ukweli'. Ni kama watanzania wameupata upya uhuru wao wa kufikiri na kujenga hoja za haja. Angekuwepo Mwendazake mambo yasingekuwa hivi yalivyo sasa. Hata CAG asingesoma Ripoti yenye ladha hii.
Dikteta ni kiongozi wa kutisha. Wa kuogofya. Wa kunyamaza mbele yake hata kama ulikuwa na hoja. Wa kuvumilia mbele yake hata kama unaumia. Wa kulia sirini na kucheka hadharani. Wa kutetemeka na kutetereka bila kucheka unapojieleza mbele yake. Wa kusifiwa bila ukweli kuambiwa. Dikteta si wa mchezomchezo!
Mwendazake hakuwa wa kawaida. Kufunguka huku kwa kumwaga maoni kama koni ni kuonesha kuwa Mwendazake alikuwa na sifa za kutisha na kuogofya. Ndugu yangu Lissu nisikie: Mwendazake hakuwa DIKTETA UCHWARA. Alikuwa DIKTETA wa kweli. Ndiyo maana hivi sasa hata wanaCCM wanashangaana jinsi walivyo huru kusema na kutenda.
Mambo yamekuwa mambo!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)
Lissu alimwita uchwara lini? Mwanzoni kabisa mwa utawala wake. Alipomaliza fungate la siku 100 akaanza zake. Hapangiwi wala hashauriki. Kila kitu anajua yeye. Kweli amekuja kuwa kamili mwishoni. Halima Mdee alishauri afungwe speed governor, hatukuelewa!Hata mimi nakubaliana na wewe kweli Magufuli alikua dictator kamili sio uchwara.
Mkuu cheti chako cha o level ni vile vya ndalochako nn? Vile vyenye picha ya mtahiniwa! Mbona bandito lipo wazi?Mimi hata sijaelewa dhumuni/main point ya hili bandiko.
Mengi yatasemwa ila mwamba alikua mnyanyasaji wa kijinsia.
KwaniWewe ndio umeshindwa kung'amua Mwenzio katumia tafsida katika kuwasilisha maoni yake.
Ana maanisha Lissu hakumpa sifa aliyokuwa anaistahili mwendazake. Badala ya kumwita dikiteta kamili yeye alimwita dikiteta uchwara akimaanisha dikiteta mdogo(mchanga)
Aisee 🤔🤔Mbona kaeleweka mkuu..yeye anapingana na Lissu alipomuita Magufuli dikteta uchwara(dikteta lakini nusu nusu) ila yeye anasema Magufuli alikua dikteta kamili ndo maana hata watu hawakua huru kusema kuanzia raia hadi CCM wenyewe.
Mimi naomba unieleweshe uhusihano wa kukokomesha ufisadi na kuthibiti upinzani. Je, wapinzani ndo walikuwa wanasababisha ufisadi?Ilibidi awe hivyo kutokana na!
Kwanza ndilo lilikuwa hitaji kamili la nchi wakati huo, lakini pia lilikuwa hitaji la Upinzani Kwa kuwa walitaka apatikane kiongozi sio dhaifu, ni mwenye chembe ya udicteta, na wakati nchi ikingia ktk Hali ya kuombea, watu waliomba apatikane kuiongozi atakayezuia wizi na ufisadi uliokuwa umekithili
Kukithili Kwa uwizi, ufisadi, huduma mbovu, uuzaji madawa ya kulevya, ukwepaji Kodi, Uonevu na kila Aina ya ufisadi, ilikuwa ni cheni iliyokuwa imechukua watu weeengi mpaka ktk ngazi za juuu kabisa za viongozi wetu,
Kuondoa huo uozo, ilitakiwa awepo Mtu kama huyo, na ilimbidi awe mithili ya Dicteta Kwa sababu bila hivyo, isingewezekana kuondoa huo mfumo
Kipindi cha nyuma, watu wengi Sana walikuwa walipoteza Maisha Yao Kwa kukosa huduma nzuri mahospitalini, kwani dawa zoote za Serikali zilikuwa zikigawanwa ju Kwa ju, huku Masikini na wasiojiweza kabisa wakiathirika na mfumo huo mbovu
Kipindi cha nyuma, vijana wengi wa Kitanzania walikosa mwelekeo Kwa sababu ya kujiingiza katika mihadarati ambapo huduma hiyo ilikuwa IPO kila eneo na hakuna kizuizi, ilifikia mtu akitaka kutaja wauza madawa, anapewa masaa 24 apotee au apotezwe, Kwa sababu tu ya nguvu ya wauza madawa, na walikuwa hatari kuishinda hata serikali yenyewe
Nahitimisha kusema, JPM ambaye ni Hayati, udicteta wake tunaousema leo, tuliutengeneza Sisi, ama mazingira yaliyokuwepo ndio yaliyomtengeneza kuwa Dicteta!
Long storyMungu wangu alikufanyaje[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
nitakujibu vema Ikiwa unania ya kutaka kujua, maana karibu Kila mtu atakaye kuuliza hivi, ukimwambia ukweli, anakimbilia kutukana matusi utadhani ni chakula chake cha AsubuhiMimi naomba unieleweshe uhusihano wa kukokomesha ufisadi na kuthibiti upinzani. Je, wapinzani ndo walikuwa wanasababisha ufisadi?
Hata Yesu aliwatukana Mafarisayo kwa unafiki wao(Soma Mathayo23:1-21) kama hufahamu kuwa tusi sehemu nyingine hutumika kuonya,kukaripia na kufundisha basi utakuwa mjinga tu.Kiwango cha ufahamu hupimwa Kwa njia nyingi, Mtu anayeshindwa kutoa hoja, na kuanza kutoa matusi, ni kipimo tosha cha kuudhihirisha ujinga wake
Mfano wako ni wa kijinga usioendana na ulichokusudia, na kiwango chako cha kufikiri kipo Chini mno, siwezi bishana na wewe!!Hata Yesu aliwatukana Mafarisayo kwa unafiki wao(Soma Mathayo23:1-21) kama hufahamu kuwa tusi sehemu nyingine hutumika kuonya,kukaripia na kufundisha basi utakuwa mjinga tu.