Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Nin wasiwasi sana na silaha za masafa merfu tulizo nazo ndani ya majeshi yetu ya ulinzi. Miaka ya 200o kuna zile zilizokuwa zinaripuka zenyewe kule mbagala. Na ninavyokumbuka Tanzania tuliwahi kununua vifaru vingi na Gun Howitzers nyingi sana wakati wa utawala wa Nyerere kutokea Urusi. Silaha azile ndizo kwa kiasi kikubwa sana zinazotumika sasa hivi vitani huko Ukraine. Urusi inazitumia na Ukraine pia inazitumia. Jambo linalojitokeza ni kuwa mizinga inayotumika katika howitzers na vifaru hivyo haipatikani tena. Urusi haizitengenezi tena, na Ukraine imekusanya mizinga karibu yote iliyokuwa kwenye nchi za Warsaw pact na haitoshi kwani mizinga mingine imekuwa hailipuki; hiyo imetokea kwenye pande zote mbili za magogoro huo. Sijaona Tanzania ikitupa vifaru vya zamani na kuleta vipya, na sijui kama Tanzania itapata tena mzinga ya kutumia kwenye vifaru hivyo kama siyo vya shoo tu. Vifaru kama hivyo leo hii vimekuwa scrap zilizosambaa kwenye ardhi ya ukraine.

Ninajua kuwa zamani shirika la Mzinga liliundwa ili kuwa linatengeza mizinga hiyo, ila sasa baada ya kutokuwa na matumizi ya mizinga hiyo kwa muda mrefu sijui tuko wapi. Ila vita hii ya Ukraine tuichukulie kama funzo kuwa utegemezi wa silaha za urusi siyo jawabu la usalama na ulinzi wetu tena. Urusi imeshapitwa na wakati sana kwenye teknolojia ya vita.

View attachment 2219644View attachment 2219645View attachment 2219646
Ukiona nchi uchumi wake ni duni,ujue haiwezi kuwa na jeshi imala,
 
Wamagharibi wenyewe wanasema Urusi anatumia silaha za zamani tu mpya hajatoa hata kidogo zaidi ya yale makombora yasiyozuilika.

Hata US/NATO hakuna anaempa Ukraine silaha mpya zote ni za zamani tu.

Yaani kwa operation ya Ukraine Urusi ni kama anasafisha stoo tu..
Urusi hajatumia silaha mpya kwa sababu hana.
T14 Armata Elungata dudus
 
Well kwa vile hujui kuwa Pentagon huwa wako mbele sana, ni vigumu kukubaliana nami kuwa hata wao wanajua kabisa namna ya kutokumwaga mchele mbele ya kuku wengi.

Technology nyingi za china ni zile walizodownload kwenye computers za Makampunia ye kijeshi ya marekani mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili wakati makampuni hayo hajajua kuwa kuna wanaowafuatilia. Baada ya hapo, China wanafanya mambo ambayo yameshapitiwa na pentagon. Ukiamini kuwa Pentagon inasema hatuna uwezo, basi ujue huamini ukweli.
Pentagon wanatabia ya kufanya hadaa sana nakumbuka Kuna kipindi mkuu wa majeshi aliwahi kusema Kiev inaweza kuanguka ndani ya siku tatu lakini kilichotokea wote tumeona.
 
Na ukute ni graduate,hii nchi Ina shida sana
Usisumbuliwe na bias ya mtu kuwa graduate au la, wewe amini facts bila kujali kama facts hizo zinatoka kwa layman au zinatokwa kwa intellectual. Kuna watu wengine ukiwaambia elimu ya juu ni kama unawaambia kabila lao, na kuna wengine (kama wewe) wanadhani elimu ya juu ni muujiza!
 
Kuna vitu unachanganya na vingine unapatia.
Kuna vingine hujui vimeundwaje na vinafanyaje kazi.
Kwanza si kweli kwamba huwezi rusha kombora la hypersonic speed kutoka ktk kifaa kilichopo ardhini.
kwa taarifa yako silaha nyingi tu zinafikia hiyo speed maana hypersonic speed ni speed yoyote inayoanzia mara 5 ya speed ya sound na ndiyo kitu wanaita mach 5.

Ni kweli aliyorusha russia ukraine siyo true cruise hypersonic missile. Yaani siyo hypersonic glide vehicle (HGV). Lakini anayo hiyo ya ukweli hajatumia inaitwa AVANGAD siyo ile KINZHAL aliyotumia ukraine ambayo ni variant ya ISKANDER.

soma hapa What to know about Russia's hypersonic missiles
Kinzhal kweli mashabiki wa Urusi wanaitaja sana wakati haina maajabu. Kwanza ina warhead ndogo kutokana na shape yake, pili ina gharama sana kutengeneza na makadirio ni kwamba Kinzhal moja inagharimu around $100 million na kwa vile haina nuclear warhead basi haina maana sana kuitumia kwenye target zisizo na gharama kubwa au umuhimu mkubwa.

Ni bora watumie Kalibr kadhaa kutoka kwenye meli au submarines hata missiles mojawapo ya hizo zikiwa shot down ila nyingi zitapenya na kufanya shambulizi, hapo gharama ni kidogo na mlipuko ni mkubwa. Au kwa angani watumie hizo jamii ya Raduga. Kinzhal ingekuwa ni anti ship hapo ingekuwa na maana sana ila ingehitaji kuwa na range kubwa au kuwa launched na stealth jet tena ikiwa kwenye internal weapons bay.

Avangard ni vigumu kuwa intercepted ila inapachikwa kwenye ballistic missile na kutumika kwenye terminal phase. Ni zaidi ya MIRVs ambazo nazo kwa speed yake ni vigumu kuzizuia ila Avangard glide vehicle ina advantages nyingine. Wako kwenye development ya Poseidon nuclear powered torpedo yenye nuclear warhead, ina unlimited range alafu ni autonomous. Pia wanajaribu kutengeneza Burevestnik itakayokuwa nuclear powered cruise missile na yenye unlimited range. Ila na hizi sanctions wanachelewa miaka
 
Usisumbuliwe na bias ya mtu kuwa graduate au la, wewe amini facts bila kujali kama facts hizo zinatoka kwa layman au zinatokwa kwa intellectual. Kuna watu wengine ukiwaambia elimu ya juu ni kama unawaambia kabila lao, na kuna wengine (kama wewe) wanadhani elimu ya juu ni muujiza!
Sidhani elimu ya juu ni miujiza,ni Jambo la kawaida hasa kwa Tanzania ya leo,kinachonikwaza ni hao wasomi kuwa wajinga licha ya kukaa darasani kwa walau miaka 16
 
Jamani huyu ameuliza kuhusu kijeshi chetu na siyo US wala Russia....
Tumwambie ukweli ni hivi...
Yale magari makubwa ya kizamani unayaonaga siku ya mashujaa, hayo chini ni ya kichina yanajulikana kama A 100, na masfa yake ni kati 40km mpaka 100km, hata Morogoro hayafikishi...
View attachment 2219729



Vile viroket unavinaga uwanja wa taifa ni vya kutungulia ndege za bangaboi sio za kisasa kama Sukhoi za jeshi la Uganda au Northrop 5E za jeshi la kenya,hutu tuanitwa SA-6 (2K12 Kub) kutoka Russia, tulitengenezwa 1958, na tuna masafa ya mpaka 24km
1652222708652-png.2219730



Na hii ndio Uganda Sukhoi, tukizitaka hizi inabidi serkali ianze kugawa basikeli kwa wabunge na mawaziri ili kwenda sambaba na bei ya mafuta na uendeshaji, Uganda wana Mafuta yao.....
View attachment 2219714


Halafu hawa jamaa hapa chini, wanachekesha sana....🤣🤣🤣
View attachment 2219732

View attachment 2219731

View attachment 2219733


Na hii ni Kenya Northrop 5E
View attachment 2219718

View attachment 2219730
Dah!...unataka tumiliki S-300 ?, Tuna adui gani wa kutisha mpaka tujihami hivyo ?
T14 Armata Tsh Nyamizi britanicca TUJITEGEMEE mohamedidrisa789
wa kupuliza
 
Kama elimu ya juu ni jambo la kawaida kwako, kwa nini uliweke mbele hata katika mijadala ambayo haihitaji elimu ya juu.
Suala la silaha tpdf ni suala la elimu,yaani hata ukiwa la Saba unajua kwamba tpdf wanajua umuhimu wa ku-update silaha,na kwa kuwa itakuwa mfuatiliaji wa hotuba za rais hasa siku ya sherehe za Uhuru,itakua umekutana na hotuba za Tambo za uboreshaji jeshi kwa silaha za Marais wetu
 
Suala la silaha tpdf ni suala la elimu,yaani hata ukiwa la Saba unajua kwamba tpdf wanajua umuhimu wa ku-update silaha,na kwa kuwa itakuwa mfuatiliaji wa hotuba za rais hasa siku ya sherehe za Uhuru,itakua umekutana na hotuba za Tambo za uboreshaji jeshi kwa silaha za Marais wetu
Unaamini Sana hotuba za wanasiasa wa Tz?

Ndio nyie huwa mnaandamana kuunga mkono hotuba.
 
Hiyo siyo kweli. Vita imeanzishwa na Urusi, na hata hivyo marekani ilisita sana kuisaidia Ukraine hadi baada ya zaidi ya mwezi na nusu. Urusi anaopoona anaanza kuelemewa ndipo anatafuta wa kulaumu kuwa marekani ndiyo ilisababisha vita. Putin alikutana na viongozi wengi sana wa nchi za Magharibi wakimwomba aachane na mambo ya kuvamia nchi jirani, yeye akadhani wanamuogopa. Sasa ngoja avune alichopanda.
Hahaha wamtoe sasa pale Ukraine, west wakiweza kumtoa putin kule Ukraine basi dunia nzima tutaamini nguvu waliyonayo. Lakini kwa tujisilaha tule twa juvenile itakua ni kichekesho kuamini.
 
Kama elimu ya juu ni jambo la kawaida kwako, kwa nini uliweke mbele hata katika mijadala ambayo haihitaji elimu ya juu.
Logic nikwamba kuna mambo nivigumu kuyatoleao maoni kama huna uelewa nayo. Kuna watu humu wanalazimisha kutolea maoni vitu ambavyo hawana taaluma navyo. Kwenye issue ya silaha hapa mzee baba elimu nilazima tu hapa layman atachangia nini, Tanzania tuna bodi ya silaha ambayo iko chini ya wizara ya ulinzi, hapa wanakutana wataalamu sio wanasiasa. Haya ni maoni yangu tu
 
Hahaha wamtoe sasa pale Ukraine, west wakiweza kumtoa putin kule Ukraine basi dunia nzima tutaamini nguvu waliyonayo. Lakini kwa tujisilaha tule twa juvenile itakua ni kichekesho kuamini.
Tule tusilaha ni moto wa kuotea mbali kiasi tunachoma vifaru nibalaa. Kuna mdau mmoja alileta hoja kuwa zama za vifaru zinakaribia kufika mwisho. Bro juvelin anashika mtu mmoja au wawili ila kakipiga kifaru kinaungua chote na waliomo ndani
 
Kuna mwanajeshi aliyepo upande wa Ukraine alituhumu US kuwa imefanya vita ya Ukraine na Russia kama sehemu ya kuteketeza siraha zake za zaman! Mizinga waliyopeleka sometime hailipuki wamepeleka siraha za zaman!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo Ukraine imekuwa Dumping area ya kutupa silaha za zamani za US zilizo outdated?
 
Akili matope,badala ya kulipa hamasa wizara ya kilimo ipeleke nje vijana wakajifunze kilimo cha hitech halafu inunue vifaa vyake kwa wingi na iwatawanye mikoani wakafundishe wengine jinsi ya kuvitumia,wewe unawaza vifaru na mizinga,Tanzania ilipo ipo katika level ya kupigana na masuala ya kujikomboa kiuchumi,hao wanapigana hizo vita za hayo mahowitzer walishapiga hatua za kiuchumi miaka lukuki iliyopita,by the way vijana wa sasa mkae mkijua Tanzania haina potential enemy wa kuwaza kuivamia kijeshi,kwa hiyo kufanya big spending kwenye sana za vita,ni ukichaa unaoashiria madhara ya uvutaji wa bangi.
Nin wasiwasi sana na silaha za masafa marefu tulizo nazo ndani ya majeshi yetu ya ulinzi. Miaka ya 2000 kuna zile zilizokuwa zinalipuka zenyewe kule Mbagala. Na ninavyokumbuka Tanzania tuliwahi kununua vifaru vingi na Gun Howitzers nyingi sana wakati wa utawala wa Nyerere kutokea Urusi. Silaha zile ndizo kwa kiasi kikubwa sana zinazotumika sasa hivi vitani huko Ukraine.

Urusi inazitumia na Ukraine pia inazitumia. Jambo linalojitokeza ni kuwa mizinga inayotumika katika Howitzers na vifaru hivyo haipatikani tena. Urusi haizitengenezi tena, na Ukraine imekusanya mizinga karibu yote iliyokuwa kwenye nchi za Warsaw pact na haitoshi kwani mizinga mingine imekuwa hailipuki; hiyo imetokea kwenye pande zote mbili za magogoro huo.

Sijaona Tanzania ikitupa vifaru vya zamani na kuleta vipya, na sijui kama Tanzania itapata tena mzinga ya kutumia kwenye vifaru hivyo kama siyo vya shoo tu. Vifaru kama hivyo leo hii vimekuwa scrap zilizosambaa kwenye ardhi ya ukraine.

Ninajua kuwa zamani shirika la Mzinga liliundwa ili kuwa linatengeza mizinga hiyo, ila sasa baada ya kutokuwa na matumizi ya mizinga hiyo kwa muda mrefu sijui tuko wapi. Ila vita hii ya Ukraine tuichukulie kama funzo kuwa utegemezi wa silaha za urusi siyo jawabu la usalama na ulinzi wetu tena. Urusi imeshapitwa na wakati sana kwenye teknolojia ya vita.

View attachment 2219644View attachment 2219645View attachment 2219646
 
Back
Top Bottom