Simba ikikaribia kupata mgao wa CAF lazima Mohamed Dewji aibuke

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Kama mashabiki wa Simba hakika tumekubali unyonge sema tu hakuna la kumfanya huyu big boss wetu, naye ameshalijua hilo. Anaongea analojisikia, anafanya analojisikia, mara Rais wa heshima, akajipa na hicho cheo au wanachama wenzangu tulimpa hicho cheo kwenye kikao gani?

Jana Boss mkubwa alisikika akisema Simba inamtia hasara na kama isingekuwa Simba hakika angekuwa na ndege zake kadhaa kama Emirates ila kinachomkwamisha kumiliki Airbus kadhaa ni Simba.

Anakuja na hesabu zake za magazijuto ambazo hata hazieleweki kabisa; mara nimetoa bilioni 1.5 kwa ajili ya usajili, jiulize ni chezaji gani la Simba pale limesajiliwa hata kwa milioni 100 au mnataka Sawadogo? It's ok, boss wewe, sawa tu, sijui watuonaje.

Ukitaka kugombana na boss muulize vipi kuhusu zile bilionI 20 atapiga hesabu zake za magazijuto na kukwambia tayari nimeshatumia bilioni 50 za kwangu toka mfukoni. Hakika Kigwangala adumu zaidi, nahisi alishaona harufu ya kupigwa. Na sisi mashabiki hatujawahi kuuliza hata taarifa ya mapato na matumizi, mbaya zaidi tunamlinda boss mkubwa.

Swali dogo, kama Simba inampa hasara kwanini asikae pending akaachia wengine?

Asilimia kubwa ya Tajiri, ngonjera zake zinaanza akishahisi mpunga wa CAF unataka kuingia. Baada ya kuingia robo, kuna salio Simba inapokea, bilioni kadhaa. Hapo hesabu ni ndogo tu jana kasema katumia Bilion kadhaa kwa usajili, kwa hiyo atajilipa kupitia Bilion za CAF. Natumai huo mpunga unaingia kwenye akaunti yake na hakuna wa kuhoji.

Waacha tuendelee kupigwa, tumechagua upande wa kupigwa.
 
Mo anaoambana sana pale Simba.ila Kuna vijana hawana nidhamu wanabeza juhudi za mo.

Hawajui timu inafanya yote hayo kama safari za mechi za ugenini na nje ya nchi ni mwendo WA ndege tu. Hamjui kama hizo Hela anatoa mo dewji....??

Kuna vitoto vipuuzi humu eti mo tapeli anainyonya Simba
 

Unataka kusemaje mkubwa mbona unaandika huku utetemeka hebu jiulize simba imeanza kushiriki michuano ya kimataifa miaka mingapi je kabla ya hapo walikua wanaenda na malori nini hizo nchi.
 
Mudy kachungulia mbali hapo anawaset makolo fc kabla Dola laki sita na nusu haijangia kwenye account.Itoshe kusema Mudy anakula na kipofu bahati mbaya kagusa mkono wa kipofu ndio anaangalia namna ya kumpooza kipofu
 
Ndiyo maana hata hela ya usajili hatoi timu inaishia kusajili wachezaji rejected kina Sawadogo
 
Kwa uelewa wako. Sikushangai.
Simba na Yanga ni timu zinazomilikiwa na serikali, kama hujui hili ni bora ukae kimya.

Hakuna mtu yeyote si Mo Dewji wala GSM watakuja kumilikishwa hizi timu.

Jiulize michakato yao mbona haikamiliki miaka nenda rudi?
 
Kiufupi hataki tena kusikia, sijui 20B. Ametoa zaidi ya hiyo, simba mkae kwa kutulia.
Mnawajua wahindi mnawasikia?
 
Simba na Yanga ni timu zinazomilikiwa na serikali, kama hujui hili ni bora ukae kimya.

Hakuna mtu yeyote si Mo Dewji wala GSM watakuja kumilikishwa hizi timu.

Jiulize michakato yao mbona haikamiliki miaka nenda rudi?
Hakuna tatizo, hata ardhi yote inamilikiwa na serikali nlakini tunasema "kiwanja changu", "shamba langu" na tunajenga nyumba zetu.
 
Ndiyo maana nimewauliza hao, wanawajua wahindi au wanawasikia tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…