Sikutegemea kama Mtwara ina fursa kiasi hiki

Mpuuzi wewe hizo korosho umelima wewe? Kama huwezi changia si ungenyamaza tu kuliko kuonyesha upuuzi wako,ni bodaboda wewe eh??
 
Zanzibar wamelostika na ndiyo maana wananchi wake hawaeleweki.
 
Chuki ni kitu kibaya mno eti mtu anawalaumu wana kusini kisa hawana maji wala barabara za lamiπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†.... Hivi tuwe wakweli nchi hii kuna jamii waliyojenga barabara za lami wao wenyewe? Mungu wa ajabu sana kusini tuna fursa nyingi mno na rasilimali za kutosha,Kuna kipindi mzee lowasa yupo waziri alikuja kung'oa mashine ya kusukuma maji kule mitema akaileta nyingine ambayo ni mbovu yote ni kwa ajili ya kutukomoa sisi, ndipo hapo tukaanza kufukua visima kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua ambavyo tunatumia mwaka mzima....Aliyefika wilaya ya newala na tandahimba atakubaliana na mimi kuwa hakuna sehemu yenye visima vingi nchi hii kuzidi sehemu hizo
 
Mtwara na lindi ni mikoa yenye fursa kubwa sana ya ardhi,hivyo kama mwekezaji ukitaka ardhi ya kutosha nenda mikoa hiyo hasa katika suala la kilimo na ufugaji.

Pia uwepo wa bahari fursa za uvuvi na mazao ya bahari nayo ni kubwa.

Ila fahamu tu watu wa kusini kiasili ni wavivu,na wakipata hela kidogo ya korosho ndio basi tena hupati hata kibarua shambani kwako,hadi hela za korosho ziishe ndio utawaona πŸ˜….

All in all kusini kuna watu wakarimu na wanao penda wageni japo sio maeneo yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…