Simba hamutoweza kutoka hapo mlipo hadi mjifunze kunyamaza

Simba hamutoweza kutoka hapo mlipo hadi mjifunze kunyamaza

Hamida Ally mwambieni ajifunze kuongea apunguze Jazba aliongea anagongagonga Meza kwamba Yanga hivi Yanga vile

Al Ahly anagongwa na Yanga baada ya hapo tunamtaka Mamelodi sio Petro Atletico de Luanda wala Wydad Casablanca tunamtaka Mamelodi tumgonge na yeye ili tuwafumbe midomo vizuri

Mwasibu OKW BOBAN SUNZU usisahau kupita huku
 
Hatuna cha kujifunza msitulazimishe...
Lazima mjifunze kufuzu hatua ya robo fainali huku mkiwa na mchezo mmoja mkononi! Siyo kila mwaka mnakuja tu na makauli mbiu yasiyo eleweka! Mara do or die, sijui mwaka wa kisasi!!

Jifunzeni kwa kaka yenu Yanga! Ijumaa anachez na Bingwa mwenzake Al Ahly, huku wote wakiwa wameshafuzu.
 
Habari wanajukwaa Langu Pendwa hapa Jf Jukwaa la Sports.

Ni siku takribani 3 saiv zimepita toka Team Bora kwa sasa Young Africans alimaarufu kama Yanga imbamize Mwarabu goli 4 pale kwa Mkapa na kujihakikishia kusonga hatua inayofuata.

Baada ya Ushindi ule tumeshuhudia Utani Mwingi sana sehemu mbalimbali kuanzia utani wa face to face mitaaani hadi katika Mitandao ya Kijamii, Twitter(x), Instagram, Facebook hata hapa Nyumbani JAMIIFORUMS jukwaa la Sports.

 I
la sasa kitu ambacho kimenifanya niibuke hapa nakuandika ni kitu cha kushangaza kutoka kwa Mashabiki na baadhi ya watu wenye hadhi ndani ya simba kuonekana wakijibu jibu hili swala la Ushindi wa Yanga hadi kufikia hatua ya kusema hawana kitu cha kujifunza kutoka kwa Yanga Mara Yanga kushinda kumechachizwa na MO.

Ujue kuna kitu kimoja Simba hua nawasema siku zote Mnajifanya Wajuaji kwenye Kila Jambo ndio utofauti wenu na mashabiki wa Yanga au hata Viongozi wa Yanga, Nyie hamkubali hata kidogo kua kwa sasa hampo vizuri.

Tuseme kukubali ni mbaya ila mngejifunza hata kunyamaza tu maana mkinyamaza hakuna mtu atawafunga, why nasema Mnyamaze kwa sababu Ukiwa Unajibu na kuonyesha kua na wewe ushawahi fanya hivi,Mara na wewe utafuzu, Mara wewe ndio club ipo juu kwa Ranks hayo mambo yatakupumbaza sana...

Chukulia kwa Yanga mara nyingi hua tunapenda kusema mashabiki wa Yanga wamepoa ila kuna Faida yake ukimuona mtu kanyamaza kapoa yule jua anajipanga vizur so hana mda wakukujibu wewe ila utakuja kushitukia tu BOOM kama sasa hivi.

Kipindi Simba mnatamba Yanga hawakua na Mda wa kuwajibu,Mlibeba Ubingwa mar 4 mfululizo hamkuwahi sikia wakisema makombe yao waliyo nayo,Hamukuwai ona wanasema washacheza pale Egypt game moja ya Moto na Ahly ila bahat haikua kwao ilikua kidogo wamtoe hamkuwahi sikia hayo wakijivunia nayo..

Do you know WHY?
Maana walijua yaliyopita yashapita wanataka ya sasa, na wao kwa mda ule hawakua vizur so walitakiwa wajipange na wakiwa vizur ndio wataanza kujibu.

Ndio tunaona sasa hivi wapo vizuri wanafanya kila kitu wanafurahii wanawatania ila nyie mnajibu eti hatuwez jifunza kutoka kwa Yanga inachekesha sana.

Hamlazimishwi ila endeleezen hizo mbwembwe mtakuja kushituka Yanga anaubingwa mara 10 Mfululizo wa Ligi na ashabeba Caf Champions League Mara Moja au zaidi.

Sasa mkuu em tuambie simba ijifunze nini kwa yanga???

Nyinyi kujifunza ilikuwa lazima..... maana ndo tumewafikisha apo mlipo sasa” haya niambie simba haipo vizuri wapi? Maana kwemye ligi yetu hata wewe ukae kimya lolote linakukita...... club bingwa imefuzu nani kakwambia simba haifuzu? Acha mbea fatilia mambo ya team yako
 
Mi ni yanga ila kusema Yanga huwa ni wakimya napinga😂😂😂Simba na Yanga mashabiki wao wote ni waruwaru na ndio Raha ya mpira
NB nawaona Simba wakitupa standing ovation tunapopita na kombe la caf pale msimbazi
 
Sasa mkuu em tuambie simba ijifunze nini kwa yanga???

Nyinyi kujifunza ilikuwa lazima..... maana ndo tumewafikisha apo mlipo sasa” haya niambie simba haipo vizuri wapi? Maana kwemye ligi yetu hata wewe ukae kimya lolote linakukita...... club bingwa imefuzu nani kakwambia simba haifuzu? Acha mbea fatilia mambo ya team yako
Pole Akili uliziacha Tumbon kwa Mama ako
 
Hamida Ally mwambieni ajifunze kuongea apunguze Jazba aliongea anagongagonga Meza kwamba Yanga hivi Yanga vile

Al Ahly anagongwa na Yanga baada ya hapo tunamtaka Mamelodi sio Petro Atletico de Luanda wala Wydad Casablanca tunamtaka Mamelodi tumgonge na yeye ili tuwafumbe midomo vizuri

Mwasibu OKW BOBAN SUNZU usisahau kupita huku
Jamaaa anahisi kila kitu ni Mbwembwe
 
Lazima mjifunze kufuzu hatua ya robo fainali huku mkiwa na mchezo mmoja mkononi! Siyo kila mwaka mnakuja tu na makauli mbiu yasiyo eleweka! Mara do or die, sijui mwaka wa kisasi!!

Jifunzeni kwa kaka yenu Yanga! Ijumaa anachez na Bingwa mwenzake Al Ahly, huku wote wakiwa wameshafuzu.
Tafuta rekodi...
 
Mi ni yanga ila kusema Yanga huwa ni wakimya napinga[emoji23][emoji23][emoji23]Simba na Yanga mashabiki wao wote ni waruwaru na ndio Raha ya mpira
NB nawaona Simba wakitupa standing ovation tunapopita na kombe la caf pale msimbazi
Kwamba kwenda robo mnahisi mshachukua kombe??haviendagi hvyo utopolo lazima upitie nusu fainali na fainali ndo uchukue kombe.Wazoefu wa cafcl tunawafundisha utaratibu wa huku kwa wakubwa.
 
Kwamba kwenda robo mnahisi mshachukua kombe??haviendagi hvyo utopolo lazima upitie nusu fainali na fainali ndo uchukue kombe.Wazoefu wa cafcl tunawafundisha utaratibu wa huku kwa wakubwa.
Kama ndio wazoef Mlishapita hizo hatua tofauti na kua kila msimu ni Robo Nyama.
 
Back
Top Bottom