Usomeni huu uzi kama wachambuzi na sio Mashabiki ama wapenzi wa timu na Taasisi tajwa.
Iwe Yanga wataingiza Timu uwanjani ama lah hiyo tar3, iwe wameshamalizana na wamekubaliana kulimaliza kwa kuurudia mchezo au vinginevyo... bado hili suala si lakulichukulia juu juu kama tuzoeavyo.
Jaribu kuyachambua haya.
Kwanini Simba haikupewa ushindi wa mechi ile na ilifika uwanjani muda wa mchezo, yanga hawakuonekana?
Kwanini Yanga haijapewa Adhabu kwa kutokuingiza timu uwanjani au kutoa timu uwanjani kabla ya mchezo kuanza?
Ni mikakati gani ya mchezo ujao iliyowekwa kufidia gharama za mechi kwa ujumla kuanzia mashabiki mpaka taasisi na makampuni. Na ni nani atapaswa kuzilipa yakitokea madai?
Achana na Yanga Ama Simba, akitokea hata mtaka sifa mmoja na mwenye uelewa mzuri wa masuala ya mpira wa miguu na sheria zake, hili suala linaweza kufikia aliwazalo mleta mada.
BADO TUNASAFARI NDEFU SANA KATIKA KUELEWANA