- Thread starter
- #21
Kuna mtu kakataa kuwa uto wametuzidi uongozi ndio maana wana timu thabiti?Yani mleta uzi unaaminisha watu eti wachezaji walihongwa na yanga ili timu iishie nafasi ya 3? Pia kunampango wakutaka timu apewe mdogo wa gsm? Unaushahidi gani wa kuthibitisha shutuma zako?
Yaani tunashindwa tu kukubali kwamba wenzetu uto wamepata viongozi wa boli hasa?
Yaani wachezaji kama pacome, aziz, ibra bacca pamoja na diara wanaweza cheza timu yoyo hapa afrika ila ukitafta huku kwetu hakuna quality player yeyote ambae anaweza kutakiwa hata na petro atletico tu.
Ifike tu muda tukubali hawa uto wametuzidi na wamepata viongozi ambao ni wa mpira hasahasa.
Tunaona kila mechi ya uto lazima rais wao atakuwepo.
Simba tujenge timu tuache shutuma za kijinga, ukimsusia mchezaji anakwenda upande wa pili na anakiwasha mpaka unajuta.
Pamoja na hayo yote unadhani wanaingiza timu mbele ya Simba kizembe kizembe kama akili za wajinga zinavyodhani?
Unadhani kwa nini wanamtaka Chama na walimwita mzee akicheza chini ya kiwango?Unahisi wao ni wapumbavu ama nani kati yenu?