Sikuwahi Muona mtu akiingia JF, JF kuna nani??

Sikuwahi Muona mtu akiingia JF, JF kuna nani??

Mkuu embui angalia mm na wewe nani wa kwanza kujiunga humuu!!
tena hii ni ID mpyaa, ukitaka nakupa ya 2010
Umenikumbusha ID yangu ya kwanza kabisa nahisi ilikuwa 2008 au 2009. Member ambaye ni mfanyakazi mwenzangu alinishauri nijiunge. kwanza nikawa nasoma tu comments za watu ila siwezi kuchangia. Baada ya muda nikajiunga ila ID yangu ilikuwa na jina langu kabisa. Post yangu ya kwanza kwenye mjadala wa kisiasa nikamwaga nyongo ya kutosha dhidi ya serikali. jamaa alipoiona ikabidi anieleze kuwa inatakiwa niweke ID isiyonitambulisha kabisa. Kuanzia hapo nikajizuia kutoa comments zozote, nikawa msomaji tu.

Ila kipindi cha uchaguzi mkuu (mara tu baada) uzalendo ukanishinda, maana nilikuwa na mahasira nisingeweza kusoma tu bila kuwajibu binadamu wa mrengo mwingine. Nikajisajili upyaaaaaaaa, na ile ID nadhani ilishapotelea mbali.
 
Kutokujuana inasaidia mtu kuwa huru na kuchangia chochote anachojisikia au anachoamini.
Chukulia mfano katika jukwaa la MMU jinsi watu wanavyochangia halafu uwe unamjua mtu na michango yake ni sheedah huoni utaanza kumchukulia tofauti?
Au gf wako yupo humu akachangia unaweza umwache kwasababu ya comments tu pia unaweza kumdharau mtu kwasababu ya jinsi anavyochangia au kumchukia
Inaleta raha na uhuru na ndio raha ya kuwa nyuma ya id fake
Hiyo ni kweli alafu kuna wakati mtu anaweza akaweka comment yake ukajibu kwa dharau au kumdhihaki sasa uje umjue unakuta ni mtu wa makamo na heshima zake alafu wewe ni kijana mdogo tu.
 
Huwa nashangaa sana nikija kila jukwaa na kuta reply na views kibaooooooo.

Nikitazama marafiki zangu ninaosoma nao, wachizi maskani na ndugu zangu hakuna anayefuatilia JF.

Sikuwahi mfumania mtu akipost kitu humuuu lakini ukiingiaa unakuta reply kama 500. Nimewahi kumsaidia broo kazi yake ya Internat cafe kwa muda wa wiki Moja sijawahi ona mtu akiingia JF.

Nilijaribu kuwauliza washkaji na madem tuliokuwatunafanya field sehemu moja kama wanaujua huu mtandao wengi walikuwa hawaujui ina mmoja ndiye alisema yeye huwa anasomaga tu post ila hachangiiiiii.

Kademu kangu ndo juzi ninakaona kanaaanza kufatilia, nafikiri huyu ndiye atakuwa wa kwanzaaaa..

Mi nauliza nyie mliopo humu mpo wapi? Mna comments mkiwa uvunguni nisiwaoneeeeee?? Na huwa mnacomments saa ngapiiiiii??

Natamani kumuona angalau memba mmoja kwa macho yangu nijue na ka ID kakeee bhanaaaaaa

Aggghhh!!!
Kwa hiyo wewe siku ukifa hakuna wa kutoa habari zako? Mie mentor na Kiagata watawajulisha na ikitokea wao wakatangulia nitawajulisha pia.
 
Umuone mtu anapost ili..??
Kwanza pitia hizo profile name.. Halafu ujihulize ilikupasa uanze lipi la kujihoji..??
 
Huwa nashangaa sana nikija kila jukwaa na kuta reply na views kibaooooooo.

Nikitazama marafiki zangu ninaosoma nao, wachizi maskani na ndugu zangu hakuna anayefuatilia JF.

Sikuwahi mfumania mtu akipost kitu humuuu lakini ukiingiaa unakuta reply kama 500. Nimewahi kumsaidia broo kazi yake ya Internat cafe kwa muda wa wiki Moja sijawahi ona mtu akiingia JF.

Nilijaribu kuwauliza washkaji na madem tuliokuwatunafanya field sehemu moja kama wanaujua huu mtandao wengi walikuwa hawaujui ina mmoja ndiye alisema yeye huwa anasomaga tu post ila hachangiiiiii.

Kademu kangu ndo juzi ninakaona kanaaanza kufatilia, nafikiri huyu ndiye atakuwa wa kwanzaaaa..

Mi nauliza nyie mliopo humu mpo wapi? Mna comments mkiwa uvunguni nisiwaoneeeeee?? Na huwa mnacomments saa ngapiiiiii??

Natamani kumuona angalau memba mmoja kwa macho yangu nijue na ka ID kakeee bhanaaaaaa

Aggghhh!!!
Kukomenti kwetu ni kama mapenzi ya paka, hatuonekani.. ukituona uchuro...

HALAFU HATA WEWE ULIPOKUWA UNAANDIKA HII THREAD SISI HATUKUKUONA NA HATUJALALAMIKA..
 
Social medias zina level..facebook inawatu wa level flan (watoto) istagram imejaa mabishoo..JF inagreat thinkers..kwahyo we bado unakua kimawazo..ukifika level flani itabidi uachane na FB na Insta..uwe Expert member wa JF
Haswaaaa!!!!
 
Hahahah aisee we jamaa umeongea mawazo yang kabisa. Binafsi JF nilianza kuipenda bila kushawishiwa na mtu ni kama zali tu nikajikuta addict wa JF lakini chakushangaza ndugu, jamaa na marafiki zangu wote nikiwauliza kama wanapitaga humu hakuna ata mmoja mwenye mpango nayo. Alaf pia JF inavichwa kinoma natamani nikutane uso kwa macho na member kadhaa ila nahisi watakuwa feki
Nikweli kuna wa humu wana upeo zaid ya akili na vyeti vyako kaa mbali....kama jamaa Fulani hv yaani daaah!!!
 
Back
Top Bottom