Washabiki wa Simba hakuna haja ya kuwatukana watu wa yanga! Ukweli lazima tukubali wanatucheka kwakua hatuna timu ya ushindani!
Ukitizama hata mipango ya kujenga timu ya ushindani haipo kabisa ni siasa,ubinafsi na makelele ndio yamejaa hapo Simba.
Toka tulivyofungwa tano na yanga wengi tulitegemea uongozi utakuja na mipango kabambe ya usajili Lakini hakuna jipya walilofanya zaidi ya kutumia nguvu kubwa kutafuta matokeo nje ya uwanja kuliko kujenga timu ya ushindani!
Ukitizama usajili unaofanyika kwenye hili dirisha dogo tuwe wa kweli tu hakuna mchezaji wa kuibeba timu ni vichekesho tu.
Viongozi wa Simba hawana uwezo wa kufanya maamuzi magumu wanaishi kwa historia kuwa Simba ni timu kubwa,wanasahau hata zamalek kule Egypt ilikuwa timu kubwa ila kwa sasa imebaki jina tu.
Wachezaji kama phiri,Onana,Saidoo, Bareke,Luis Miquisone, na uyu waliemleta sijui Sarr hawana uwezo wa kuifikisha Simba popote, viongozi wachukue hatua, vinginevyo Simba itabaki jina tu.