Silaha mpya ya nyuklia ya Marekani yaleta tishio zaidi kwa ustaarabu wa binadamu

Ni hekima kumdhibiti kichaa mwenye panga kwa kutumia panga ili kumnyanganya panga, ndiyo sababu watoto hawapaswi kuwa na ndevu, wasije wakajikata wakati wa kuzinyoa,, imagine leo alshabab wawe na uwezo wa kuunda nyuklia, nani atapona?
Yupi kichaa wa kudhibitiwa ? Je ni yule anaelimiliki na ameishawahi kulitumia kuangamiza watu na bado anamiliki akizidi kuliboresha?? Au yule ambae hana zinabaki husia akimiliki ataangamiza watu??
 
Nchi iliyowahi kuyatumia hayo mabomu ni wao wenyewe wamarekani.

Hata zama hizi naamini iko siku litatumika hata kwa bahati mbaya ili nasi tuone na kujifunza.
 
View attachment 3341714Wizara ya Nishati ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kukamilika kwa utengenezaji wa bomu jipya la nyuklia aina ya B61-13. Wakati dhana ya jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu inazidi kukubaliwa duniani, Marekani inaenda kinyume na kutishia usalama wa binadamu wote kwa kuboresha silaha zake za nyuklia.
Ripoti inasema B61-13 lilitengenezwa katika msingi wa bomu la awali aina ya B61-12, lakini lina uwezo mkubwa zaidi ikiwemo kuangamiza maeneo lengwa yaliyoko chini ya ardhi. Licha ya hayo B61-13 lina nguvu mara 21 zaidi ya bomu la nyukilia lililoshambulia mji wa Hiroshima, Japan mwaka 1945 wakati wa Vita Vikuu vya Pili Duniani.
Tukiangalia kitabu cha historia cha silaha za nyuklia cha Marekani, tutagundua kuwa kila ukurasa umejaa damu na moto. Marekani ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuunda silaha za nyuklia na kufungua sanduku la Pandora. Pia ilikuwa nchi ya kwanza duniani kurusha bomu la nyuklia kwenye jiji wanaloishi binadamu, na kusababisha malaki ya vifo. Aidha, Marekani pia ilifanya mashindano ya silaha za nyuklia na Umoja wa Sovieti, na kuunda mabomu mengi ya nyuklia yanayoweza kuangamiza dunia mara kadhaa. Aina mpya ya silaha ya nyukilia B61-13 ni mfano mpya wa Marekani kutojali usalama wa binadamu wote.
Wazimu wa Marekani kuunda mabomu ya nyuklia unatokana na maslahi ya mashirika ya silaha nchini humo. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, mwaka huu bajeti ya kijeshi ya Marekani imefikia dola bilioni 886 za Kimarekani, na itaongezeka hadi zaidi ya trilioni moja mwaka ujao. Kati ya fedha hizo, nyingi zitatumiwa katika kuendeleza silaha kali zaidi za nyuklia. Mashirika makubwa ya silaha nchini marekani kama vile Lockheed Martin na Northrop Grumman yanatumia vikundi vya ushawishi ili kufanya mikakati ya kinyukilia ya Marekani kuwa njia yao ya kujipatia faida.
Kinachoshangaza zaidi ni kwamba wakati Marekani inaendeleza silaha zake za nyuklia kwa nguvu kubwa, inaendelea kuzinyooshea kidole nchi nyingine juu ya suala la nyuklia. Hivi karibuni Marekani imeipaka matope China, ikidai kwamba idadi ya mabomu ya nyuklia ya China inaongezeka kwa kasi, na kufanya Marekani “kushindwa kulala usiku”. Lakini ukweli ni kwamba Marekani ina zaidi ya mabomu 3,700 ya nyuklia yanayoweza kufanya kazi. Na idadi hii ni zaidi ya mara sita kuliko ile ya China. Aidha, kuna tofauti kubwa kati ya mikakati ya China na Marekani. Awali China ililazimika kuunda silaha za nyuklia kutokana na vitisho vya nyukilia vilivyoletwa na Marekani na Umoja wa Soviet. Hata sasa mkakati wa nyukilia wa China ni kujilinda. Kwani China imeahidi kutozitumia silaha za nyukilia kwanza, na kutozitumia dhidi ya nchi zisizo na silaha za nyuklia.
Lakini kwa upande wa Marekani, kinyume na China, mkakati wake wa nyuklia ni kutumia silaha za nyuklia kwanza katika hali yoyote. Hatari ya mkakati huu ni wazi, na inaongeza sana vitisho kwa binadamu wote. Bomu jipya la nyuklia la Marekani B61-13 ni uthibitisho mpya wa mkakati huo. Bomu hilo linaweza kubebwa na ndege zisizoonekana kirahisi kwenye rada aina za B-2 na B-21, na kufanya shambulizi kwanza dhidi ya maeneo lengwa muhimu ya maadui hata yale yaliyoko chini ya ardhi.
Chini ya sintofahamu hizi za ustaarabu wa binadamu, wanasiasa wa Marekani wanapaswa kuelewa kwamba silaha za nyuklia sio medali ya hadhi kubwa ya nguvu, bali ni “upanga
wa Damocles” unaoning’inia juu ya vichwa vya binadamu wote. Siku moja wakati B61-13 litakaporushwa angani, halitaleta usalama kwa nchi yoyote, bali litaangamiza ustaarabu wote wa binadamu.
Hizo tactical gravity nuclear Bombs siyo mabom mapya yanakuwa upgraded tu, na yalikuwa yana hifadhiwa kwenye maghara ya air bases za USA barani Ulaya, waliyaondoa Barani Ulaya na Turkey. kwenye mwishoni mwa miaka ya sabini kama sikosei.

Kitu kingine mbona hata Warusi wanazo type ya mabom kama hayo mengi tu.

Kama unavyo sema USA ikileta mchezo kwa kutishia watu au kuzitumia kikweli kweli basi wakae wakijua kwamba kama unavyo sema upanga wa Domacles bado utaendelea kuning'inia kwenye shingo la kila kiumbe hapa Duniani bila kujali anatoka Taifa gani, race gani au status gani.

Kadri miaka inavyo kwenda ndiyo Dunia inavyo sogelea upanga huo hatari, labda Mungu aingilie KATI kabla mambo hayaja anza kuharibika beyond repair.
 
View attachment 3341714Wizara ya Nishati ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kukamilika kwa utengenezaji wa bomu jipya la nyuklia aina ya B61-13. Wakati dhana ya jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu inazidi kukubaliwa duniani, Marekani inaenda kinyume na kutishia usalama wa binadamu wote kwa kuboresha silaha zake za nyuklia.
Ripoti inasema B61-13 lilitengenezwa katika msingi wa bomu la awali aina ya B61-12, lakini lina uwezo mkubwa zaidi ikiwemo kuangamiza maeneo lengwa yaliyoko chini ya ardhi. Licha ya hayo B61-13 lina nguvu mara 21 zaidi ya bomu la nyukilia lililoshambulia mji wa Hiroshima, Japan mwaka 1945 wakati wa Vita Vikuu vya Pili Duniani.
Tukiangalia kitabu cha historia cha silaha za nyuklia cha Marekani, tutagundua kuwa kila ukurasa umejaa damu na moto. Marekani ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuunda silaha za nyuklia na kufungua sanduku la Pandora. Pia ilikuwa nchi ya kwanza duniani kurusha bomu la nyuklia kwenye jiji wanaloishi binadamu, na kusababisha malaki ya vifo. Aidha, Marekani pia ilifanya mashindano ya silaha za nyuklia na Umoja wa Sovieti, na kuunda mabomu mengi ya nyuklia yanayoweza kuangamiza dunia mara kadhaa. Aina mpya ya silaha ya nyukilia B61-13 ni mfano mpya wa Marekani kutojali usalama wa binadamu wote.
Wazimu wa Marekani kuunda mabomu ya nyuklia unatokana na maslahi ya mashirika ya silaha nchini humo. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, mwaka huu bajeti ya kijeshi ya Marekani imefikia dola bilioni 886 za Kimarekani, na itaongezeka hadi zaidi ya trilioni moja mwaka ujao. Kati ya fedha hizo, nyingi zitatumiwa katika kuendeleza silaha kali zaidi za nyuklia. Mashirika makubwa ya silaha nchini marekani kama vile Lockheed Martin na Northrop Grumman yanatumia vikundi vya ushawishi ili kufanya mikakati ya kinyukilia ya Marekani kuwa njia yao ya kujipatia faida.
Kinachoshangaza zaidi ni kwamba wakati Marekani inaendeleza silaha zake za nyuklia kwa nguvu kubwa, inaendelea kuzinyooshea kidole nchi nyingine juu ya suala la nyuklia. Hivi karibuni Marekani imeipaka matope China, ikidai kwamba idadi ya mabomu ya nyuklia ya China inaongezeka kwa kasi, na kufanya Marekani “kushindwa kulala usiku”. Lakini ukweli ni kwamba Marekani ina zaidi ya mabomu 3,700 ya nyuklia yanayoweza kufanya kazi. Na idadi hii ni zaidi ya mara sita kuliko ile ya China. Aidha, kuna tofauti kubwa kati ya mikakati ya China na Marekani. Awali China ililazimika kuunda silaha za nyuklia kutokana na vitisho vya nyukilia vilivyoletwa na Marekani na Umoja wa Soviet. Hata sasa mkakati wa nyukilia wa China ni kujilinda. Kwani China imeahidi kutozitumia silaha za nyukilia kwanza, na kutozitumia dhidi ya nchi zisizo na silaha za nyuklia.
Lakini kwa upande wa Marekani, kinyume na China, mkakati wake wa nyuklia ni kutumia silaha za nyuklia kwanza katika hali yoyote. Hatari ya mkakati huu ni wazi, na inaongeza sana vitisho kwa binadamu wote. Bomu jipya la nyuklia la Marekani B61-13 ni uthibitisho mpya wa mkakati huo. Bomu hilo linaweza kubebwa na ndege zisizoonekana kirahisi kwenye rada aina za B-2 na B-21, na kufanya shambulizi kwanza dhidi ya maeneo lengwa muhimu ya maadui hata yale yaliyoko chini ya ardhi.
Chini ya sintofahamu hizi za ustaarabu wa binadamu, wanasiasa wa Marekani wanapaswa kuelewa kwamba silaha za nyuklia sio medali ya hadhi kubwa ya nguvu, bali ni “upanga wa Damocles” unaoning’inia juu ya vichwa vya binadamu wote. Siku moja wakati B61-13 litakaporushwa angani, halitaleta usalama kwa nchi yoyote, bali litaangamiza ustaarabu wote wa binadamu.
Mkuu kumbuka kwamba hilo ni tactical Nuclear BOM silo la kuangamiza Dunia nzima!!
 
Back
Top Bottom