Simba ikikaribia kupata mgao wa CAF lazima Mohamed Dewji aibuke

Simba ikikaribia kupata mgao wa CAF lazima Mohamed Dewji aibuke

Hakuna tatizo, hata ardhi yote inamilikiwa na serikali nlakini tunasema "kiwanja changu", "shamba langu" na tunajenga nyumba zetu.
Ndio uelewa, Simba na Yanga zinamilikiwa na serikali, na Sheikh Karume ndio alitowa pesa za hayo majengo ya hizo club Jangwani na Msimbazi.

Sunderland ndio ilikuwa timu ya Waarabu serikali wakaipora kutoka kwa wamiliki wakaibadili jina na ikapewa jina la Kawawa Simba wa Vita.

Mo Dewji anaujuwa ukweli na GSM wanaujuwa ukweli, wanakula na vipofu lakini wenye timu wenyewe halisi wapo, au muulize Manji atakueleza vizuri.
Hakuna tatizo, hata ardhi yote inamilikiwa na serikali nlakini tunasema "kiwanja changu", "shamba langu" na tunajenga nyumba zetu.
 
Mo anaoambana sana pale Simba.ila Kuna vijana hawana nidhamu wanabeza juhudi za mo.

Hawajui timu inafanya yote hayo kama safari za mechi za ugenini na nje ya nchi ni mwendo WA ndege tu. Hamjui kama hizo Hela anatoa mo dewji....??

Kuna vitoto vipuuzi humu eti mo tapeli anainyonya Simba
Kama anapata hasara kwanini anaforce kuendelea kupata hasara??
 
Kama mashabiki wa Simba hakika tumekubali unyonge sema tu hakuna la kumfanya huyu big boss wetu naye ameshalijua hilo hatuna la kumfanya anaongea analojisiki anafanya analojisikia mara rais wa heshima akajipa na hicho cheo au wanachama wenzangu tulimpa hicho cheo kwenye kikao gani.

Jana Boss mkubwa alisikika akisema Simba inamtia hasara na Kama isingekua Simba hakika angekua na ndege zake kadhaa kama Emirates ila kinachomkwamisha kumiliki Airbus kadhaa ni Simba, anakuja na hesabu zake za majazijuto ambazo hata hazieleweki kabisa mara nimetoa bilion 1.5 kwa ajili ya usajili, jiulize ni chezaji gani la simba pale limesajiliwa hata kwa milion 100 au mnataka Sawadogo its ok boss wewe sawa tu sijui watuonaje.

Ukitaka kugombana na boss muulize vipi kuhusu zile bilion 20 atapiga hesabu zake za magazijuto na kukwambia tiyari nimeshatumia bilioni 50 za kwangu toka mfukoni hakika Kigwangala adumu zaidi nahisi alishaona harufu ya kupigwa. Na sisi mashabiki hatujawahi kuuliza hata taarifa ya mapato na matumizi mbaya zaidi tunamlinda boss mkubwa.

Swali dogo kama Simba inampa hasara kwanini asikae pending akaachia wengine.

Asilimia kubwa ya Tajiri ngonjera zake zinaanza akishahisi mpunga wa CAF unataka kuingia baada ya kuingia robo kuna salio Simba inapokea bilioni kadhaa hapo hesabu ni ndogo tu jana kasema katumia Bilion kadhaa kwa usajili kwa hiyo atajilipa kupitia Bilion za CAF natumai huo mpunga unaingia kwenye akaunti yake na hakuna wa kuhoji.

Waacha tuendelee kupigwa tumechagua upande wa kupigwa.
Mo ni kichefuchefu
 
Kama hapato faida SI aiache klabu? Unawezaje kufanya biashara ambayo Kila uchwao inakupa hasara.
 
Ndiyo maana nimewauliza hao, wanawajua wahindi au wanawasikia tu?
Tunawsjuwa sana kuliko unavyofikiria.

Kwanza tusi generalise kuhusu Wahindi. Wahindi wapo wa makabila nanjamii na lugha tofauti tofauti kukiko unavyofikiria.

Hapa tumuongelee Mo. Kazaliwa Tanzania, tena Singida, kakulia singida mpaka alivyikwendankujiendelezankwa masomo yake huko USA. Alipirudi hakukaa sana akajiingiza kwenye siasa na hatimae akawa mbunge wa Singida.

Akafanya biashara zake, zimekuwa ni mfano kwa Africa mpaka nchi zingine nje ya Tanzania zimempa nyadhifa kwa uwezo wake. Nengi mengineyo ni haya tunayasoma kila siku kwenye media.

Tumjuwe vipi zaidi utakavyo?
 
Mamaa naelewa wako wa makabila tofauti, nimeishi nao ila sitapenda kuingia ndani zaidi.
Kusema wahindi unawajua, sina neno tofauti na hili.

Ni kama mtu asema Watanzania huwajui wewe? Hiyo ndiyo asili yake, Mtanzania mwenye asili ya kihindi. Zaidi wana simba wanajua wanachodai, nayeye kishasema katumia zaidi ya wanachokisema siku zote. Uwe na jioni njema ikielekea usiku ... 🙌🏻🙌🏻🙌🏻😅😅😅😅😅
 
Mo anaoambana sana pale Simba.ila Kuna vijana hawana nidhamu wanabeza juhudi za mo.

Hawajui timu inafanya yote hayo kama safari za mechi za ugenini na nje ya nchi ni mwendo WA ndege tu. Hamjui kama hizo Hela anatoa mo dewji....??

Kuna vitoto vipuuzi humu eti mo tapeli anainyonya Simba
Siyo wapenenzi wa Simba hao, hao Ni wa upande wa pili. Watu wa Simba hakuna asiyejua juhudi za MO.

Nimesikiliza maelezo yote ya MO katika interview ile, hakuna lolote baya alilopjibu. Waache kutafsiri kwa uvhochezi.
Mtu amejibu nipo tayari vyovyote iwavyo kufanya kwa ajili ya mapenzi yake kwa Simba SC. Anakwambia hahesabu hasara kuifadhili Simba.
Mtu ameulizwa, unatoa fedha zako kwa Simba, je, unaweka kwa faida au kwa hasara. Ndiyo maana akajibu, "ndiyo Kuna hasara, kama ingekuwa fedha ninayotoa kwa Simba nimetumia kivingine, ningeweza hata kununua ndege. Lakini sihesabu kama ni hasara kwa vile naipenda sana Simba SC tangu utoto wangu. Hivyo natoa fedha kwa Simba kwa kuopenda"
Haya sasa, onyesheni ubaya wa majibu hayo enyi wanafiki na wafitini.
 
Back
Top Bottom