Simba 10 wauawa Ngorongoro, yadaiwa ni kisasi baada ya Simba kuwala punda wawili wa wafugaji

Simba 10 wauawa Ngorongoro, yadaiwa ni kisasi baada ya Simba kuwala punda wawili wa wafugaji

Ila wafugaji kuna muda wanazingua...... hii ni hujuma na haitafumbiwa macho
Binadamu na wanyama wa kufugwa wanaouawa na wanyama hutosikia popote! Ila swala auawe sasa
 
Simba ni muhimu zaidi kuliko wamasai?
Kila mmoja anaumuhimu wake. Suali lako sio valid!

Wamasai wamekosea km
Ni kwel

Lakini isijekuwa hii ni fake story iliyotengenezwa ili kujustify namna ya kuondoa watu kule ngorongoro

Nchi ina drama sana hiyo
 
Hii ni study case nzuri inapaswa kuigwa nchi nzima sehemu zote wanazosumbuliwa na wanyama wakali tafuteni hiyo sumu waliyotumia hao mashujaa na ndio iwe kiboko ya wanyama wasumbufu nchi nzima, tena kule wanaosumbuliwa na fisi dawa ndio hii kuwategea mizoga yenye sumu.

Nawapa hongera sana waliofanya ubunifu huu, bado tembo wanaokula mazao ya wanavijiji.
 
Isiwe michezo tu ili lile la kuwaondoa wafugaji litimie
 
Kwanza simba wameua punda wawili iweje wao waue simba 10? Kwamba hawajui hesabu? Si wangeua simba wawili ngoma iwe droo?
Swali linakuja Wamasai wanakula punda?

Je Wamasai wameanza kuishi lini pamoja na Wanyama humo Ngorongoro?
 
Wajinga wameua hadi simba watoto, maslahi ya taifa yanakuja mwanzo siku zote
 
Lakini watu wanaoishi karibu na wanyama watakuwa labda tayari wanazo instructions fulani kuhusu hao wanyama.
 
Yani kwa akili za kawaida uue simba 10 kwa ajili ya punda wawili???
 
Hao wamasai walioua Simba watalipa gharama kubwa sana kwa walichokifanya. Watajuta. Ninaisihi serikali iwaondoe hao masai haraka sana eneo hilo wasije kusababisha madhara zaidi.
Ukute nawe ni mshauri wa Mama Abdul.
 
Hao simba itakuwa ni waduanzi, simba gani hao wanakula mizoga? Simba huwa hawali mizoga, wanakula fresh wanachoua wenyewe
 
umewahi kufuatilia au unaishi JF kila siju???
Achana na jf, mi ni mmoja kati ya zile jamii zilizo karibu na hifadhi za wanyama, tembo wameua watu nashuhudia na mazishi nahudhuria ila kusikia TANAPA au chombo chochote chenye mamlaka kusema kitu hakunaa. Ila mtu akutwe na nyama ya nyumbu sasa! Au jangili akamatwe huko pori wengine ni kubutuliwa risasi wanaishia hukoo...
Sio kama nina jealous hapana, humo kwenye mahifadhi ndipo nimezaliwa na kukulia hadi namalizia first degree ndo mzee anastaafu utumishi TANAPA!
 
Taarifa za awali kutoka eneo la Ndutu, Kata ya Endulen, Wilaya ya Ngorongoro, zinaeleza kuwa leo Septemba 19, 2026, simba wapatao 10 wameuawa katika tukio linalodaiwa kuhusishwa na kisasi baada ya simba hao kuwala punda wawili wa wafugaji katika eneo hilo.

Taarifa zinaonesha kwamba awali simba waliokuwa wamekufa hadi saa 4:00 asubuhi walikuwa watano. Taarifa za baadaye zinaeleza kuwa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 10.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, simba hao wanadaiwa kulishwa mzoga wenye sumu, katika tukio linalodaiwa kufanywa na baadhi ya wafugaji baada ya tukio la kuuawa kwa punda wao lililoripotiwa kutokea Septemba 17, 2026.

Jeshi la Polisi pamoja na askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamefika eneo la tukio na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo na kuwabaini wote waliohusika.

Tathmini ya awali imeibua madai mengine kwamba uharibifu huo unaweza kuwa na lengo la kusababisha uhaba wa maji na hivyo kutengeneza mazingira ya kudai kuruhusiwa kwa mifugo kuingizwa katika maeneo ambayo yamewekewa zuio kwa sababu za uhifadhi.

Mamlaka zinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa kadiri taarifa zilizothibitishwa zitakavyopatikana.

View attachment 3674200View attachment 3674201
Wahusika wakamatwe haraka.
 
Hao wamasai walioua Simba watalipa gharama kubwa sana kwa walichokifanya. Watajuta. Ninaisihi serikali iwaondoe hao masai haraka sana eneo hilo wasije kusababisha madhara zaidi.
wewe uondolewe unapoishi kwa sabbu kuna jirani yako kauwa simba???
hivi unafikiri ngorongoro ni kama mtaa mmoja ??tu
ila watu bana
 
Yani hadi Simba Sasa hivi wanakula Mizoga!?
Maisha yanakwenda kasi Sanaa.
 
Back
Top Bottom