Simba 1-0 Prisons | Ligi kuu bara | Benjamin Mkapa

Mwanzoni ulisema umeangalia kwa camera ya nyuma ni faulo ya wazi kabisa. Saivi unasema jamaa kaunawa mpira bila ubishi. Inaonekana unafosi uhalali wa penati
 
Sasa sio mara ya kwanza. Tukianza kufukua makaburi hizi point za simba hazina uhalali. Swali ni kwamba ni lazima simba na Yanga zishinde ndo ligi iwe kamili?

Wacheze hizo timu mbili basi ligi iishe mshindi apewe kombe.

Huu upumbavu mpira unakuwa wa kupuuzi esp kama unafuatilia pia mpira wa wenzetu, hapa kwetu hata kama una katimu umekapenda kanavyojituma unataka ukachangie kaongeze nguvu unaghairi maana unajua timu ni mbili tu. Mwishowe ndo tunakuwa na ligi uchwara na timu ya taifa uchwara.

Mfano hai, sasa hapa point tatu unaziringia kabisa kuwa una point 3 kweli?

 
Mwanzoni ulisema umeangalia kwa camera ya nyuma ni faulo ya wazi kabisa. Saivi unasema jamaa kaunawa mpira bila ubishi. Inaonekana unafosi uhalali wa penati
Mwanzoni nilisema tumebebwa, hiyo ni baada ya kuona replay kutoka kwenye angle iliyokuwa ina face lango

Lakini baada ya replay ya pili ambayo ilichukuliwa upande wa nyuma ya goli la prisons niliona kwa uwazi kabisa mjuba akiunawa
 
Sasa ofsa kwani ile penati ya yanga na namungo unaweza kuijadili kwa namna gani ukaitofautisha na hizi za simba unazozita fraud?

Au ile ya mayele kushika halafu penati wanapewa yanga?
 
Sasa ofsa kwani ile penati ya yanga na namungo unaweza kuijadili kwa namna gani ukaitofautisha na hizi za simba unazozita fraud?

Au ile ya mayele kushika halafu penati wanapewa yanga?
Ndo upuuzi ninaoongelea, Nikaedit maoni yaliyopita kuwa Hapa kama ni mpenzi wa soka unataka kapesa kako uwekeze kwa katimu ulikokapenda kanakojituma ushawishi na marafiki wajipige pige hivyo hivyo timu iongeze juhudi uwanjani ukikumbuka haya unaghairi na kuweka nguvu kwenye mpira wa Epl na kununua tiketi za kuona mpira live kama utaweza maana utaufurahia mpira kuliko hiyo pesa uwaongezee nguvu wanyongwaji wa hapa Tanzania.

Mfano Epl Norwich na Sunderland uwanja utajaa ila hapa kwetu mbao na Yanga haujai na Yanga itapewa penati.
 
Hapa akili yako ilifosi penati iwe halali kuna faulo imechezwa na umejiridhisha kwa angle ya camera ya nyuma. Mimi ndio nikakwambia mbona wenzako wanahisi pengine labda ni penati iliyotokana na kushika mpira ndipo ukaja na kauli mpya eti umejiridhisha kwa camera ya nyuma kuwa mpira umeshikwa. Tuwekee hapa hiyo clip inaonesha upande wa angle hiyo unabwabwaja eti clip inagoma. Acha ushabiki mkuu
 
Daah yani we jamaa mbona unatumia nguvu kubwa kufosi ionekane sio penati?

Hivi umejiridhisha vya kutosha mpaka ukaona hiyo sio penati?
 
Hahahaha Nimesikia Mtaani Kuna Watu Mmejifunza Kupiga Penalty.

Heri Hata Kama Ndio Hivyo Hivyo Ni Heri Mshinde Hata Mechi Zenu Hivyo Hivyo Mlete Ushindani.

Bingwa Mtetezi Si Uachwe Point 100 Mambo Gani Hayo.
 
Daah yani we jamaa mbona unatumia nguvu kubwa kufosi ionekane sio penati?

Hivi umejiridhisha vya kutosha mpaka ukaona hiyo sio penati?
Kwa kutumia marejeo ya Azam niliyofanikiwa kuyaons haikuonesha mchezaji wa Prisons akishika mpira. Bahati nzuri mwenzetu umepata nafasi ya kuona clip ya angle ya camera ya nyuma. Tupia hapa utudhibitishie kuwa ni penati halali
 
Wale mnaosema hakuugusa, msikieni goalkeeper wa prisons ambaye alikuwepo eneo la tukio
 
Kwani mpira si ulikuwa live kila mtu kaona? Ni makosa tu a mwamuzi lakini kiuhalisia haiku penalty halali.
 
Simba Tulichobaki Saiv Ni Mpinzani Kutafutiwa Kadi Nyekundu Au Tupewe Penalty Au Tuongezewe Muda Mrefu Baada Ya Dk 90 Na Kama Tukiwa Tunaongoza Goli Moja Muda Wa Nyongeza Uwe Kidogo Hata Kama Zlipotea Dk Nyingi Uwanjani Ndo Tushinde [emoji17]
Kwahivyo zikiongezwa dakika nyingi anayecheza ni Simba SC tu, hiyo timu nyingine ingali imesimama tu haichezi wala haifungi bao, endapo bao litafungwa litakataliwa kwa kuwa hizo dakika ni za Simba SC.

Nyie watu bhana....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…