Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Acha uongo T-4 haijawahi kutumika kwenye vita yeyote.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Bora ume sema wewe, nimeshangaaa kishenzi na kuona hapa kuna upenzi flani wa ki magharibi na marekani hiyo kifaru nimeshtuka kusikia imetia team hadi ukraine nikapuuza na mada husika
 
Usichukie,nukuu point yangu,Tanzania haina uwezekano wa kuvamiwa kama Ukraine,ukiangalia historia ya Ukraine na Tanzania tuko tofauti sana,Tanzania inafanana na nchi kama Uswisi,tukitumia fedha nyingi kwenye zana za kivita ni upotezaji wa fedha,zana zilizopo zinatosha kwa ajili ya maonyesho ya tarehe 9 December na siku ya uhuru.
 
Mkuu hatuna silaha mkuu ingia online uone.

Active presonnel wenyewe ni 27,000 tu
 
Kiduku aweze Marekani ashindwe? Haya ni maajabu ya dunia. Hata kama hatuwapendi Wamarekani tuwe wakweli yeye ndio mbabe wa dunia.
Kuna watu wanaleta maneno ya vijiwe vya kahawa.
Lini amewapi kusikia majaribio ya silaha Us?

Anatishwa na hivi vimasikini kama Korea kaskazini?
Huyo akiamuliwa ni siku moja tu anapotezwa.
Kwenye sila Us hajapata mshindani.
Ana silaha ambazo hakuna taifa linazo
 
Urusi hajatumia silaha mpya kwa sababu hana.
T14 Armata Elungata dudus
Wanataka atumie silaha gani mpya? T-15 Armata iko kwenye development, Bumerang APC iko kwenye development, Su-57 hazifiki hata 10. Watumie nini kipya sasa, watoe wapi.

Kwani hizi silaha ambazo Ukrainians wanapewa ni mpya? Mbona Marekani inawapa silaha za zamani vilevile, Ujerumani inachukua zilizo outdated ndio inawapa na bado wanazitumia vizuri. Australia, UK na wengineo wanatoa silaha ambazo walitakiwa watupe hawana kazi nazo. Poland mpaka ikataka iwagawie bure Mig-29, jirani yao mwingine sikumbuki ni Estonia kawapa T-72 za zamani.

Silaha mpya za maana walizonazo Ukraine ni NLAW, Bayraktar TB2, Switchblade na Caesar chache sana.
 
Mkuu, Marekani hadi sasa hawana hayo makombora, kama hujui. Wanajaribu kutengeneza, lakini bado hawajafanikiwa.

Ironically. yule kiduku wa Korea Kaskazini tayari anayo!
Kwenye masuala ya ulinzi una safari ndefu sana kama unakaa hapo unaamini North Korea wana hypersonic missiles. Na umekosea mengi hata kwenye uzi huu, kuna sekta zako unafanya vizuri ila hii unaamini mambo yasiyokuwepo
 
Hayo magari makubwa ya A100 wenyewe People's Liberation Army waliyakataa hayakukidhi vigezo, sijui ni vigezo gani hivyo.
Sikumbuki yalitengenezwa na kampuni ya NORINCO au nani. Kwahiyo duniani sidhani kama tulionayo ni zaidi ya nchi tatu.

Hatuna air defence system ya kueleweka, hizo SAM ni very outdated na bahati mbaya Tanzania najua hatufanyi sana modifications za silaha. Hizo MANPADS sijui ni version ya mwaka gani yani zinakatisha tamaa ukiziona.

Uganda wana ndege za kisasa ila operation cost inawatoa jasho. Hawana training nzuri na ndege zao chache hawana hata zaidi ya squadron moja. Kama South Africa wanazo JAS-39 Gripen sometines wanasuasua training sembuse Uganda uchumi wa kujikongoja. Wenye airforce imara Afrika ni Egypt, Morocco na Algeria.

Afrika hii hakuna nchi inajua kutengeneza silaha kama South Africa. Wana anti aircraft missiles zinaitwa Mokopa niliona Finland walizinunua wakazitumia kwenye corvette zao. Wana helicopter launched anti tank missiles za 10km range. Waliwahi tengeneza attack helicopter Marekani wakaweka sanctions isiuzwe ilikuwa nzuri kabisa. Wana attack boats na MRAP vehicles. Sisi hata shells za vifaru sijui kama tunajua.

Kati ya majirani wote, nikilinganisha jeshi la Kenya na Tanzania kuna kitu nashawishika kuamini
 

Tim nato mnaangaika sanaa
 

Na Cyber Warfare
 
Kwenye masuala ya ulinzi una safari ndefu sana kama unakaa hapo unaamini North Korea wana hypersonic missiles. Na umekosea mengi hata kwenye uzi huu, kuna sekta zako unafanya vizuri ila hii unaamini mambo yasiyokuwepo
Mkuu, hujui kitu.
Nyamaza na tafuta muda ujiridhishe mwenyewe kwa kutafuta habari.
Weka unazi wa unaowapenda pembeni. Sifaidiki na chochote kwa kukupa wewe taarifa hizo ambazo ni dhahiri huna, halafu unajifanya wewe ni mjuwaji katika maswala hayo.

Hii ndiyo tabia ya kiTanzania isiyofaa kabisa. Kajiridhishe mwenyewe. Katafute taarifa hiyo, imejaa tele kama unajua jinsi ya kutafuta habari.
 
Ninavyoelewa Mimi ni sawa na kichuguu alivyoandika hapo, lakini hata refference uliyoweka hapo inasupport statement ya kichuguu, huwezi kutuma Hyper Missile kutoka chini, lazima ipigwe juu kwa juu.
Kwani hakuna rocket zinazofikia mach 5?
Je, rocket haziwezi kuwa launched toka kwenye fixed station (launchpad) ambayo ipo kwenye earth surface?

Kitu cha msingi ni namna hiyo rocket ikirushwa ikiwa hewani unafanyeje manouvability ya kuifanya iwe Hypersonic glide missile (HGV) kama hiyo Vangad ya Russia au ile version ya mchina.

Soma vizuri hiyo article kuna kitu hujakitilia mkazo au maanani ungeona hii point nimekufafanulia. Soma na zingine zinazoelezea kuhusu hizo silaha utaelewa.
 
Usa ilidanganya tu ili adui aingie Chaka

Kama kuna kitu usa yupo much concerned ni suala la ulinzi wa Taifa lake

So ukijichanganya unapotea
Tatizo lenu kuamini USA hawezi kutanguliwa kwenye kitu chochote cha teknolojia!
Kwa mawazo yenu mngekuwa enzi zile Yuri Gagarin anaenda outer space orbit kabla wamarekani hawajaweza kutengeneza chombo cha kuweza kufika huko msingeamini kama sasa msivyo amini Russia na China Walitangulia kwenye teknolojia ya HGV.

Marekani astronauts walikuwa wanakesha kupiga hesabu za kuvusha chombo chao kwenye point of 'go-no go' wakati huo Yuri ashavuka zamani na chombo chake huku cosmonauts wenzie wanajipongeza na Vodka.
 
Hujui kuwa tuliwahi kuvamiwa na Amin?
 
Historia ya mashindano ya kwenda anga za juu unaikosea. Mpaka mwaka 1957 marekani ilikuwa haifikirri kwenda anga za juu wakati Urusi ilianza mwaka 1951; kwa hiyo urusi ilianza mapema shughuli hiyo. Mwaka 1957 waliporusha satellite ile ya Sputnik, ndipo Marekani nao wakaona kuna haja ya kuingia kwenye anga za juu kwani hiyo spunik inaweza kuangusha Bomu la atomik ndani ya nchi kwa kutokea angani. Ndipo NASA ilipoanzishwa mwaka 1958; kwa hiyo Wakati Gagarin anaingia angani mwaka 1960, ilikuwa ni baada ya warusi kufanya utafiti wa takriban miaka kumi wakati NASA ndipo wanaaza tu. Rais Kennedy alipofungua ile Appolo program mwaka 1961, ndipo NASA nao wakaanza maswala ya safari za anga za juu, juhudi zilioiwezesha marekani ni kuwa ya kwanza kupeleka watu kwenye mwezi; zilipigia safari nyingi sana kwenda mwezini na kurudi; sita zilitua na watu, na nyingine zilikuwa zinazunguka mwezi na kurudi na nyingi sana zililuwa zinakwenda bila watu.

Kwa hiyo ingawa ni kweli kuwa Urusi ilitangulia kujishughulisha kwenye mambo ya anga za juu, siyo kuwa ilishinda mashindano hayo, kwani baadaye NASA ndiyo mshindi. Iwapo wangeanza pamoja mashindano hayo, ni wazi NASA angewaacha Urusi mbali sana. Safari za NASA zimetusaidia vitu vingi sana ikiwemo aina za magodoro ya zero g, viatu vya laba, Inertial navigation Systems zinazotumika kwenye usafiri wa ndege za abiria, na mengine mengi sana ambapo juhudi za urusi zilizokuwa ni za kutaka ufahari tu. Hakuna product kwenye maisha ya kila siku unayoweza kuihusisha moja kwa moja na space program ya Urusi labda satellite tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…