Sikutegemea nilichokikuta ukweni

Ni kweli inategemea familia ila kwa ujumla ukienda uchagani jiweke vizuri.
Niliozesha pacha wangu kama miaka mitano ilishapita ,huko kwa wahaya nilihakikisha anaenda bure kabisa kwa sababu wajomba walitaka kuingiza drama ila sisi kama familia hatukua tunataka chochote ,kwa sababu mahari ni kama biashara tu.
 
Acha uoga kijana. Mahari huwa haiishi. Wewe tuma mshenga wako wapeleke hiyo 1.5m, hakuna atakaeikataa hela. Mipango ya harusi itaendelea, utaoa maisha yataendelea. ACHA UOGA.
 
Siungi mkono hoja
Usikope mahari usipolipa utadharaulika milele. Kuna babu mmoja daily alikuwa anazarau mkwewe pale wakigombana kwamba kwanza mahari yenyewe amekopa na Hadi Leo hajamalizia... Na mwanae alisomesha mwenyewe.
Ukitaka heshima usikope mahari lipa yote
 
kwanza uelewe kwa tamaduni nyingi mahari inaongelewa na ndugu/ukoo na si baba wa binti tu
kwahiyo hao watu ndo wanatakiwa kushawishiwa kwamba uwezo wako ni huo wa 1.5
huku tarime sisi tunaolea hadi ng'ombe 20 na 30 hiyo ni kama M10 hadi M20
 
mahari siyo issue ya kidini .
eti mkurya umuoe kwa hizo M4. thubutu ni M10 na kuendelea
 
Acha ubishi mkuu waislamu hawana mambo mengi kwenye suala la mahari hilo lipo wazi sio mambo ya kusadikika.
Hilo ni kweli mwamba waislamu mwanamke anataja mahari yake ila siku hizi mambo yanaenda tofaut kidogo mahari inajadiliwa before alaf yeye atasema tu siku hizi kuoa mahari gharama kwa wote sio zipo ila zinaendana na hadhi ya familia mara nyingi
 
kwakuwa natambua kwamba mahari huwa haiishi (baada ya kuelezwa na wakubwa wangu)
Hao unaowaita wakubwa zako wamekudanganya(huenda na wao hawana uelewa kuhusu hilo) kwa sababu msingi mkuu wa ndoa ni mahari bila mahari hakuna ndoa na inasisitizwa sana muowaji kumaliza mahari haraka iwezekanavyo kwa sababu ikitokea umefariki kabla ya kumaliza deni la mahari kesho utakuwa na dhima kubwa kwa Mola wako.
 
Ninesoma replies nyingi nimegundua wengi humu wanalalamika maari kubwa kwa sababu hawana kazi au wanapitia maisha magumu

Mimi ni mchaga kutoka Rombo, nimeoa mmasai. Ni haki ya mzaszi kutaka maharishi ya mwanae, Leo anakuja lofa mmoja na shida zake analalamika kuwa mahari ni kubwa.

Nililipa million 4 na sikulalamika. Fair kabisa

Jifunzeni kuheshimu tamaduji za wengine na wanawake mnaowaoa. Unakuja jamaaa linanunua malaya kwa mwaka linatumia zaidi ya hiyo mahari aliyotajiwa huku linalalama kuwa maharishi ni nyingi

Juzi nimetoka kumkemea mtu kazulimiwq lako na nane na baba mkwe anatangaza kila kona. Mwanaume unatakiwa kuvunga kitu kama hicho unamezea sio kulia kulia lia

Kifupi mwanaume hutakiwi kulia lia umeshindwa kulipa maharishi. Kama umeshindwa pita na njia zako sio kulia kulia au kulaumu wake, AIBU
 
Kijana umenichekesha, mahali huwa sio deni, hakuna mtu atakupeleka mahakamani kukudai maali.

Hata wakisema milioni mia, kama kweli binti unampenda basi unaomba kutoa kilichopo nyingine unaahidi kumalizia lakini ndio imeisha hiyo.

Tunakwenda ukweni ili kurasimisha undugu, unaishi na binti wa watu kwao hawakujui, akikufia utasema nini??
 
Kwahyo hakumuoa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…