Una maana Urusi hawana silaha walizotengeneza toka enzi hizo, tokea sisi tunaagiza toka kwao?
Na haya makombora yanayokwenda spidi ya G5, na kuwa na uwezo wa kuepa kinga dhidi yake, nayo ni teknologia ya zamani?
Urusi hizo guided munitions hana nyingi kwenye stock maana ni gharama sana. Hata hizo hypersonic missiles unazosema ni za gharama maradufu na hakuna jeshi linaweza sutain kuzitumia, Urusi hana hata hypersonic missiles 100 yani zimeanza miaka mitatu sijui hapo nyuma. Ndio maana Israel baada ya kuona inatumia missile ya $100,000 kufanya interception ya maroketi ya Hamas yenye gharama za $200 ikaamua iunde mfumo wa kutumia laser ambao sana sana utakula umeme tu. Israel wako very concerned na cost kuliko majeshi makubwa mengine duniani.
Marekani wanazo GPS guided shells za 152mm kwa ajili ya hizi self propelled howitzers zao ila gharama ya shell moja ni $70,0000. Sasa unakuta kuna mahitaji ya shells kama elfu 10 kwa wiki kwenye battle front nzima, huwezi tumia hizo expensive pekee lazima uchanganye. Ndio maana Ukraine kapewa stationary artillery kadhaa kutoka Marekani, yeye mwenyewe anazo za kwake alizokuwa anatengeneza na kapewa more advanced na zenye long range ni 155mm Casar za Ufaransa hizo nazo shells zake expensive.
Tukirudi kwa hoja ya mleta mada. Kama last week niliona CEO wa Raytheon Technologies anasema hawana tena uwezo wa kutengeneza Stinger MANPADS hizi zinazotolewa Ukraine kwa maana block hiyo mara ya mwisho Marekani inainunua ni miaka 13 iliyopita kama sijakosea kumbukumbu. Wanasema components zilizotumika ni old technology ambayo suppliers hawatumii tena, pia facilities za kuunda zilishafungwa na kubadilishwa matumizi na watalaamu washapungua na kujikuta kwenye mambo mengine. Na processors zake zinaisha muda wa matumizi mwaka 2023.
Ni kama leo hii unamwambia mtengenezaji wa meli ya mwaka 2002 akubadilishie TV kadhaa zilizoungua anakwambia hana tena pa kupata TV za chogo.
Concern ya OP ni kubwa na mwenyewe kwenye hii vita ilinishtua. Mwezi jana mwishoni Ujerumani ilitaka kutoa Gepard anti aircraft tank (Ujerumani wana classification ngumu ya silaha) kwa Ukraine. Hizo Gepard ziko kwenye storage facilities maana Ujerumani ilishaacha kuzitumia ila iliwahi kuziuza kwa Switzerland na kufanya technology share ya kutengeneza munitions zake. Kwa kuwa Ujerumani iliachana nazo basi haijui kutengeneza hizo munitions kwa sasa, ikaiomba Switzerland kwamba isaidie kuipa Ukraine ammunition ila wakakataa kwa vile sera yao ni neutrality.
Teknolojia ngumu hupotea kama haifanyiwi kazi au haina soko. Kuna sababu za msingi kwa nini Ufaransa iliachana na project ya kutengeneza Eurofighter Typhoon ikaenda kutengeneza Dassault Rafale. Leo hii hao Ujerumani, Spain, UK na Italy waliobaki kwenye hiyo project hawawezi kutengeneza fighter on their own ila Ufaransa anaweza. Kwanini Japan watumie gharama nyingi kutengeneza Type 99 tank, au South Korea na K2 Blackpanther, au Ufaransa na Lecrerc. Hivi vifaru vyote haviizidi uwezo Abrams ya Marekani ila vina bei zaidi ya mara mbili yake.
Ukisoma projects za Marekani kuna wakati wanatengeneza silaha fulani sababu mojawapo ni kufanya kampuni iwe busy na teknolojia isipotee.