Simba 1-0 Prisons | Ligi kuu bara | Benjamin Mkapa

Simba 1-0 Prisons | Ligi kuu bara | Benjamin Mkapa

Tatizo ni namna ya kufungua huo ukuta hapo ona watu 9 hadi 10 wote wapo golini Kwa namna hii timu inahitaji ubunifu zaidi
Ujinga zaidi ni pale kocha anapofanya sub dakika za 70

Yaani anaamini kwa uzembe huu unaweza kurekebishika kwa kumshauri mchezaji huyo huyo aliyecheza hovyo abadilike, wakati benchi wapo mbadala wake wataoweza kufanya vizuri zaidi

Sometimes naona hata ni bora kuwapa nafasi wale madogo wa timu B wanaweza kujituma kwa nguvu zote ili mradi waonekane na wapewe dhamana ya kuchezea kikosi cha kwanza kwa siku zote

Usikute kikosi hiki kikicheza na kikosi B kinafungwa, who knows?
 
Nakumbuka enzi ya Aussems, ilikuwa Simba akifungwa mechi moja au ku draw basi next game kocha atabadilisha mfumo, anaweza mpanga mchezaji mmoja juu ya mabeki ili kuongeza ulinzi, na Kennedy Juma alikuwa anatumika zaidi kwenye hili.

Lakini huyu kocha wetu wa sasa hajui kuiona hatari na kuifanyia kazi mapema, hizi counter wanazopiga hawa jamaa ni wazi anatakiwa mtu wa kusimama juu ya mabeki asipande, kazi yake iwe kuzima haya mashambulizi ya kushtukiza ya hawa jamaa, lakini naona kocha yupo tu, akili yake yote kushambulia, then tukifungwa aanze ku panic .
Kocha kafundisha Riali madruidi uyo ujue
 
Simba wanatakiwa kuboresha kiungo cha kati alafu wasilazimishe sana kutaka kupita katikati wakati pamejaa.wapanue uwanja kutumia wingi za pembeni ili prison atanuke.bila kufanya hivyo hii mechi ushindi niwa kubahatisha.Alafu pia simba haina wachezaji aggresive kabisa.yaani timu inacheza kwakurelax kama ipo bonanza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Yaani mwenyewe najiuliza hivyo hivyo, ni nini tatizo na juzi hapo Mo kasema kweli kuna matatizo namimi naanza kuamini sasa
Matatizo si yalikuwa yanajulikana tangu match ya kwanza ya ligi kuwa ni GSM anawahonga timu pinzani na mbaya zaidi akaja kuwa mzamini mwenza?
 
Simba wanatakiwa kuboresha kiungo cha kati alafu wasilazimishe sana kutaka kupita katikati wakati pamejaa.wapanue uwanja kutumia wingi za pembeni ili prison atanuke.bila kufanya hivyo hii mechi ushindi niwa kubahatisha.Alafu pia simba haina wachezaji aggresive kabisa.yaani timu inacheza kwakurelax kama ipo bonanza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Hilo nalo tatizo, wachezaji wana relax sana hata timu ikitangulia kufungwa, naona ustaa umejaa sana kwenye vichwa vyao, hawajui kulazimisha matokeo mechi nyingi wako slow wanadhani magoli yatakuja yenyewe tu.
 
Sakho anatakiwa kuingia ili akipata mipira akimbie katikati wamkate wapate foul lakin magoli ya kutengeneza ni magumu mno.hawa mabeki wakati hawatoki kwwnye 18.ina maana kwa sare hii prison anachukua ubingwa.
Prison tena ndio anachukua Ubingwa?
 
Back
Top Bottom