Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Simba hatarini kupokonywa kombe; TFF kufungiwa na FIFA kwa sababu ya Yanga

Maana ya mechi kuchezwa hii, kuwepo na timu moja ya ushindani, kamisaa na refedii wa mchezo. Ikitokea timu moja ikaingia mitini, taratibu zote za kimpira zitafuatwa na refa atanzisha na kumaliza mpira na kumpa ushindi timu iliyopo. Hivyo hii mechi nayo itakuwa imechezwa na iko kikanuni kabisa. Kwa utaratibu huu hakuna mechi ambayo itapita bila kuchezwa kwa kigezo cha timu moja kutokuja uwanjani.
Ndio maana yake mkuu. Ili ushindi uwe VALID lazima mshindi acheze mechi zote; vinginevyo huo ushindi utakuwa BATILI. Kama TFF watarogwa wakatoa kombe kwa Simba (hata kama watakuwa na pointi nyingi), Yanga watawashikisha adabu ambayo hawatakuja kuisahau hapa duniani.
 
Jambo wakuu!

Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha. Naomba niwatonye jambo moja la hatari linaloinyemelea soka ya Tanzania endapo TFF hawatachukua hatua zinazofaa kuepushia mbali hatari hii.

Mechi iliyopita kati ya Simba na Yanga ilishindikana kuchezeka baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kugoma kupeleka timu kiwanjani kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni zinazoendesha ligi kuu (VPL). Huenda kweli madai yao yalikuwa na mashiko ndio maana hadi leo hawajachukuliwa hatua zozote za kinidhamu kama ilivyo kawaida. Na kwa bahati mbaya, hadi leo hakuna mtu yeyote (sio serikali, TFF, bodi ya ligi au wizara ya michezo) aliyetoa sababu za msingi za kuahirishwa kwa mechi ile, licha ya kwamba Yanga wanainyooshea kidole TFF kwa kuvuruga muda wa mchezo bila sababu zinazoeleweka.

Mimi sio mtu wa mpira kiviiiiile lakini nadhani Yanga wapo sahihi kwa asilimia 90% kwa kuwa TFF wameshindwa kuwaadhibu kwa kugomea mchezo au kutoa maelezo kuhusu kadhia nzima. Nina wasiwasi mchawi ama yupo ndani ya TFF au bodi ya ligi. Ndio maana wanashindwa kuadhibiana wenyewe kwa wenyewe ili kuepuka aibu. Pia wanakwepa kudaiwa fidia na timu za Yanga na Simba kwani awali timu hizi zililalamika kutumia gharama kubwa za maandalizi ya mchezo husika na hivyo kutaka aliyeharibu mchezo kuwalipa fidia.

Jambo jingine linalowaumiza vichwa TFF ni kuhusu mamilioni ya fedha za mashabiki walizokusanya kama viingilio. Je, fedha hizi zinarejeshwaje kwa wahusika na watawatambuaje? Tukumbuke kuwa tiketi za mashabiki zilichanwa kabla ya kuingia kiwanjani.

Utamu wa utata huu unaanzia hapa. Sikiliza kwa makini. Kwa muijbu wa sheria na kanuni za TFF, ili timu itangazwe kuwa bingwa wa ligi ni lazima iwe imecheza jumla ya mechi 34 kwa msimu huu wa ligi (2020/2021). Hii ni kwa sababu kuna jumla ya timu 18 katika ligi, ambapo kila timu ikicheza dhidi ya timu zote (home and away) inapaswa kukamilisha jumla ya mechi au michezo 34.

Lakini mwelekeo unaonyesha Yanga hawapo tayari tena kupeleka timu kucheza dhidi ya Simba. Viongozi wao wameishasema tena na tena kwamba wao wameishacheza huo mchezo na hawako tayari kupeleka timu kiwanjani kwa namna yoyote ile. Kwa maana hiyo, ikiwa Yanga wataendelea na msimamo huu maana yake ni kuwa, mpaka msimu unamalizika Simba watakuwa wamecheza jumla ya michezo 33, hivyo kukosa uhalali wa kisheria kukabidhiwa kombe la ushindi. Na kwa kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa hata Simba wakicheza michezo 33 wana uwezo wa kuchukua kombe, Yanga wamewatega TFF walikoroge walinywe. Wanawasubiri wausage mtama wabugie wenyewe!

Movie nzima iko hivi: endapo TFF wataogopa kuwakabidhi Simba kombe lao kwa kuogopa kuadhibiwa na Yanga, basi serikali itaingilia kati ili Simba wakabidhiwe kombe kwa nguvu na kinyume cha sheria za FIFA. Ifahamike kwamba sheria za FIFA zinakataza serikali kuingilia mambo ya michezo na adhabu ya papo kwa papo itakayotolewa ni kuifungiwa kwa TFF, hivyo kupelekea ligi yetu kufutwa na timu zetu kutoshiriki mechi za kimataifa. Aidha, Yanga nao watakimbilia mahakamani kuwashitaki TFF kwa kuwakabidhi Simba kombe kinyume cha sheria. Hapa sasa movie itakuwa imefikia patamu sana. Matokeo yake TFF watapigwa rungu ya pili na FIFA kwa kusababisha masuala ya soka kupelekwa mahakamani. Yanga wanafanya hivi kwa makusudi ya kuwakomoa Simba (watani wa jadi) ama kwa kujua au kutokujua madhara yake ya ujumla kwa mpira wa Tanzania.

The ultimate END of this fantastic movie is that TFF will be banned forthwith by FIFA and Simba will not be crowned the championship of VPL this season. Kwa hiyo sasa nchi itaingizwa kwenye migogoro ya FIFA moja kwa moja na ligi ya VPL itasahaulika duniani. Wapenzi wa mpira katika nchi hii wajiandae kisaikolojia kutazama mashindano ya ndondo. Hakutakuwa na mashindano ya VPL msimu ujao.

Nawasilisha.​
Hadithi za kahawani.
 
Bodi ya Ligi walitangaza Mechi imefutwa na Itapangiwa tarehe Nyingine..

Nani angepewa hizo point za mchezo Uliosemekana Umefutwa..??
Kwenye katiba ya TFF kuna kipengele cha kufutwa mechi au ni umbumbu tu umetumika kufuta ile mechi? Mpira wa Tanzania bado unaendeshwa kijima sana.
 
1.Simba atapigwa na Yanga tarehe 3/7 bila wasiwasi kwa makubaliano ya kikao.
2. Au tff watoe point 3 na goli kwa Yanga simba iendelee kutafuta ubingwa wake Kwengine.
Nb: Tunzeni comment hii [emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]
 
Huwa nawaambia Yanga ni kubwa kuliko taasisi yoyote ya Michezo hapa nchini watu hawataki! na niliwahi sema ili kudhihirisha hilo Mwakalebela ataachiwa muda si mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app

Asingelialia kuomba Samahani akatizama angefutiwa adhabu.

Hata Ndolanga na Rage walilialia wakatolewa Jela, Je na wao ni Wakubwa kuliko Taasisi za Michezo?
 
Kuna uwezekano mkubwa waYanga kujifungisha kwa biashara leo kli kuondoa kabisa uwezekano wa kujikuta katika meno ya Simba!! Hiyo tarehe tatu piga ua yanga hataingiza timu uwanjani!! Wenyewe wanasema heri lawama kuliko fedheha ya kupigwa mkono au wiki!!
 
Kwenye katiba ya TFF kuna kipengele cha kufutwa mechi au ni umbumbu tu umetumika ile mechi? Mpira wa Tanzania bado unaendeshwa kijima sana.
Hapo ndio sijui.. mi najua TFF walibugi kusogeza Mechi kinyume na Sheria
 
Kwenye katiba ya TFF kuna kipengele cha kufutwa mechi au ni umbumbu tu umetumika ile mechi? Mpira wa Tanzania bado unaendeshwa kijima sana.
Mechi ilisogezwa mbele mkakataa, basi ikafutwa kabisa Bado mnakataa mnataka mpewe points za mechi ambayo hata Refa hakuwepo.

Hivi mkiambiwa hata kulikua na tishio la kiusalama mpaka ikasogezezwa mbele mtasemaje? Timu ya Wananchi lakini mmeamua kuwaumiza Wananchi waliolipa kuingilio.
 
IMG-20210625-WA0216.jpg
 
Yanga utaenda mahakama I kwa Lili wakati wanajua FIFA hairusu kwenda mahakamani.kanuni zipo wazi itafungiwa
 
Katika historia yangu ya kufuatilia mpira wa Tanzania sijawahi kuona Rais wa TFF ng'ombe na mbumbumbu kama Karia. Nashangaa kwanini amechukua fomu kugombea tena wakati uongozi wake umeharibu sana mpira wa nchi hii. Ikiwa suala dogo tu la kurudisha viingilio vya mashabiki linamshinda, uongozi gani anataka tena? Mpuuzi kabisa.
 
Uongozi wa Yanga wameishakataa kata kata ( kupitia kwa msemaji wao) kupeleka timu kiwanjani. Wewe unaishi duniani gani mkuu?
Mtu anaokoa roho yake,nyinyi mnamlazimisha akutane uso kwa uso na Simba,si wauwaji nyinyi!!! Ebooo!
 
Back
Top Bottom