Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Ukiona nchi uchumi wake ni duni,ujue haiwezi kuwa na jeshi imala,
 
Urusi hajatumia silaha mpya kwa sababu hana.
T14 Armata Elungata dudus
 
Pentagon wanatabia ya kufanya hadaa sana nakumbuka Kuna kipindi mkuu wa majeshi aliwahi kusema Kiev inaweza kuanguka ndani ya siku tatu lakini kilichotokea wote tumeona.
 
Na ukute ni graduate,hii nchi Ina shida sana
Usisumbuliwe na bias ya mtu kuwa graduate au la, wewe amini facts bila kujali kama facts hizo zinatoka kwa layman au zinatokwa kwa intellectual. Kuna watu wengine ukiwaambia elimu ya juu ni kama unawaambia kabila lao, na kuna wengine (kama wewe) wanadhani elimu ya juu ni muujiza!
 
Kinzhal kweli mashabiki wa Urusi wanaitaja sana wakati haina maajabu. Kwanza ina warhead ndogo kutokana na shape yake, pili ina gharama sana kutengeneza na makadirio ni kwamba Kinzhal moja inagharimu around $100 million na kwa vile haina nuclear warhead basi haina maana sana kuitumia kwenye target zisizo na gharama kubwa au umuhimu mkubwa.

Ni bora watumie Kalibr kadhaa kutoka kwenye meli au submarines hata missiles mojawapo ya hizo zikiwa shot down ila nyingi zitapenya na kufanya shambulizi, hapo gharama ni kidogo na mlipuko ni mkubwa. Au kwa angani watumie hizo jamii ya Raduga. Kinzhal ingekuwa ni anti ship hapo ingekuwa na maana sana ila ingehitaji kuwa na range kubwa au kuwa launched na stealth jet tena ikiwa kwenye internal weapons bay.

Avangard ni vigumu kuwa intercepted ila inapachikwa kwenye ballistic missile na kutumika kwenye terminal phase. Ni zaidi ya MIRVs ambazo nazo kwa speed yake ni vigumu kuzizuia ila Avangard glide vehicle ina advantages nyingine. Wako kwenye development ya Poseidon nuclear powered torpedo yenye nuclear warhead, ina unlimited range alafu ni autonomous. Pia wanajaribu kutengeneza Burevestnik itakayokuwa nuclear powered cruise missile na yenye unlimited range. Ila na hizi sanctions wanachelewa miaka
 
Sidhani elimu ya juu ni miujiza,ni Jambo la kawaida hasa kwa Tanzania ya leo,kinachonikwaza ni hao wasomi kuwa wajinga licha ya kukaa darasani kwa walau miaka 16
 
Dah!...unataka tumiliki S-300 ?, Tuna adui gani wa kutisha mpaka tujihami hivyo ?
T14 Armata Tsh Nyamizi britanicca TUJITEGEMEE mohamedidrisa789
wa kupuliza
 
Kama elimu ya juu ni jambo la kawaida kwako, kwa nini uliweke mbele hata katika mijadala ambayo haihitaji elimu ya juu.
Suala la silaha tpdf ni suala la elimu,yaani hata ukiwa la Saba unajua kwamba tpdf wanajua umuhimu wa ku-update silaha,na kwa kuwa itakuwa mfuatiliaji wa hotuba za rais hasa siku ya sherehe za Uhuru,itakua umekutana na hotuba za Tambo za uboreshaji jeshi kwa silaha za Marais wetu
 
Unaamini Sana hotuba za wanasiasa wa Tz?

Ndio nyie huwa mnaandamana kuunga mkono hotuba.
 
Hahaha wamtoe sasa pale Ukraine, west wakiweza kumtoa putin kule Ukraine basi dunia nzima tutaamini nguvu waliyonayo. Lakini kwa tujisilaha tule twa juvenile itakua ni kichekesho kuamini.
 
Kama elimu ya juu ni jambo la kawaida kwako, kwa nini uliweke mbele hata katika mijadala ambayo haihitaji elimu ya juu.
Logic nikwamba kuna mambo nivigumu kuyatoleao maoni kama huna uelewa nayo. Kuna watu humu wanalazimisha kutolea maoni vitu ambavyo hawana taaluma navyo. Kwenye issue ya silaha hapa mzee baba elimu nilazima tu hapa layman atachangia nini, Tanzania tuna bodi ya silaha ambayo iko chini ya wizara ya ulinzi, hapa wanakutana wataalamu sio wanasiasa. Haya ni maoni yangu tu
 
Hahaha wamtoe sasa pale Ukraine, west wakiweza kumtoa putin kule Ukraine basi dunia nzima tutaamini nguvu waliyonayo. Lakini kwa tujisilaha tule twa juvenile itakua ni kichekesho kuamini.
Tule tusilaha ni moto wa kuotea mbali kiasi tunachoma vifaru nibalaa. Kuna mdau mmoja alileta hoja kuwa zama za vifaru zinakaribia kufika mwisho. Bro juvelin anashika mtu mmoja au wawili ila kakipiga kifaru kinaungua chote na waliomo ndani
 
Kuna mwanajeshi aliyepo upande wa Ukraine alituhumu US kuwa imefanya vita ya Ukraine na Russia kama sehemu ya kuteketeza siraha zake za zaman! Mizinga waliyopeleka sometime hailipuki wamepeleka siraha za zaman!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo Ukraine imekuwa Dumping area ya kutupa silaha za zamani za US zilizo outdated?
 
Akili matope,badala ya kulipa hamasa wizara ya kilimo ipeleke nje vijana wakajifunze kilimo cha hitech halafu inunue vifaa vyake kwa wingi na iwatawanye mikoani wakafundishe wengine jinsi ya kuvitumia,wewe unawaza vifaru na mizinga,Tanzania ilipo ipo katika level ya kupigana na masuala ya kujikomboa kiuchumi,hao wanapigana hizo vita za hayo mahowitzer walishapiga hatua za kiuchumi miaka lukuki iliyopita,by the way vijana wa sasa mkae mkijua Tanzania haina potential enemy wa kuwaza kuivamia kijeshi,kwa hiyo kufanya big spending kwenye sana za vita,ni ukichaa unaoashiria madhara ya uvutaji wa bangi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…