Sikuwahi kutegemea haya, hatimaye leo yamenikuta

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2023
Posts
6,799
Reaction score
22,209
Wakuu habari ya muda huu.

Sisi wengine kama ilivyo kwa wengi, hapa ndipo pa ku-share issues tunapohisi ku-release baadhi ya mambo yakituzidia.

Mchana wangu umeharibika ghafla sana.😅 Kulingana na tides za kibiashara safari hii (ofcourse ni mambo ya kawaida tu), landlord wangu hatimae leo kamvamia binti yangu ofisini na kumsihi amkabidhi funguo ya ofisi.
Na imekuwa kama coincidence maana this whole week sijatokea kabisa ofisini kwa kukimbizana na issue nje ya ofisi.

Yaani licha ya kulipa kodi kwa uaminifu siku zooote quarter hii biashara imeyumba nika delay 2 months.

Nimepigiwa simu na binti yangu na kiukweli nikaona isiwe ishu, nimempa maelekezo machache tu ili kusudi shughuli zisikwame. Kichwa kisha jam hiki. Let me clear my mind first, nitayawaza badae.
😅😅.
1000140220.jpg
 
Wakuu habar ya muda huu.

Sisi wengine kama ilivyo kwa wengi, hapa ndipo pa ku share issues tunapohis ku release baadh ya mambo yakituzidia.
Mkuu pole sana kwa hiyo changamoto. Wengine ambao hawajawahi kukutana na kadhia ya kufunga ofisi wanaweza wasikuelewe, ni maumivu makubwa sana.

Ulifanyia kazi ushauri wangu wa kuweka lile wazo lako hapa? Unaona kama leo umeweza kushare hili hapa kwanini lile ambalo ni la ufumbuzi endapo watu wangekuunga mkono usiliweke hapa pia?
 
Kwenye utafutaji haya matukio ni kawaida kukutana nayo, tena mengine magumu zaidi ya hilo.

Kikubwa piga moyo konde kesho nayo ni siku, sali mshukru Muumba wako kisha move on.

Usijilaumu wala kuilamu nafsi yako, mapito yako kwa ajili ya watu na watu ndo mimi na wewe.

Endelea kupambana kiongozi, usife moyo kesho yako ni njema
 
Wakuu habar ya muda huu.

Sisi wengine kama ilivyo kwa wengi, hapa ndipo pa ku share issues tunapohis ku release baadh ya mambo yakituzidia.

Mchana wangu umeharinika ghafla sana.😅 Kulingana na tides za kibiashara safari hii (ofcourse ni mambo ya kawaida tu), landlord wangu hatimae leo kamvamia binti yangu ofisini na kumsihi amkabidhi funguo ya ofisi.
Na imekua kama coisedence maana this whole week sijatokea kabisa ofisini kwa kukimbizana na issue nje ya ofisi.

Yan licha ya kulipa kodi kwa uaminifu siku zooote quarter hii biashara imeyumba nika delay 2 months.

Nimepigiwa simu na binti yangu na kiukwel nikaona isiwe ishu nimempa maelekezo machache tu ili kusudi shughuli zisikwame. Kichwa kisha jam hiki. Let me clear my mind first, nitayawaza badae.I
😅😅.
View attachment 3003640
Swali fikirishi je Huwa hupokei simu za mwenye numba? (Landlord),km Ndiyo Hilo ni kosa maswali mengine baadae
 
Pole sana mkuu.
Shida kubwa kwa wengi huwa akidaiwa anamkimbia mdai, anakwepa mawasiliano, sisemi wewe umefanya hivi, ila wengi wanakuwa waoga kuongea na wadai wao, akidhani kumkimbia ndio dawa. Kumbe ni kimyume kabisa. Unatakiwa kuwa muwazi na pengine hata wewe kuwahi kumwambia shida yako ya kukuchelewesha kulipa deni kabla hajakuuliza au muda kufika. Ukifanya hivyo mara nyingi utapunguza matatizo kama haya.Mimi nimewahi kuona jamaa anadaiwa halafu katika kudaiwa, mdai akamkopesha tena jamaa zaidi. Ni lugha tu nzuri.
 
Pole saan mkuu. Miezi hii migumu balaa halafu shida zinatofautiana tu ila biashara Zina changamoto sana.
Sisi wengine tunaobangaiza kwenye biashara ya usafirishaji tunakiona cha moto sabbu abiria hakuna halafu polisi Kila geti wanataka hela.
Yaani utenge elfu sitini kila siku ya mapolisi tu kwa mwezi 1.8 mil sijui huu uonevu katika nchi hii utaisha lini. Ttanzania mazingira ya kufanya biashara magumu sana.
 
Back
Top Bottom