Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Nafikiri hii ni ndoto nyevu, yanga wataleta timu tarehe 3 na mechi itachezwa vizuri tu
Na wasipopeleka timu mnyama anapewa point tatu kiroho safi kabisa...
 
Mbona hii ingekuwa mbinu nzuri sana ya kuzinyima timu ubingwa? Kwamba hufahamu kanuni kuwa timu isipoenda uwanjani, timu iliyofika uwanjani inapewa point tatu?

Hizi shule siku hizi mnaenda kujifunza nini?
 
Tatizo simba huyu ameenda pole mno hadi ataikosa nyama au atakuta imeioza. Tazama nchi zote duniani ligi zao zimefika tamati lakini ligi hii ya TFF inatarajiwa kufika tamati mwaka ujao. Haya ni maajabu ya dunia ndugu yangu Bujibuji .
Dunian wapi? Mbona sehem kibao tu ligi zinaendelea? Vipi morocco sio duniani? South Africa sio dunian ,bahat nzur umesema ww sio mtu wa soka ajabu unaonekana uyanga umekuganda sana kichwani.

Labda nikukumbushe na tunza hii comment yanga asipoleta timu uwanja Simba ubingwa upo pale pale ,alafu baada ya hapo subir uone nan ataumia kati ya yanga na tff.
 
Emergency ipi ilitokea ambayo haikuwa wazi, ingali kuwa hivyo basi ttf wangefanya yao ili wabaki bila lawama
 
Mpira wa bongo ni maigizo yasiyo na 'steringi' wala 'kubwa la maadui'
 
Lakini si kuna kikao kilifanyika baina ya hizi timu mbili kama serikali ilivyoagiza wakutane na wakakubaliana mechi kurudiwa na timu zote zikasaini.
Yanga wasipoingiza timu Simba watapatiwa points 3 na wanakabidhiwa kombe bila shinikizo la serikali na Yanga kupewa adhabu kama kawaida.
 
Kwa Faida yako tu na wana Yanga SC 'Oya Oya' Wenzako wengi hapa JamiiForums ni kwamba mpaka hivi sasa huko CAS bado hawana Ratiba ya Kuisikiliza Yanga SC na huu 'Upuuzi' wao ( wenu )

Tatizo lenu wana Yanga SC wengi siyo Watu wa Kusoma ili Kujiridhisha vyema Kitaarifa na Kimaarifa na huenda ndiyo maana imegundulika kuwa Watu wengi ambao hawajaelimika ( hawakusoma ) ni wana Yanga SC.

Na kama kuna Taasisi ya Michezo ( Soka ) inayoheshimika na kuanzia CAF hadi FIFA basi ni hii ya TFF ya Rais Bora na Mchapakazi Wallace Karia. CAS watapokea Lawama zenu ( Yanga SC ) na watawauliza na kuomba Ufafanuzi zaidi kutoka Shirikishoni ( TFF ) ambao nao pia watawapa ule Ushahidi mwingine wa Yanga SC 'Kufoji' sahihi ya aliyekuwa Mchezaji wenu Bernard Morrison.

Ismail Aden Rage aliwashaurini vizuri sana kuwa achaneni na hii Kesi kwani hamtashinda na mtapoteza bure tu muda wenu ila hamumuelewi na mnajifanya Wabishi, mnajua na mna Kiburi mno.

Wanachofanya Viongozi wa Yanga SC ni kila wakiona ( wakisikia ) Mchezaji Bernard Morrison anafanya vizuri na Simba SC 'wanaibuka' nae kwa 'Kuliibua' Sakata lake huku 'wakimhonga' na Yule 'Mpuuzi' Mwenzenu mwingine Mtangazaji wa Wasafi FM 'Mnafiki' Maulid Kitenge alishikie bango ili wana Yanga SC mjiamini na muamini kuwa huko CAS mtafanikiwa tu.

Namalizia kwa Kutoa hii 'Siri' ambayo sikutaka Kuitoa Kwenu ( wana Yanga SC ) ila kwakuwa 'mmechokoza' leo nawaambieni kuwa aliyemuuza Mchezaji Bernard Morrison kuja Yanga SC kutoka Yanga SC ni Injinia Hersi Said Mwenyewe kwa Baraka zote za 'Boss' wake Gharib Said Mohammed ( GSM ) ambaye ni mwana Simba SC na mpaka Kadi ya Uanachama wa Simba SC anayo kama ilivyo kwa Afisa Mhamasishaji wenu Antonio Nugaz ambaye Binafsi kama GENTAMYCINE namjua ni mwana Simba SC 'lia lia' hadi Wanafamilia wake wa hapa Dar es Salaam na Kwao Tanga.

Siku nyingine ikinipendeza au nikijisikia kusema hapa nitawapeni wana Yanga SC Siri iliyojificha nyuma ya Kauli ya 'Kujiamini' ya Msemaji wa Simba SC Haji Manara 'Bugatti' ya kwani mara kwa mara anasema Simba SC itachukua Ubingwa wa 'back to back' mara Kumi ( 10 ) mfululizo.
 
Endapo viongozi Wa Yanga watapeleka timu uwanjani basi yafaa wachapwe viboko hadi wachaniwe nguo zao wabaki utupu,mana itabidi wawaeleze washabiki na wanachama juu kukataa kucheza mchezo ulopita!
 
Mbona umepaniki sana? Hatuleti timu kufa sasa![emoji16]
 
Watapatiwa alama tatu kwa maelekezo ya serikali ama?[emoji3]
 
Ngoja niwape ujanja TFF.

TFF wawape Yanga point tatu, halafu Simba wapewe adhabu kwa kutofika uwanjani. Kwa kuwa Simba na TFF ni damu damu, basi Simba watakaa kimya.

Ila , TFF wakitaka kushindana na Yanga, mwisho utakuwa mbaya kwa upande wa TFF.

Kwa sasa, kuna utandawazi, siyo kwamba malalamiko hayatafika FIFA. Mashabiki wa Yanga walishaandika barua FIFA, ila FIFA wameiweka pending huku wakifuatilia kwa umakini mpaka ligi iishe.
 
Haahhaaa ahahaaaa wanatia aibu sanaaa watopolo
 
wata prove kua ni wajinga na walikurupuka kufanya maamuzi na hakuna atakaewaelewa.
 
"Mimi sio mtu wa mpira kiviiiiile lakini nadhani Yanga wapo sahihi kwa asilimia 90%"

Tulia nenda ukapete mchele au kafume vitambaa
Yes. Ndio maana sijaweka 100% kiongozi wangu. Kama ningekuwa mtu wa mpira ningeweka 100% au 0% kwa uhakika kabisa. Unajua udekezaji wa Yanga na Simba unaofanywa na TFF ndio uliotufikisha hapa. Wewe fikiria Yanga hawakupeleka timu lakini hadi leo hawajachukuliwa hatua yoyote. Sasa utawezaje kusema kuwa walikuwa sahihi kwa 100% wakati hawakuadhibiwa?

Anyway, tuache hayo ya Yanga na Simba. Je wale washabiki waliolipa kiingilio na hawakuona mpira watarejeshewaje fedha zao? Na tayari tiketi zao zimechanwa!!!
 
Endeleeni kuamini hivyo na mawazo yenu ya kiutopolo. Mmeshindwa mpira uwanjani mnaaanza kulalama. Mapimbi kweli nyie. [emoji38][emoji38][emoji38]
 

yani umejifichaficha kuwa wewe sio yanga lakini njia ya mwongo fupi. wewe ni utopolo. nakuonea huruma sana kuwa haya unayotabiri yatakupukutikia mikoni. kwa taarifa tu yanga itakuja julai 3 na mechi itachezwa. nani ajuaye, labda yanga atashinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…