Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Mnazingua sana mnajikuta viazi mnaleta tu nyuzi ambazo hazina mashiko sisi tunategema jf kukuta vitu smart sa nikikutana na huu utopolo nashindwa kujizuia
Kwa hiyo unachotaka nini au unatafuta ban nimuite Moderator aje kufanya kazi yake?
 
Achana na stori za vijiweni. Yanga umefafanua zaidi ya mara 2 utapeleka timu uwanjani. Mwanzo alipotoa tamko Bumbuli kesho yako Yanga wakamkana,juzi pia Yanga waliwakana wazee waliosema hawaendi uwanjani. Sasa hizo stori za Yanga kutopeleka timu unazitoa wapi?

Halafu unachosema ni vitu vya kufikirika,ingekuwa rahisi hivyo si timu nyingi tu zingekuwa zinahujumu wengine kwa kutokufika uwanjani. Kanuni zipo wazi,kinachotumika ni busara tu. Wajidanganye wasilete timu
Umekurupuka, soma tena hoja yake na umuelewe vizuri.
 
Tatizo simba huyu ameenda pole mno hadi ataikosa nyama au atakuta imeioza. Tazama nchi zote duniani ligi zao zimefika tamati lakini ligi hii ya TFF inatarajiwa kufika tamati mwaka ujao. Haya ni maajabu ya dunia ndugu yangu Bujibuji .

Ukiwa muongo uwe pia na kipaji cha kumbukumbu,umeshaona ligi ya Egypt inamalizika lini? Umejitahidi hapo juu kujitetea wewe si mtu wa mpira kivile,na huku kwenye Comment unatiririka ki Utopolo style.Tulieni,tar 3 tunatangaza ushindi mbele yenu
 
Wewe ndio kilaza halafu hujijui kama ni kilaza. Taarifa ya kusogeza mbele mchezo ilikuwa wazi na haikutaja mambo unayoyawaza wewe. Na hata ikitokea kesi imeenda mbali basi huko mbali watataka hiyo taarifa ya kuahirisha mchezo ilikuje!? Ilitolewa na nani na kwa sababu zipi?
Unaona ulivyo bwabwa ,embu soma tena ulichocomment alaf jipige kichwan sema mm ni shoga a.k.a bwabwa niliyejaza kinyesi kichwan badala ya ubongo
 
Sheria inasema muda wa mchezo ukikaribia ingiza timu uwanjani, na baada ya muda wa mchezo kufika subiria nusu saa uwanjani kama.timu haijaingia uwanjani ondoa timu uwanjani na inahesabika mpinzani hajafika mchezoni, Yanga waliondoa timu saa 17:30 hapo Simba anahesabika amekimbia mechi.
Wakat yanga anaingia uwanjan kulikwepo marefa na viongozi wa meza kuu? Ukijibu hili bila unafki ntajua kweli unazijua kanuni za mpira
 
hivi ukiwa utopolo na akili zinahama, yaani mtu anaamka na kupost upuuzi kama huu.
Gomeeni kuja tarehe 3 halafu muone Fifa watachukua maamuzi gani.
 
Wakat yanga anaingia uwanjan kulikwepo marefa na viongozi wa meza kuu? Ukijibu hili bila unafki ntajua kweli unazijua kanuni za mpira
Kikubwa bi Pre March meeting ilifanyika asubuhi na kila timu ikawasilisha list ya wachezaji, na waamuzi wakatambushwa, kawaida ikifanyika pre March basi mchezo upo
 
Jambo wakuu!

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha. Naomba niwatonye jambo moja la hatari linaloinyemelea soka ya Tanzania endapo TFF hawatachukua hatua zinazofaa kuepushia mbali hatari hii.

Mechi iliyopita kati ya Simba na Yanga ilishindikana kuchezeka baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kugoma kupeleka timu kiwanjani kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni zinazoendesha ligi kuu (VPL). Huenda kweli madai yao yalikuwa na mashiko ndio maana hadi leo hawajachukuliwa hatua zozote za kinidhamu kama ilivyo kawaida. Na kwa bahati mbaya, hadi leo hakuna mtu yeyote (sio serikali, TFF, bodi ya ligi au wizara ya michezo) aliyetoa sababu za msingi za kuahirishwa kwa mechi ile, licha ya kwamba Yanga wanainyooshea kidole TFF kwa kuvuruga muda wa mchezo bila sababu zinazoeleweka.

Mimi sio mtu wa mpira kiviiiiile lakini nadhani Yanga wapo sahihi kwa asilimia 90% kwa kuwa TFF wameshindwa kuwaadhibu kwa kugomea mchezo au kutoa maelezo kuhusu kadhia nzima. Nina wasiwasi mchawi ama yupo ndani ya TFF au bodi ya ligi. Ndio maana wanashindwa kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe ili kuepuka aibu. Pia wanakwepa kudaiwa fidia na timu za Yanga na Simba kwani awali timu hizi zililalamika kutumia gharama kubwa za maandalizi ya mchezo husika na hivyo kutaka aliyeharibu mchezo kuwalipa fidia.

Jambo jingine linalowaumiza vichwa TFF ni kuhusu mamilioni ya fedha za mashabiki walizokusanya kama viingilio. Je, fedha hizi zinarejeshwaje kwa wahusika na watawatambuaje? Tukumbuke kuwa tiketi za mashabiki zilichanwa kabla ya kuingia kiwanjani.

Utamu wa utata huu unaanzia hapa. Sikiliza kwa makini. Kwa muijbu wa sheria na kanuni za TFF, ili timu itangazwe kuwa bingwa wa ligi ni lazima iwe imecheza jumla ya mechi 34 kwa msimu huu wa ligi (2020/2021). Hii ni kwa sababu kuna jumla ya timu 18 katika ligi, ambapo kila timu ikicheza dhidi ya timu zote (home and away) inapaswa kukamilisha jumla ya mechi au michezo 34.

Lakini mwelekeo unaonyesha Yanga hawapo tayari tena kupeleka timu kucheza dhidi ya Simba. Viongozi wao wameishasema tena na tena kwamba wao wameishacheza huo mchezo na hawako tayari kupeleka timu kiwanjani kwa namna yoyote ile. Kwa maana hiyo, ikiwa Yanga wataendelea na msimamo huu maana yake ni kuwa, mpaka msimu unamalizika Simba watakuwa wamecheza jumla ya michezo 33, hivyo kukosa uhalali wa kisheria kukabidhiwa kombe la ushindi. Na kwa kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa hata Simba wakicheza michezo 33 wana uwezo wa kuchukua kombe, Yanga wamewatega TFF walikoroge walinywe. Wanawasubiri wausage mtama wabugie wenyewe!

Movie nzima iko hivi: endapo TFF wataogopa kuwakabidhi Simba kombe lao kwa kuogopa kuadhibiwa na Yanga, basi serikali itaingilia kati ili Simba wakabidhiwe kombe kwa nguvu na kinyume cha sheria za FIFA. Ifahamike kwamba sheria za FIFA zinakataza serikali kuingilia mambo ya michezo na adhabu ya papo kwa papo itakayotolewa ni kuifungiwa kwa TFF, hivyo kupelekea ligi yetu kufutwa na timu zetu kutoshiriki mechi za kimataifa. Aidha, Yanga nao watakimbilia mahakamani kuwashitaki TFF kwa kuwakabidhi Simba kombe kinyume cha sheria. Hapa sasa movie itakuwa imefikia patamu sana. Matokeo yake TFF watapigwa rungu ya pili na FIFA kwa kusababisha masuala ya soka kupelekwa mahakamani. Yanga wanafanya hivi kwa makusudi ya kuwakomoa Simba (watani wa jadi) ama kwa kujua au kutokujua madhara yake ya ujumla kwa mpira wa Tanzania.

The ultimate END of this fantastic movie is that TFF will be banned forthwith by FIFA and Simba will not be crowned the championship of VPL this season. Kwa hiyo sasa nchi itaingizwa kwenye migogoro ya FIFA moja kwa moja na ligi ya VPL itasahaulika duniani. Wapenzi wa mpira katika nchi hii wajiandae kisaikolojia kutazama mashindano ya ndondo. Hakutakuwa na mashindano ya VPL msimu ujao.

Nawasilisha.​
Kuna hesabu umepiga hapa zimekaa ki utopolo utopolo tu. Kama Simba atacheza mechi 33 basi Yanga nayo watakua wamecheza idadi hiyo hiyo ya Mechi. HaHaiewezekaniimba awe amecheza mechi 33 wakati Yanga awe amemaliza mechi zake zote wakati Timu hizi zinapaswa kukutana.

Pili hata tukiamua kuwapa Yanga ushindi wa Mechi ile ambayo haikuchezwa ili lengo lao la kuikwepa Simba litimie (aibu), Simba haitegemei points hizo tu ndo iwe Bingwa. Mtaji wa Points ilizojikusanyia, na inazoendelea kujikusanyia unaifanya Simba iiache mbali sana Yanga kiasi cha kwamba ubingwa uko pale pale tu.

Nje ya mada mbona hutuletei ile mikeka yako ya premier bet bro tupige hela? Kuna behewa flan hivi ulikua ukitupia hatukosi kadhaa
 
Ligi za Kenya,Misri,Moroco...... zenyewe zipo sayari ya Mars au jaribu kujificha utopolo wako
Tatizo simba huyu ameenda pole mno hadi ataikosa nyama au atakuta imeioza. Tazama nchi zote duniani ligi zao zimefika tamati lakini ligi hii ya TFF inatarajiwa kufika tamati mwaka ujao. Haya ni maajabu ya dunia ndugu yangu Bujibuji .
 
Kinachonipa shida Tu ligi zote duniani zilisimama Tanzania ikafungua ligi mapema Sana kabla ya nchi nyingi.

Chukulia mfano ligi ya uingereza yenye timu 20 ishamalizika, na walianza nyuma ya ligi yetu, sisi timu 18 mpaka sasa ligi haijaisha

Hapa ndiyo utajua kuwa ubingwa unaandaliwa tena kichawi chawi TFF ndiyo waandaaji wa ligi mbovu kama hii.

Ndiyo maana hata Voda wakaamua kujiondia kufadhiri ligi mbovu ya TFF
 
Back
Top Bottom