Barieda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 1,808
- 2,470
Wakuu kwema,
Moja kwa moja kwenye mada, katika maisha yangu nilijitunza sana ili kuhakikisha sizai hovyo na mwanamke ambaye sitamuoa na nihakikishe napata mwanamke sahihi kwangu na kwa mstakabali mzima wa familia yangu (watoto).
Katika harakati za maisha nimefanikiwa kukutana na dada, ambaye kwa mwonekano wa nje Angefaa sana kuwa mke wangu na mama wa watoto wangu, nikiri kuwa nilimpenda sana, bila shaka hata yeye kanipenda sana, kwa ufupi kaja kwangu nimeendelea kula mzigo dada kabeba ujauzito na anaelekea kujifungua.
Juzi hapa nikiwa kitandani nawaza mambo ya dunia, kwa upole na kwa hekima ya hali ya juu kaniingizia jambo ambalo ukweli limenitoa kwenye reli.
Kwa kutanguliza msamaha na kwa unyenyekevu wa hali ya juu kanieleza kuwa pindi akiwa chuo kuanzia second year hali ya maisha ilikuwa ngumu sana kwa upande wake kutokana na wazazi kutomtimizia mahitaji ya msingi (fedha ya chakula) kwani alisomeshwa na wazazi .
Hivyo kutokana na hali hiyo ilipelekea kuhama hosteli na kwenda kukaa kinyumba na mwanachuo mwenzake (mwanamme) mpaka kumaliza chuo kisha akaachana naye, huyo jamaa alikuwa na boom, hivyo basi kutokana na hali hiyo jambo hilo amekaa nalo moyoni kwa muda mrefu ila ameshindwa kuvumilia anaomba msamaha na kunisihi nimuamini katika maisha yake yote.
Niseme tu kwamba sijaongea chochote mpaka sasa, nimekosa cha kumjibu na hapa moyo wangu unarindima hasira isiyo na mfano, chakula hakipandi na nahisi kupaliwa na kila kiingiacho kinywani kwangu, kila adhabu nayowaza nahisi ni ndogo kwake.
Wakuu wenye hekima na busara naomba mawazo yenu, maake nahisi mi nimefika ukomo wa kuwaza zaidi ya kutaka kufanya maamuzi magumu na ya ovyo.