Mtoa post kama vile upo akilini mwangu, nami huwa najiuliza hili swali lakini naishia kushangaa tu. Hapa kazini kwangu tupo hamsini na nne lakini sijawahi kuona mtu akijishighulisha jamii forums, zaidi wanapenda kuingia insta, whatsap na FB ila nimejitahidi kupiga debe watu wajiunge nimeambulia wawili tu na wenyewe wanaingia dakka sifuri wanatoka. Ila nimegundua watu wanaojiunga jf na kuchangia mada mbalimbali au kuzianzisha ni watu wenye fikra pana sana, wanaotaka kujua vitu kwa upana zaidi. Binafsi kama sina kazi ya kujishughulisha siwezi kaa hata dakika tano bila kuingia JF. Namshukuru sana mgunduzi wa JF