Simba hamutoweza kutoka hapo mlipo hadi mjifunze kunyamaza

Simba hamutoweza kutoka hapo mlipo hadi mjifunze kunyamaza

Habari wanajukwaa Langu Pendwa hapa Jf Jukwaa la Sports.

Ni siku takribani 3 saiv zimepita toka Team Bora kwa sasa Young Africans alimaarufu kama Yanga imbamize Mwarabu goli 4 pale kwa Mkapa na kujihakikishia kusonga hatua inayofuata.

Baada ya Ushindi ule tumeshuhudia Utani Mwingi sana sehemu mbalimbali kuanzia utani wa face to face mitaaani hadi katika Mitandao ya Kijamii, Twitter(x), Instagram, Facebook hata hapa Nyumbani JAMIIFORUMS jukwaa la Sports.

 I
la sasa kitu ambacho kimenifanya niibuke hapa nakuandika ni kitu cha kushangaza kutoka kwa Mashabiki na baadhi ya watu wenye hadhi ndani ya simba kuonekana wakijibu jibu hili swala la Ushindi wa Yanga hadi kufikia hatua ya kusema hawana kitu cha kujifunza kutoka kwa Yanga Mara Yanga kushinda kumechachizwa na MO.

Ujue kuna kitu kimoja Simba hua nawasema siku zote Mnajifanya Wajuaji kwenye Kila Jambo ndio utofauti wenu na mashabiki wa Yanga au hata Viongozi wa Yanga, Nyie hamkubali hata kidogo kua kwa sasa hampo vizuri.

Tuseme kukubali ni mbaya ila mngejifunza hata kunyamaza tu maana mkinyamaza hakuna mtu atawafunga, why nasema Mnyamaze kwa sababu Ukiwa Unajibu na kuonyesha kua na wewe ushawahi fanya hivi,Mara na wewe utafuzu, Mara wewe ndio club ipo juu kwa Ranks hayo mambo yatakupumbaza sana...

Chukulia kwa Yanga mara nyingi hua tunapenda kusema mashabiki wa Yanga wamepoa ila kuna Faida yake ukimuona mtu kanyamaza kapoa yule jua anajipanga vizur so hana mda wakukujibu wewe ila utakuja kushitukia tu BOOM kama sasa hivi.

Kipindi Simba mnatamba Yanga hawakua na Mda wa kuwajibu,Mlibeba Ubingwa mar 4 mfululizo hamkuwahi sikia wakisema makombe yao waliyo nayo,Hamukuwai ona wanasema washacheza pale Egypt game moja ya Moto na Ahly ila bahat haikua kwao ilikua kidogo wamtoe hamkuwahi sikia hayo wakijivunia nayo..

Do you know WHY?
Maana walijua yaliyopita yashapita wanataka ya sasa, na wao kwa mda ule hawakua vizur so walitakiwa wajipange na wakiwa vizur ndio wataanza kujibu.

Ndio tunaona sasa hivi wapo vizuri wanafanya kila kitu wanafurahii wanawatania ila nyie mnajibu eti hatuwez jifunza kutoka kwa Yanga inachekesha sana.

Hamlazimishwi ila endeleezen hizo mbwembwe mtakuja kushituka Yanga anaubingwa mara 10 Mfululizo wa Ligi na ashabeba Caf Champions League Mara Moja au zaidi.
Utakuwa mgeni nchi hii ama umejifunza kiswahili wiki iliyopita.

Ni yanga hawa hawa wanaojiita aidha mabingwa watetezi,ama wakilikosa kombe wanaitwa mabingwa wa kihistoria.
Ni hawa hawa yanga walioishiriki klab bingwa mara nyingi zaidi kuliko Simba na kutolewa hatua za awali,lakini wanamcheka Simba kuishia robo fainali mara nyingi.
Ni hawa hawa yanga wanaojinadi wao ni bora miaka yote kuliko Simba.
Hawa jamaa wana Sifa sana
 
Back
Top Bottom