fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 384
- 658
Mama yangu alichagua kutoolewa na baba yangu. Alimsihi, lakini alikuwa amependa mtu mwingine. Alijaribu kuwa sehemu ya maisha yangu nilipokuwa mdogo, lakini baada ya hapo, kimsingi alitoweka maishani mwangu. Mimi na baba yangu wa kambo hatukuelewana, alikuwa mtu wa kutukana na sote tulimwogopa.
Baadaye (nikiwa kijana), nilijaribu kuungana na baba yangu. Lakini alikuwa na uchungu sana, alikataa kuwa na uhusiano wowote na mimi. Hakutaka hata kuzungumza nami, na akaniuliza nisimsumbue. Sikuwa na sura ya baba.
Baadaye sana, nilipokuwa mtu mzima, nilijitahidi kujaribu tena. Nilikuwa nimeoa, na kupata watoto (nilikuwa mtoto wake wa pekee). Alikuwa babu, na hakujua.
Nilimtafuta kwa miaka kadhaa na hatimaye nikampata
Alikuwa sasa ni mtu mzima alie hudumu katika msikiti mkubwa pale jijini Mwanza
Alijitolea kwa kufanya usafi wa makubazi na kusafisha vyoo pale msikitini
Viongozi walikuwa wakimlipa kiasi kidogo ambacho hakikukidhi mahitaji yake'
Alikuwa akilala katika chumba kidogo kilicho mtosha peke yake kujihifadhi
Kilikuwa ni chumba kilichotumika kuhifadhia Sanda za maiti walio pata ajari au kukosa ndugu zao
Kwakuwa nilikuwa nimemtafuta baba yangu kwa miaka mingi sasa sura yake haikuwa imebadilika sana japo uso wake ulikuwa na makunyanzi ngozi ilio kunjamana na kuiondoa nuru ya furaha katika muonekano wake
Nilimhitaji baba yangu ili kuwaelimisha wanangu juu ya ukoo wangu sikuwa nikiyapenda maisha ya kukaa pasina ukoo japo wazazi wangu wote hawakuwa watu wakujari'
Nilikuwa nimekaa pale mimbari ghafula taswira ile ilio ondoka miaka mingi machoni pangu ilikuwa imesimama mbele yangu ikiwa na kibalaghashia ambacho waumini walikuwa wakitupia sadaka zao'
Moyo kama ulinipasuka pwaaaa!
Huyu nilimuona wapi?
Niliunganisha fikra zangu na hatimae nikasema huyu ni mtu pekee alie lipia gharama kadhaa juu ya makuzi yangu'
Nilimgoja pindi alipo nifikia ili nichangie kiasi kadhaa kwenye kile kibalaghashia'
Niliinua kichwa changu nakumtazama kwa mkazo yule mzee nikitaraji huenda angelinikumbuka lakini haikuwa kama nilivyo fikiri baba aliendelea na shughuli yake yakuzikusanya Sadaka hata mbele yangu alitikisa kile kibalaghashia'
Nilikuwa ni kijiuliza ni kwa njia gani ningeliweza kuanzisha maongezi na mtu yule'
Moyo wangu ulinisemeza kuwa na subra atakapo keti mfate na umuelezee kile uwazacho'
Baada ya muda mzee alimaliza kukusanya sadaka na watu sasa walitawanyika pale msikitini ndipo nilipo msogelea na kumuita kwa jina lake halisi'
Samahani Mzee Amlani!
Naomba kuongea na wewe mzee wangu'
Jina hilo halikuwa likijulikana pale mjini na hata msikitini hakuitwa hivyo jambo lilomtia mshutuko huku macho akiwa ameyatumbua na sasa kumbukumbu zilikuwa zimemuingia aliniita kwa mshutuko huku macho yake yakitoa miale ya huzuni ilio tengeneza mifereji ya machozi'
Burhaaani
Burhaaani
Sauti yenye mitetemo na mikwaruzo ilio beba tumaini juu ufufuo baada ya mauti'
Huyu sasa alikuwa amenikumbatia huku jasho lilo ambatana na machozi vikimtiririka mithiri ya mtu alie fukuzwa na Dubu'
Tuliketi juu ya lile jamvi lenye nyumba tukufu ya Al qaabah huku nikiyaelekeza macho yangu iliko Kibrah'
Baba alikuwa akaniuliza simulizi nyingi za miaka kadhaa iliopita kati yetu huku akitaka kujua juu ya mama yangu'
Nilimueleza kinaga ubaga japo khadidu za mama sikuwa nikizijua ni wapi aliko kuwa hasa baada ya kuachana na yule mme wake wa mala ya pili
Baba alikuwa mwenye huzuni na majuto ni wazi alikuwa akiitafuta toba ya kweli toba ya kuikana Damu yake na Mungu kumpa laana pasina kupata mtoto baada ya hapo'
Nilianza kuujaza Moyo wangu upendo japo alikuwa ni baba msaliti lakini sikuwa na namna zaidi ya kuikabili ilio kweli huyo alikuwa ni baba yangu Mzazi