Sikutegemea Rais Samia angeiongoza Tanzania Masikini vizuri kuliko Magufuli

Sifuri kivipi na dira gani iliyopotea mpaka sasa? Magufuli alikuwa na agenda kuu 4, SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, ujenzi wa makao makuj Dodoma na Air Tanzania. Ndani ya mwaka mmoja mama anaendeleza ujenzi katika vipande vyote vya Reli, na kazi inaendelea.

SGR katika kipindi cha mwaka mmoja ni kama amefanya double ya hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Bwawa. Air Tanzania zinaendelea kuaibgezeka na kufanya safari kama kawaida. Ndani ya mwaka mmoja amejenga vituo vya afya vingi kuliko Rais yoyote aliyewahi kumtangulia. Ndani ya mwaka mmoja Samia amejenga madarasa mengi kuliko Rais yeyote aliyemtangulia. Ndani ya mwaka mmoja amekamilisha mradi wa Megawati 85 pale Ubungo ambapo magufuli aliutelekeza akituaminisha kuwa gesi yote imeuzwa. Ni Samia Huyu kwa mara ya kwanza ameitoa bajeti ya Kilimo toka bilion 200+ hadi 900+; Ni Samia Huyu aliyefungua ten ajira baada ya msoto wa miaka 7.

Ni wapi unapata ujasiri wa kumpa sifuri kwenye uongozi wake. Punguzeni chuki Samia tries her best despite the difficult moment facing the world.
 
Tanzania hatujawahi kuwa na raisi toka tupate Uhuru na ndio maana ni taifa sio tu masikini bali ni fukara.Tatizo la wanaojiita maraisi wa Tanzania ni kutaka kutawala na sio kuongoza.wanataka kumiliki nchi na kila kitu kilichomo.Mimi hakuna raisi ninayemtambua mpaka pale tukipata raisi atakayerudisha nchi mikononi mwa wananchii.
 

"Huyu mama", "Mzanzibari" haya maneno ya kejeli ndio kitu pekee walichonacho mashabiki wa mwendazake. Wamejaa ubaguzi wa kikabila,kitaifa na kijinsia
 
Tunaomba ilo tipa lililotumika kwenda kumwaga hizo korosho mwaisa
 
Mafisadi Magufuli alishamalizana nao ndio maana Mama ni Rahisi kuongoza

Magufuli kasafisha njia!...
 

..Kwenye suala la UKATILI Jpm amemzidi Ssh kwa mbali sana.

..Jpm angetoa kauli ya " ukinipara nitakuparua " lazima ingefuatiwa na tukio la mpinzani au mwanaharakati kuumizwa.

..Hakuna mwanadamu asiye na mazuri yake. Na kuna mambo mazuri Jpm aliyafanya.

..Kinacholeta tabu na mabishano ni kwamba mabaya[ ukatili ] ya Jpm yalivuka mipaka kuweza kuyafunika kwa mazuri yake.
 
Magu hakuwahi kuwa na qualities za Uraisi, Wala hakustahili kuwa Rais hata wa chama Cha Muziki
Qualities za Urais ni zipi?
Ungepewa wewe hio nafasi ungeiweza?

Kwenye keyboard mpo vizuri kutaype,wake zenu tu wanawapeleka puta
 
Alishasema hakutaka Apendwe mke wake alishampenda imetosha,huku watu kila siku ni kuanzisha uzi

Yalishapita hayo,wakunyooka walinyooshwa,tufanye mambo mengine sasa 😁😁
 
Qualities za Urais ni zipi?
Ungepewa wewe hio nafasi ungeiweza?

Kwenye keyboard mpo vizuri kutaype,wake zenu tu wanawapeleka puta
Unazungumzia mke Wangu na sio nchi, acha kupaniki, hivi Chato Iko kwenye topten kweli kwenye matokeo ya six?
 
Uchawi upo mkuu...uchawi wa hela....
 
Mnajiuliza na kujijibu wenyewe kweli nyie viazi kweli
 
Kwa kipimo chochote cha mwenye akili, Rais Samia is ahundred better kuliko mtangulizi wake.
 
Kama hana pressure ya makundi kwanini akawaondoa kina Lukuvi na Ndugai kwenye serikali yake, na kuwajaza watoto wa marafiki zake, na yule waziri shemeji yake?

Mnamjaza sifa za uongo.
Kwani Ndugai na Lukuvi, ni lazima wawe viongozi wakati wote? Kutokuwepo kwao kumepunguza nini? Jambo la muhimu ni je, Serikali inatekeleza namna gani majukumu yake.

Mbona huongelei Kalemani, Kabudi, Luhaga, Chamuriho, na wengine ambao waliwahi kuhudumu kwenye nafasi za Uwaziri, na baadaye wakaondolewa au kuachwa?

Tumsute Rais Samia kwa Serikali yake kushindwa kutekeleza majukumu yake lakini siyo eti kwa nini fulani yumo au hayumo kwenye Serikali yake. Labda kuwe na ushahidi wa kutosha kuwa kuna watu anapendelea au anawaonea, maana akifanya hivyo atakuwa amekiuka kiapo chake. Vingenevyo, tumwunge mkono katika yale yote mazuri ili Taifa lipige hatua baada ya kudumazwa kwa miaka 5.
 
Kila mwenye uelewa mkubwa anajua kuwa Marehemu, kupewa nafasi kubwa kama ile ilikiwa ni kumwonea, sawa na kumbebesha kilo 50 mtoto wa miaka 15.

Nafasi kubwa kama ile inahitaji sana hekima na uelewa mpana wa mbo mengi kuliko maguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…