Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
SILAHA YA MASIKINI NI UNAFIKI
Kwa Mkono wa Robert Heriel
Uzoefu wangu unanieleza jambo hili. Na nimeshalithibitisha kwa yakini kuwa Silaha namba moja kabisa ya Mtu masikini ni Unafiki.
Umasikini upo wa namna mbalimbali, upo umasikini wa kiuchumi, umasikini wa kifikra, umasikini wa Kiroho miongoni mwa aina zingine za umasikini.
Lakini aina zote huunganishwa na sifa kuu ya UNAFIKI ambao ndio silaha kubwa,
Masikini hajiamini pasipo unafiki, silaha ya unafiki ndio humfanya masikini kujiamini.
Unafiki wa umasikini huondoka pale anapokuwa na watu anaowazidi, pia Unafiki wa Masikini huondoka baada ya kutajirika kama sio Kufa kabisa.
Masikini akipata matako hulia Mbwata! Pia wakati mwingine matako Hulia mbutuu!
Masikini usimpe cheo atatesa wenzake, atakuwa mbinafsi na kujishibisha pekee yake. Atabambikizia wenzake kesi kwa sababu za kihuni kabisa. Masikini akipewa cheo hujigeuza mungu, Masikini asipewe cheo. Masikini! Masikini! Masikini silaha yake Unafiki.
Masikini akikupenda usimuamini wala usifurahie sana.
Masikini akikuchukia usimzingatie, kwa maana yeye hakuchukii wewe bali anachukia hali yako. Hali yako ikibadilika na kuwa nafuu utashangaa analeta mazoea. Masikini hawapendani ila kwa unafiki.
Kwenye masikini 100, basi 90 ni wanafiki. Kumi tuu ndio watakuwa wapo halisi.
Masikini ndoto yao kubwa wakiwa matajiri ni kulipa kisasi, kukomesha, kutamba na kusumbua wengine.
AINA ZA UNAFIKI WA MASIKINI
1. Unafiki wa Masikini kwa Masikini
2. Unafiki wa Masikini kwa Matajiri.
1. Unafiki wa masikini kwa Masikini
Huu ni umasikini ambapo masikini humwekea unafiki masikini mwenzake hasa yule anayeonyesha kuhangaika kujinasua na umasikini. Kama vile; Unaweza ukawa unahangaika kupambana na maisha ili uwe na unafuu wa maisha, uwapo mbele za masikini wenzako wanakupongeza na kukupa moyo lakini ukiwapa mgongo wanakusengenya, wanakuundia zengwe, wanakufanyia fitna. Kumbuka watu hawa ni watu wako wa karibu kabisa.
Unafiki huu upo maeneo ya uswahilini, vijiweni, na maeneo yote yenye watu wa hali ya chini. Sio ajabu mambo ya uchawi na ushirikina yakahusishwa ili usifanikiwe.
2. Unafiki wa Masikini dhidi ya matajiri
Huu ni unafiki ambao masikini hujipendekeza kwa maslahi yao. Unafiki huu sema hautokei mara kwa mara kwa sababu ya uchache wa matajiri ndani ya jamii yetu. Hata hivyo Siku hizi kumekuwa na Ongezeko la Masikini Jeuri, ambao kw alugha inayoeleweka tunawweza kuwaita WANAFIKI JEURI.
Mnafiki sharti awe na Rafiki wengi, mtu yeyote mwenye marafiki wengi ana sifa ya unafiki. Masikini hawezi epuka sifa hii kutokana na sababu kuwa wingi wa marafiki kwao una manufaa ulinganisha na Matajiri
Kupendwa na Masikini wengi lazima uwe na tahadhari kubwa sana, kwani masikini hawapendagi mtu isipokuwa hali na vitu vya mtu.
Namna bora ya kuondokana na Umasikini ni Kujitambua, kujipenda, kuthamini kazi uifanyayo na kuipenda ili iweze kukupa baraka.
Masikini wengi hawajitambui, hawajipendi, hawathamini wala kupenda kazi wazifanyazo, isipokuwa wanapenda visivyo vyao, sio ajabu masikini wakawa watu wa vijicho na husda.
Kwa bahati nzuri mimi mwenyewe ni Masikini na nipo kwenye jamii Masikini, hivyo isije onekana nawasema kundi fulani nisilokuwepo.
Masikini tufanye kazi, tuache majungu, tuache unafiki.
Kwa yeyote iliyomuuma atanisamehe ingawaje najua masikini msamaha wao ni wakinafiki. Wanajifanya wanasamehe alafu wanakusubiria siku ukipata anguko uone watakavyochekelea 😀😀😀😀.
Utasikia wakisema Afadhali, alikuwa akijidai sana, alikuwa anatusumbua, alikuwa mjuaji, na maneno mengi kama hayo.
Akitoboa utasikia tena; Tulijua lazima atoboe, mtoto wetu huyo jamani tumsapoti, Yaani anafanya kazi sana ni haki yake, tulikuwa tunamuombea 😀😀😀 muache kujiombea wenyewe shida zenu muombee watu. Masikini bhana kwa Unafiki hawajambo.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mvomero. Morogoro