Sikuwa na mpango wa kuwa na Mtoto wa nje lakini huenda ikawa hivyo

Sikuwa na mpango wa kuwa na Mtoto wa nje lakini huenda ikawa hivyo

Wakuu kwema,

Moja kwa moja kwenye mada, katika maisha yangu nilijitunza sana ili kuhakikisha sizai hovyo na mwanamke ambaye sitamuoa na nihakikishe napata mwanamke sahihi kwangu na kwa mstakabali mzima wa familia yangu (watoto).

Katika harakati za maisha nimefanikiwa kukutana na dada, ambaye kwa mwonekano wa nje Angefaa sana kuwa mke wangu na mama wa watoto wangu, nikiri kuwa nilimpenda sana, bila shaka hata yeye kanipenda sana, kwa ufupi kaja kwangu nimeendelea kula mzigo dada kabeba ujauzito na anaelekea kujifungua.

Juzi hapa nikiwa kitandani nawaza mambo ya dunia, kwa upole na kwa hekima ya hali ya juu kaniingizia jambo ambalo ukweli limenitoa kwenye reli.

Kwa kutanguliza msamaha na kwa unyenyekevu wa hali ya juu kanieleza kuwa pindi akiwa chuo kuanzia second year hali ya maisha ilikuwa ngumu sana kwa upande wake kutokana na wazazi kutomtimizia mahitaji ya msingi (fedha ya chakula) kwani alisomeshwa na wazazi .

Hivyo kutokana na hali hiyo ilipelekea kuhama hosteli na kwenda kukaa kinyumba na mwanachuo mwenzake (mwanamme) mpaka kumaliza chuo kisha akaachana naye, huyo jamaa alikuwa na boom, hivyo basi kutokana na hali hiyo jambo hilo amekaa nalo moyoni kwa muda mrefu ila ameshindwa kuvumilia anaomba msamaha na kunisihi nimuamini katika maisha yake yote.

Niseme tu kwamba sijaongea chochote mpaka sasa, nimekosa cha kumjibu na hapa moyo wangu unarindima hasira isiyo na mfano, chakula hakipandi na nahisi kupaliwa na kila kiingiacho kinywani kwangu, kila adhabu nayowaza nahisi ni ndogo kwake.

Wakuu wenye hekima na busara naomba mawazo yenu, maake nahisi mi nimefika ukomo wa kuwaza zaidi ya kutaka kufanya maamuzi magumu na ya ovyo.
Ushauri wa bure: Amekuambia kwa sababu anahofia siku moja lisije kuibuka na mko familia ukaumia!! Wanaumie msiwe makatili hivi jamani....

Nakushauri muoe awe MKEO na sahau yaliyopita. Usije ukamwacha ukaenda kuona aliyetoa ujauzito kadhaa. Kikubwa fungeni ndoa acheni kumuudhi Maulana
 
Ahsante kwa ushauri.
 
nilidhani atakwambia ana mtoto kumbe ni ishu ya kuisho kinyumba chuo?

Mambo ya kawaida sana hayo na hata mabinti wa kishua tuliwaona wanaishi kinyumba na washkaji wa kawaida tu.

Hasira zako zipo wapi labda maana hawa mabinti kukuta hawajachakatwa ni kama kutafuta shilingi iliyodondoka sokoni.
 
Ushauri wa bure: Amekuambia kwa sababu anahofia siku moja lisije kuibuka na mko familia ukaumia!! Wanaumie msiwe makatili hivi jamani....

Nakushauri muoe awe MKEO na sahau yaliyopita. Usije ukamwacha ukaenda kuona aliyetoa ujauzito kadhaa. Kikubwa fungeni ndoa acheni kumuudhi Maulana
Mwanaume hasahau wala kusamehe bali anapotezea tu ila kwa mwanamke yeye anasamehe alafu kana siku atayafufua upyaaa
 
Ila huyo dada naye fala sana,atasemaje a negative past.Ila nawe umezidi,unamhukumu mtu wa past relationship?,hv ukija kumfumania utafanyaje ikiwa tu saa hiz msosi haupandi?...........Man Up!
 
Mkuu mpaka sasa sina majibu.
Mkuu hapo inaonyesha dhahiri huyo dada anakupenda sana, tena heshimu sana uamuzi wa yeye kukueleza hayo. Kafanya jambo la msingi sana mimi naona, kakueleza hali halisi ili apate kuwa huru kabisa.

kwanini nasema hivi? Just imagine, angekausha tu halafu itokee siku moja huna hili wala lile halafu ukutane na hizo habari kwa mtu wa nje anaemjua binti kwamba kipindi anasoma alikuwa anaishi hostel bubu (kaolewa kichuochuo) ungejisikiaje?

kakueleza sababu she give up everything she did before, kaamua kuanza safari mpya na wewe, kaamua kuwa huru. Hata ikitokea kuna siku zikakupata habari kama hizo hautokuwa suprised sababu tayari unajua..

Mkuu, nakusihi tu mpende huyo dada. Anapenda kuwa huru ndio maana kakueleza. Ingekuja kuwa case kubwa sana kama ungeyajua haya kutoka kwa mtu wa pembeni, muda huo ushachelewa. Just cool down and go on with that innocent lady
 
Ila huyo dada naye fala sana,atasemaje a negative past.Ila nawe umezidi,unamhukumu mtu wa past relationship?,hv ukija kumfumania utafanyaje ikiwa tu saa hiz msosi haupandi?...........Man Up!
Binti yupo honest ashukuru, mabinti karibu wote age 16 hadi 23 huwa wanachakatwa sana kwa mazingira tofauti.

Ni kawaida kabisa,
 
Back
Top Bottom