Silaha mpya ya nyuklia ya Marekani yaleta tishio zaidi kwa ustaarabu wa binadamu

Silaha mpya ya nyuklia ya Marekani yaleta tishio zaidi kwa ustaarabu wa binadamu

Baada ya kuandika na kujadili yote haya ...
Turudi kufanya kazi za kuvuja jasho
Si utani
Hebu nipe gharama, nina simu yangu iko kwa android 7 , nahitaji ifanyiwe flash halafu kuiroot ili uweze kupigwa window ili ikiwashwa itoe logo ya samsung note 20......
 
Wangeanza kuzitumia sasa ili tuelewe zinafanyaje kazi na tuone zipi nzuri na zipi mbaya.
 
Wapo vzr kuweka vitisho kwa nchi masikini, na kwa maoni yetu wanapata majibu wao kama taifa wanazungumziwaje kwenye Dunia ya ushindani wa nguvu ya kivita? Tuendelee kuwapa wanayo stahili
 
View attachment 3341714Wizara ya Nishati ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kukamilika kwa utengenezaji wa bomu jipya la nyuklia aina ya B61-13. Wakati dhana ya jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu inazidi kukubaliwa duniani, Marekani inaenda kinyume na kutishia usalama wa binadamu wote kwa kuboresha silaha zake za nyuklia.
Ripoti inasema B61-13 lilitengenezwa katika msingi wa bomu la awali aina ya B61-12, lakini lina uwezo mkubwa zaidi ikiwemo kuangamiza maeneo lengwa yaliyoko chini ya ardhi. Licha ya hayo B61-13 lina nguvu mara 21 zaidi ya bomu la nyukilia lililoshambulia mji wa Hiroshima, Japan mwaka 1945 wakati wa Vita Vikuu vya Pili Duniani.
Tukiangalia kitabu cha historia cha silaha za nyuklia cha Marekani, tutagundua kuwa kila ukurasa umejaa damu na moto. Marekani ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuunda silaha za nyuklia na kufungua sanduku la Pandora. Pia ilikuwa nchi ya kwanza duniani kurusha bomu la nyuklia kwenye jiji wanaloishi binadamu, na kusababisha malaki ya vifo. Aidha, Marekani pia ilifanya mashindano ya silaha za nyuklia na Umoja wa Sovieti, na kuunda mabomu mengi ya nyuklia yanayoweza kuangamiza dunia mara kadhaa. Aina mpya ya silaha ya nyukilia B61-13 ni mfano mpya wa Marekani kutojali usalama wa binadamu wote.
Wazimu wa Marekani kuunda mabomu ya nyuklia unatokana na maslahi ya mashirika ya silaha nchini humo. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, mwaka huu bajeti ya kijeshi ya Marekani imefikia dola bilioni 886 za Kimarekani, na itaongezeka hadi zaidi ya trilioni moja mwaka ujao. Kati ya fedha hizo, nyingi zitatumiwa katika kuendeleza silaha kali zaidi za nyuklia. Mashirika makubwa ya silaha nchini marekani kama vile Lockheed Martin na Northrop Grumman yanatumia vikundi vya ushawishi ili kufanya mikakati ya kinyukilia ya Marekani kuwa njia yao ya kujipatia faida.
Kinachoshangaza zaidi ni kwamba wakati Marekani inaendeleza silaha zake za nyuklia kwa nguvu kubwa, inaendelea kuzinyooshea kidole nchi nyingine juu ya suala la nyuklia. Hivi karibuni Marekani imeipaka matope China, ikidai kwamba idadi ya mabomu ya nyuklia ya China inaongezeka kwa kasi, na kufanya Marekani “kushindwa kulala usiku”. Lakini ukweli ni kwamba Marekani ina zaidi ya mabomu 3,700 ya nyuklia yanayoweza kufanya kazi. Na idadi hii ni zaidi ya mara sita kuliko ile ya China. Aidha, kuna tofauti kubwa kati ya mikakati ya China na Marekani. Awali China ililazimika kuunda silaha za nyuklia kutokana na vitisho vya nyukilia vilivyoletwa na Marekani na Umoja wa Soviet. Hata sasa mkakati wa nyukilia wa China ni kujilinda. Kwani China imeahidi kutozitumia silaha za nyukilia kwanza, na kutozitumia dhidi ya nchi zisizo na silaha za nyuklia.
Lakini kwa upande wa Marekani, kinyume na China, mkakati wake wa nyuklia ni kutumia silaha za nyuklia kwanza katika hali yoyote. Hatari ya mkakati huu ni wazi, na inaongeza sana vitisho kwa binadamu wote. Bomu jipya la nyuklia la Marekani B61-13 ni uthibitisho mpya wa mkakati huo. Bomu hilo linaweza kubebwa na ndege zisizoonekana kirahisi kwenye rada aina za B-2 na B-21, na kufanya shambulizi kwanza dhidi ya maeneo lengwa muhimu ya maadui hata yale yaliyoko chini ya ardhi.
Chini ya sintofahamu hizi za ustaarabu wa binadamu, wanasiasa wa Marekani wanapaswa kuelewa kwamba silaha za nyuklia sio medali ya hadhi kubwa ya nguvu, bali ni “upanga wa Damocles” unaoning’inia juu ya vichwa vya binadamu wote. Siku moja wakati B61-13 litakaporushwa angani, halitaleta usalama kwa nchi yoyote, bali litaangamiza ustaarabu wote wa binadamu.
Jifunze kuandika kwa paragraph.

Halafu nguvu ya marekani ni uwezo wake wa kushambulia na kujilinda dhidi ya maadui.
 
Kwanini hiko kipande kimoja cha bomu kisidondoshwe pale Gaza?
Hayo ndio mawazo yao kwahio umelenga mule mule Kuna kiongozi wa wamarekani ametoa wazo hilo ili kuwasarenda hamas kama Walivyofanya kuwasarenda waJapan. Kilichotokea Iran akaongeza urutubishaji ili kuwatoa kwenye mstari jumlisha na zile True promise wakaona ata Iran ashughulikiwe kwanza. Sasa fuoa ndio lipo apo Iran hatakiwi kua na bomu ili muda wowote wafanye unyama wao
 
Si utani
Hebu nipe gharama, nina simu yangu iko kwa android 7 , nahitaji ifanyiwe flash halafu kuiroot ili uweze kupigwa window ili ikiwashwa itoe logo ya samsung note 20......
Mkuu jaribu kuwa seriously basi..
Mi mbona comment yangu haifanani na haya maneno yako...

Unataka kusema kuvuja jasho ndo huku
 
Hongera sana Marekani, endelea kutulinda dhidi ya uzombi wa makobaz.
 
Ulimwengu umejaa mambo ya kuajabisha...
Yeye anazitengeneza na kuziboresha kila siku, ajabu hataki wenzie wawe nayo, na akisika wanamawazo ya aina hiyo ananunaa
 
Ulimwengu umejaa mambo ya kuajabisha...
Yeye anazitengeneza na kuziboresha kila siku, ajabu hataki wenzie wawe nayo, na akisika wanamawazo ya aina hiyo ananunaa

Makobaz msiachiwe mumiliki chochote chenye maangamizi, hamkawii kujilipua.
Acheni Mmarekani amiliki na kuendelea kutulinda dhidi yenu.
 
Makobaz msiachiwe mumiliki chochote chenye maangamizi, hamkawii kujilipua.
Acheni Mmarekani amiliki na kuendelea kutulinda dhidi yenu.
Nini maana ya kobazi?? Na kuna uhusiano gani kati ya nlichoandika na neno kobazi??
Nieleweshe tafadhari
 
Wanatengeneza ila hawazitumii, wangejaribia hata Tanzania basi
Inaitwa detterance.

Mfano Watu wote ambao wana bifu na Marekani au Israel hupenda kuonesha Silaha na Majeshi yao, lengo ni kumfanya adui yako ashindwe kuamua akupige au akuache kwanza..

Ndio maana unaona Israel huwa anawapiga maadui zake licha ya mikwara yao
 
Ulimwengu umejaa mambo ya kuajabisha...
Yeye anazitengeneza na kuziboresha kila siku, ajabu hataki wenzie wawe nayo, na akisika wanamawazo ya aina hiyo ananunaa
Ni hekima kumdhibiti kichaa mwenye panga kwa kutumia panga ili kumnyanganya panga, ndiyo sababu watoto hawapaswi kuwa na ndevu, wasije wakajikata wakati wa kuzinyoa,, imagine leo alshabab wawe na uwezo wa kuunda nyuklia, nani atapona?
 
Back
Top Bottom