Simba barua yenu ya kugomea mechi ina mkanganyiko mkubwa,,mjitafakari kabla hayajawakuta

Simba barua yenu ya kugomea mechi ina mkanganyiko mkubwa,,mjitafakari kabla hayajawakuta

Barua hii iliyoandikwa na Simba Ina mkanganyiko sana sijui wamekurupuka ama vipi,,nimeisoma vizuri mstari baada ya mstari na nimeona wamejichanganya pakubwa!
Kwanza nukuu ya kwanza hii hapa;-
1) Nukuu''katika sintofahamu iyo Simba iriarifiwa na meneja wa uwanja kuwa hana maelekezo ya kamishna wa mchezo'' kupitia mstari huu ni wazi kuwa Simba awajazuiliwa kuingia uwanjani na mabaunsa kama walivyoainisha kwenye barua yao bali wamezuiliwa na meneja wa uwanja kwani ndie mwenye mamlaka na funguo za mageti ya uwanja kuruhusu watu waingie uwanjani!

2) Nukuu ya pili " Mabaunsa wa klabu ya yanga walivamia msafara wa Simba huku wakiendelea na vurugu na wakizuia msafara wa Simba kuingia uwanjani kufanya mazoezi" kupitia mstari huu pia Simba wameandika juu ya mabaunsa wa yanga sasa hapa najiuliza wamejuaje kwamba wale ni mabaunsa wa yanga? Ni uthibitisho upi walioutumia kung'amua kwamba wale ni mabaunsa wa yanga? Pale akukuwepo na kiongozi yeyote wa YANGA,,je walikuwa na vitambulisho? Ama jezi za yanga? Viongozi wote wa yanga wamesajiliwa tff kikanuni na Sheria za Mpira zinavyotaka akuna sehemu yanga wamesajili jina la baunsa!
Lakini pia barua ya Simba inasema mabaunsa wa yanga wamezuia timu kuingia uwanjani wakati ukiangalia Ile video lile tukio watu walikuwa nje ya uwanja Ina maana na wao awakuwa na mamlaka ya kuingia ndani ya uwanja kwakuwa meneja wa uwanja alipiga rock!
Mabaunsa wanawezaje kumzuia mtu asiingie uwanjani wakati uwanja wenyewe umefungwa?
Simba nawashauri mpeleke timu uwanjani na adhabu za kikanuni uamuliwa kikanuni na sio kugomea mechi vinginevyo point 3 na magoli 3 itakuwa ni halali ya yanga!
Kama mganga wenu aliwapa masharti magumu na mkaona imebuma vilio vingekuwa vingi muwaambie ukweli wanachama wenu na sio kichaka cha ukizuiwa kufanya mazoezi,,mbona yanga mechi iliyopita ilizuiwa kufanya pale mazoezi kwanini awakugomea mechi?
Simba ina wakati mgumu. Walifikiri wataenda kuroga, meneja akaamua kuwabania. Sasa wakubali tu leo ni ubaya ubwela. Na hakuna kususia mechi kwa sababu za kipuuzi.
 
Haki itaamuliwa kikanuni na sio vinginevyo suala la kugomea mechi ni tofauti kabisa
Tabu ipo wapi?

Simba imeona kuna mazingira yanayohatarisha mchezo kuwa fair kwa upande wa Simba, kama imekosea kanuni Yanga itapewa hizo P3 wanazozitaka sana mpaka wanazuia mazoezi.

NO REFORM NO DERBY.

Utaratibu uwe huu huu mpaka derby iwe huru.
 
Simba ina wakati mgumu. Walifikiri wataenda kuroga, meneja akaamua kuwabania. Sasa wakubali tu leo ni ubaya ubwela. Na hakuna kususia mechi kwa sababu za kipuuzi.
Kikanuni na Sheria za Mpira ziko wazi kama umesusa pasipokuwepo na sababu za msingi wenzako wanapewa point 3 na magoli 3,
 
Miaka yote ya mechi za watani,mwenyeji anakabidhiwa uwanja,mgeni anaingia uwanja siku ya mechi akitokea mahali alipoweka kambi.Ndio maana hata meneja hakuwa na taarifa za wao kuja uwanjani. Hata Yanga hii nafasi ya kutumia huu uwanja kabla ya mechi round ya kwanza hakupewa, je hizo kanuni hazikuwepo, maana aliingia uwanjani akitokea Avic Town na mechi alicheza.
 
Tabu ipo wapi?

Simba imeona kuna mazingira yanayohatarisha mchezo kuwa fair kwa upande wa Simba, kama imekosea kanuni Yanga itapewa hizo P3 wanazozitaka sana mpaka wanazuia mazoezi.

NO REFORM NO DERBY.

Utaratibu uwe huu huu mpaka derby iwe huru.
Yanga derby iliyopita walizuiwa pia na mwenyeji alikuwa Simba mbona awakugomea mechi?
 
Whatever kaka. Lakini muhimu ujumbe ufike kuwa Simba sio wannyonge kama wanavyoaminishana kwenye vikao vyao.

Uwepo wa waheshimiwa kwenye uongozi wa timu yao lazima uendane na fair competition bila kuathiri kanuni na utaratibu wa uendeshaji wa mpira wetu.
Simba na Yanga hakunaga mnyonge ni timing tu , na uzuri wanajua wanachofanya nyie mashabiki ndio hamjui
 
Yanga derby iliyopita walizuiwa pia na mwenyeji alikuwa Simba mbona awakugomea mechi?
Sasa tunajuaje kuwa mlizuiwa kama hamkutoa malalamiko rasmi? Huenda mlizuiwa, huenda ni porojo.
 
Barua hii iliyoandikwa na Simba Ina mkanganyiko sana sijui wamekurupuka ama vipi,,nimeisoma vizuri mstari baada ya mstari na nimeona wamejichanganya pakubwa!
Kwanza nukuu ya kwanza hii hapa;-
1) Nukuu''katika sintofahamu iyo Simba iriarifiwa na meneja wa uwanja kuwa hana maelekezo ya kamishna wa mchezo'' kupitia mstari huu ni wazi kuwa Simba awajazuiliwa kuingia uwanjani na mabaunsa kama walivyoainisha kwenye barua yao bali wamezuiliwa na meneja wa uwanja kwani ndie mwenye mamlaka na funguo za mageti ya uwanja kuruhusu watu waingie uwanjani!
Ukisoma kwamba kamishna alikuja hadi uwanjani na meneja akaruhusu, utakuta yote yaliyobaki uliyoandika ni nonsense
 
Kanuni zinasema Timu ngeni first leg isipoomba kufanya mazoezi kwenye uwanja tarajiwa wa mechi, basi second leg Timu ngeni nyingine nayo isiende kufanya mazoezi?
Usipende kudandia gari kwa mbele kabla ya ku reply unatakiwa kwanza uangalie comment inajibu kuhusu hoja ipi. Niliyemuuliza swali kasema kuwa kwenye derby iliyopita Yanga aliruhusiwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye huo uwanja. Nimemwambia alete video tuone kama ni kweli.

Wewe unakuja na hoja mpya kabisa
 
Mechi inachezw saa moja na robo usiku simba wameenda kwa mkapa saa moja usiku kufanya mazoezi kosa lao lipi?
Uwanja wa taifa una utaratibu wake ili uweze kuingia. Meneja hakuwa na taarifa za ujio wa simba. Ulitaka awaruhusu bila kufuata taratibu?
 
Weka h
Wewe mtu uwezo wako wa kufikiri mdogo sana. Sijui kwanini washabiki wa Yanga huwa hamna akili. Mabaunsa wa YANGA nani hawajui? Si wanajulikana? Ina maana video hamjaziona au?

Meneja wa uwanja anapokea maelekezo kwa timu mwenyeji ambae ni Yanga, na mwenyeji ndio anakabidhiwa uwanja na ndo maana anaruhusiwa kuleta mabaunsa wake.

Simba anaruhusiwa kugomea mechi kwasababu hawezi kucheza Leo wakati jana wachezaji hawakufanya mazoezi kwasababu walizuiwa. Inakubalika Dunia nzima. Huwezi peleka wachezaji uwanja wakati hawajafanya training, utaonekana makalio

Umeandika waraka mrefu wa kitu ambacho hukijui. Kweli common sense is not common
hapa kanuni inayoiruhusu Simba kugomea mechi,
 
Kwa akili za kawaida una amini ni 'Watu' wa Simba ndio wameizuia timu sio?! Au unafikiri the so called 'Makomandoo' wa Azam ndio wamefanya upumbavu ule?

Jaribu kufikiri kwa fikra huru. Ushabiki wa timu zetu usitupofushe.
Kwamba mabaunsa hao mnaowaita wa yanga ndio waliokua na ufunguo wa kuingia ndani ya uwanja? Niliona gari ya polisi imebock njia kabisa ili gari ya simba isisogee getini.

Kwa kifupi inaonekana hapakua na mawasiliano kati ya simba na meneja wa uwanja
 
Back
Top Bottom