Simanjiro: Mwanaume wa miaka 30 amuoa kwa nguvu binti wa miaka 14 kwa ridhaa ya baba

Simanjiro: Mwanaume wa miaka 30 amuoa kwa nguvu binti wa miaka 14 kwa ridhaa ya baba

John Walter

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
68
Reaction score
63
Na John Walter-Manyara
Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Loswaki wilaya ya Simanjiro aliyejulikana kwa jina Lalahe Karoli (30) kwa tuhuma za kumtorosha na kwenda kuishi kinyumba na mtoto mwenye umri wa Miaka 14 kwa ridhaa ya Baba wa Mtoto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga amethitisha tukio hilo ambapo amesema mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumtorosha binti huyo na kumpeleka chumbani kwake na kumlazimisha kufanya nae ngono kisha kuishi nae kwa nguvu.

Kamanda Kuzaga amesema kwa kushirikiana na timu ya upelelezi na raia wema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi.

Pia Jeshi hilo limeeleza kuwa limemkamata Baba wa Mtoto aitwaye Lembris Salonic (60) mkazi wa Loswati Terati wilaya ya Simanjiro ndiye aliyeidhinisha kuolewa kwa binti yake huyo.

Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa ili kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na watoto ambavyo vinarudisha nyuma Maendeleo ya mtoto na jamii kwa ujumla.

IMG_6952.JPG
 
Na John Walter-Manyara
Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Loswaki wilaya ya Simanjiro aliyejulikana kwa jina Lalahe Karoli (30) kwa tuhuma za kumtorosha na kwenda kuishi kinyumba na mtoto mwenye umri wa Miaka 14 kwa ridhaa ya Baba wa Mtoto.
Pia Jeshi hilo limeeleza kuwa limemkamata Baba wa Mtoto aitwaye Lembris Salonic (60) mkazi wa Loswati Terati wilaya ya Simanjiro ndiye aliyeidhinisha kuolewa kwa binti yake huyo.
Tuwe makini na mambo haya: hawa watu - Lalahe Karoli na Lembris Salonic huwezi kuwashitaki kwenye mahakama moja na kosa moja. Unamtuhumu Lalahe kwa kwa kumtorosha binti, unamtuhumu Lembris kwa kudhinisha. Hii ni Kangaroo court, BTW, sheria yetu ya ndoa ianruhusu binti wa miaka 12 kuolewa kwa ruhusa au usimamizi au ridhaa ya wazazi
 
Back
Top Bottom