bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Kama mashabiki wa Simba hakika tumekubali unyonge sema tu hakuna la kumfanya huyu big boss wetu, naye ameshalijua hilo. Anaongea analojisikia, anafanya analojisikia, mara Rais wa heshima, akajipa na hicho cheo au wanachama wenzangu tulimpa hicho cheo kwenye kikao gani?
Jana Boss mkubwa alisikika akisema Simba inamtia hasara na kama isingekuwa Simba hakika angekuwa na ndege zake kadhaa kama Emirates ila kinachomkwamisha kumiliki Airbus kadhaa ni Simba.
Anakuja na hesabu zake za magazijuto ambazo hata hazieleweki kabisa; mara nimetoa bilioni 1.5 kwa ajili ya usajili, jiulize ni chezaji gani la Simba pale limesajiliwa hata kwa milioni 100 au mnataka Sawadogo? It's ok, boss wewe, sawa tu, sijui watuonaje.
Ukitaka kugombana na boss muulize vipi kuhusu zile bilionI 20 atapiga hesabu zake za magazijuto na kukwambia tayari nimeshatumia bilioni 50 za kwangu toka mfukoni. Hakika Kigwangala adumu zaidi, nahisi alishaona harufu ya kupigwa. Na sisi mashabiki hatujawahi kuuliza hata taarifa ya mapato na matumizi, mbaya zaidi tunamlinda boss mkubwa.
Swali dogo, kama Simba inampa hasara kwanini asikae pending akaachia wengine?
Asilimia kubwa ya Tajiri, ngonjera zake zinaanza akishahisi mpunga wa CAF unataka kuingia. Baada ya kuingia robo, kuna salio Simba inapokea, bilioni kadhaa. Hapo hesabu ni ndogo tu jana kasema katumia Bilion kadhaa kwa usajili, kwa hiyo atajilipa kupitia Bilion za CAF. Natumai huo mpunga unaingia kwenye akaunti yake na hakuna wa kuhoji.
Waacha tuendelee kupigwa, tumechagua upande wa kupigwa.