Simba inavuna walivyochopanda

Simba inavuna walivyochopanda

Wakati nilipinga usajili wa Simba kwenye baadhi ya maeneo kwenye Uzi wangu mashabiki wa Simba walinitungana Sana nakuniita me ni mshabiki wa yanga eti kisa nimeenda tofauti na mitazamo yao utazani hili jukwaa ni kwaajili ya Simba na yanga pekee.

Wazungu wanasema best transfer is to keep best your players in the club ndo maana Liverpool hawajasajili mchezaji yoyote zaidi kuwabakisha wachezaji wao waliwapa mafanikio msimu uliopita Kama mo salah,mane,vvd n.k.Hiv kilikuwa na aja gani kumnunua yule straiker mbrazili wakati statistics zake za ufungaji hazirizishi au ndo ile 10% imeusika alafu unakataa kumwongezea mkataba okwi et ana dai dau kubwa wakati unamlipa huyu mbrazili Mara 2 ya dau aliloitaji okwi.

Hiv ukiwekewa niyonzima na kahata yupi utachagua? Kahata ana kipi special Cha kumzidi niyonzima? kingine ndo chanzo kikuu Cha kufeli Simba ni kumuuza kotei Bila kuleta replacement sahihi ukiangalia timu ya Simba Sasa hiv aina kabisa kiungo mkabaji, shobobo na mkude ni wazuri wakiwa na mpira ila sio wazuri wakiwa hawana mpira.

Tatizo lingine lilikuwa msimu uliopita lilikuwa backline nilitegemea msimu huu watafanyia kazi me nilitegemea watamsajili beki no 5 ya nkana alikuwa mzuri eti wamembakisha Wawa ni matumizi mabaya ya fedha Bora tu angebaki juuko kuliko Wawa

NB: Malengo walijiwekea Simba msimu huu wa kufika semi fainal ya caf champion league ufanani na usajili waliofanya wametumia hela nyingi kuwasajili wabrazili wanaoenda kukaa bench mpira wa 10% unarudisha Sana mpira wa Tanzania.
Maeneo yote uliyoyataja Simba tumesajili tena wachezaji bora sana, kocha ameamua asiwachezeshe sisi tufanye nini.
 
Mkuu washabiki wa Simba asilimia kubwa huwa hawataki kuambiwa ukweli.
Wao wanataka kila kitu kuhusu simba usifie tu.
Maeneo yote tumesajili, kocha amekariri kuwa wachezaji ni Kotei na Okwi, mpe kocha mwenye akili akuoneshe ubora wa wachezaji wapya.
 
Hamtaki kusema kitu! UCHEBE si kocha wa mbinu! Hata jana amedhihirisha hilo! Kikosi cha SIMBA cha mwaka jana hata JULIO ama MECKY MEXIME angefanikiwa... Kocha hana mbinu ndo mana CAF hakupata hata point 1 ugenini walau basi kwa mbinu zake angezuia zile tano tano!
Hiyo ndio point kubwa, kocha hajui mpira, hajui hata kufanya sub, jana Mkude alipoanza kuboronga akamsimamisha Fragha na Muzamir kupasha, badala kufanya sub faster ili timu itulie akawaacha wanapasha mpaka mpira unaisha
 
Tatizo mashabiki wengi wa Simba hawataki kukubali ukweli kuwa pamoja na mapungufu ya Kotei kwenye kupiga pasi lakini alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kupokonya mipira na kutibua mashambulizi ya adui. Kotei alificha sana madhaifu ya Mkude, Nyoni na Wawa (japo kwenye mechi ya jana Nyoni na Wawa walijitahidi sana kucheza vizuri). Kama kuna kosa lilifanyika wakati wa usajili ni kuacha kusajili beki wa kati mmoja na kiungo mkabaji mmoja wenye uwezo na kulijua soka la Afrika. Kwa mpira wa sasa hivi beki wa kati na kiungo mkabaji ndio huwa wanaanzisha mashambulizi kueleka kwenye eneo la timu pinzani ndio maana hawa watu wanatakiwa watu wa kazi zaidi na wasio watu wa mbwembwe.

Ukiangalia vizuri mechi ya jana UD Songo walikuwa wanapita zaidi katikati kwa sababu kuna shimo lilikuwa wazi kwa Mkude. Walishindwa kabisa kupita pembeni kwa sababu Gadiel na Kapombe walikuwa vizuri sana.

Wakati mwingine ujuaji wa viongozi wetu kwenye usajili ndio tatizo. Yaani suala la kumuacha Kotei linanikumbusha namna walivyomuacha Hamis Tambwe miaka ile baadae tukabaki tunalia jinsi alivyokuwa anatuadhibu.

Pia kulikuwa na haja gani ya kuwaleta wabrazili watatu kwa mpigo ilihali tunajua kuwa itabidi wakae benchi mpaka wazoee ligi yetu? Kuna haja sasa ya "MO" kuunda timu ya scouting ya hata watu watano wakiwemo wachezaji wa zamani na makocha wa Simba wapewe pesa wazunguuke kwenye ligi mbalimbali ndani na nje ya nchi kisha waushauri uongozi kwa wale wachezaji wanaowana wanafaa kuchezea Simba. Na muda mzuri wa kufanya usajili ni sasa kuingia pre contract na wachezaji wazuri maana ligi zikiisha kila mchezaji mzuri anawahiwa na klabu vigogo za Afrika kama ilivyotokea.

Ni muda muafaka sasa Kwa Simba kuwa na timu ya scouting na match analyst. Timu ya scouting kwa haraka inaweza kuonekana kama inaongeza gharama lakini iwapo itafanya kazi vizuri inaweza kupunguza gharama sana kwani unaweza kupata mchezaji bora sana ambaye hajulikani kwa gharama ndogo lakini uwanjani akakupa matokeo mazuri kuliko hata wachezaji ulisajili kwa mamilioni.
Kiungo mkabaji wa kati ni Fragha, mabeki wa kati wapo wa kumwaga, Mlipili, Kennedy na Dos Santos. Simba hakuna kocha.
Hiki kikosi cha Simba ukimpa Matola anafanya maajabu.
 
Alichofanikiwa sana kocha ni kuwaaminisha watu kuwa kuondoka kwa Kotei ni pengo kwa kutompanga Fragha, wengi wanalalamika kuwa Kotei ni pengo wakati kuna kiungo mkabaji Fragha na mzuri kuliko Kotei, ametulia, ana pasi za uhakika. Kocha angekuwa anampanga watu wangeona usajili ulivyo bora.
 
Labda inawezekana kwenye mazoezi hajaonesha kiwango cha kuaminika na Uchebe.
 
Kiungo mkabaji wa kati ni Fragha, mabeki wa kati wapo wa kumwaga, Mlipili, Kennedy na Dos Santos. Simba hakuna kocha.
Hiki kikosi cha Simba ukimpa Matola anafanya maajabu.
Mheshimiwa Chesty nikisoma maelezo yako ukiwajibu wanabodi mbali mbali kwenye huu uzi unaelekea upo karibu sana na uongozi wa Simba kama wewe mwenyewe sio kiongozi. Kwa jinsi ninavyoelewa kuwa mpira wa miguu hauna lugha kwa maana anaweza kutoka mchezaji Ghana kwenda kucheza China wakati hata hajui neno moja la Kichina na akacheza ligi msimu mzima bila wasiwasi. Sasa vipi hawa wabrazili wetu ambao tumeambiwa wamepewa kamusi wajifunze Kiswahili kwanza ndio waanze kupangwa? Au Uchebe hakushirikishwa kwenye usajili wao? Au kuna wachezaji Uchebe alipendekeza wasijaliwe halafu uongozi ukapuuza na kuwasjili hao wabrazili? Au amemaindi mlivyolipiga panga lile garasa lake Zana Coulibaly lililosajiliwa As Vita?
 
Maeneo yote tumesajili, kocha amekariri kuwa wachezaji ni Kotei na Okwi, mpe kocha mwenye akili akuoneshe ubora wa wachezaji wapya.
Kwahiyo ubora wa mchezaji unaonyeshwa na kocha? Au mchezaji mwenyewe? Kama hawa perform mazoezini wataanzaje sasa kwenye mechi?
Pengo la kotei lipo linaonekana kabisa mkude hawezi kukaba hili kila siku linasemwa na linaonekana wazi kabisa.
Kwa okwi anacheza Deo kanda ambaye anajua sana kuchezea Moira na kupiga vichenga lakini output yake huwa ni mbovu lakini okwi anajua sana kuwatoka watu na kufunga.
 
Mheshimiwa Chesty nikisoma maelezo yako ukiwajibu wanabodi mbali mbali kwenye huu uzi unaelekea upo karibu sana na uongozi wa Simba kama wewe mwenyewe sio kiongozi. Kwa jinsi ninavyoelewa kuwa mpira wa miguu hauna lugha kwa maana anaweza kutoka mchezaji Ghana kwenda kucheza China wakati hata hajui neno moja la Kichina na akacheza ligi msimu mzima bila wasiwasi. Sasa vipi hawa wabrazili wetu ambao tumeambiwa wamepewa kamusi wajifunze Kiswahili kwanza ndio waanze kupangwa? Au Uchebe hakushirikishwa kwenye usajili wao? Au kuna wachezaji Uchebe alipendekeza wasijaliwe halafu uongozi ukapuuza na kuwasjili hao wabrazili? Au amemaindi mlivyolipiga panga lile garasa lake Zana Coulibaly lililosajiliwa As Vita?
Hahahaha, mie sipo karibu na uongozi ila nahisi ni kweli hakupenda garasa lake liondolewe Simba.

Uchebe amefanikiwa kuwashawishi watu kuwa Simba hawana kiungo mkabaji kama Kotei kwa kuamua kutompanga Fragha.

Pale Simba tulipoanza tu kushambuliwa alimsimamisha Fragha na Muzamir kupasha, nadhani ulikuwa ushauri wa kocha msaidizi, alichofanya aliwasimamisha lakini akagoma kuwaingiza.

Angemuingiza Fragha pale nyuma pangetulia ila anataka kuwaaminisha watu kuwa hatuna kiungo mkabaji na mabeki ili aendelee kumchezesha Wawa.

Ushauri wangu afungashiwe virago tutafute kocha mbongo atuletee ubingwa.
 
Wakati nilipinga usajili wa Simba kwenye baadhi ya maeneo kwenye Uzi wangu mashabiki wa Simba walinitungana Sana nakuniita me ni mshabiki wa yanga eti kisa nimeenda tofauti na mitazamo yao utazani hili jukwaa ni kwaajili ya Simba na yanga pekee.

Wazungu wanasema best transfer is to keep best your players in the club ndo maana Liverpool hawajasajili mchezaji yoyote zaidi kuwabakisha wachezaji wao waliwapa mafanikio msimu uliopita Kama mo salah,mane,vvd n.k.Hiv kilikuwa na aja gani kumnunua yule straiker mbrazili wakati statistics zake za ufungaji hazirizishi au ndo ile 10% imeusika alafu unakataa kumwongezea mkataba okwi et ana dai dau kubwa wakati unamlipa huyu mbrazili Mara 2 ya dau aliloitaji okwi.

Hiv ukiwekewa niyonzima na kahata yupi utachagua? Kahata ana kipi special Cha kumzidi niyonzima? kingine ndo chanzo kikuu Cha kufeli Simba ni kumuuza kotei Bila kuleta replacement sahihi ukiangalia timu ya Simba Sasa hiv aina kabisa kiungo mkabaji, shobobo na mkude ni wazuri wakiwa na mpira ila sio wazuri wakiwa hawana mpira.

Tatizo lingine lilikuwa msimu uliopita lilikuwa backline nilitegemea msimu huu watafanyia kazi me nilitegemea watamsajili beki no 5 ya nkana alikuwa mzuri eti wamembakisha Wawa ni matumizi mabaya ya fedha Bora tu angebaki juuko kuliko Wawa

NB: Malengo walijiwekea Simba msimu huu wa kufika semi fainal ya caf champion league ufanani na usajili waliofanya wametumia hela nyingi kuwasajili wabrazili wanaoenda kukaa bench mpira wa 10% unarudisha Sana mpira wa Tanzania.
Nakumbuka kwenye uzi ule tulitukanwa sana tulioponda usajili wa simba
 
Kwahiyo ubora wa mchezaji unaonyeshwa na kocha? Au mchezaji mwenyewe? Kama hawa perform mazoezini wataanzaje sasa kwenye mechi?
Pengo la kotei lipo linaonekana kabisa mkude hawezi kukaba hili kila siku linasemwa na linaonekana wazi kabisa.
Kwa okwi anacheza Deo kanda ambaye anajua sana kuchezea Moira na kupiga vichenga lakini output yake huwa ni mbovu lakini okwi anajua sana kuwatoka watu na kufunga.
Visingizio ni mazoezini, kwa hiyo Gadiel na Manula walionesha viwango mazoezini kuliko Shabalala na Kakolanya.

Aussems hajifichi udhaifu wake kwa mtu anayejua mpira, ndio maana aligombana na Masoud Djuma.
 
Simba niliwashangaa sana kumsajili Ajib na kumwacha Okwi kisa kadai pesa nyingi hivi Mo anapoongea kuwa anataka kushindana na Tp mazembe huwa anaota au anakurupuka kama Okwi kadai pesa nyingi aachane na kusajili wachezaji kama Ajibu na Hizo pesa ampe Okwi maana kazi yake tulikuwa tunaiona, wanamng'ang'aniaBoko wakati umri umeenda na ni majeruhi mara kwa mara wangemruhusu tu aende Porokwa na pesa za usajili wakaongeza kwa Okwi, unaacha beki kama Juuko unamwongezea mkataba wawa ambaye umri umeenda, mtu kama Ndemla unamwongezea mkataba wakatu humtumii kweli nimeamini wahindi mchezo wao ni kriketi sio mpira
 
Simba imekosa upgrade ya Okwi, Kotei na Niyonzima ndiyo maana imepoteana.

Okwi anajua kuforce mashambulizi, kufunga na kupiga pasi za mwisho.

Msimu uliopita watu magoli mengi ya hatua za Knockout stage Okwi alihusika.

Kingine Okwi alikuwa amekomaa kiakili na anaijua football culture ya simba vizuri kuliko Deo Kanda.
Kwahiyo ubora wa mchezaji unaonyeshwa na kocha? Au mchezaji mwenyewe? Kama hawa perform mazoezini wataanzaje sasa kwenye mechi?
Pengo la kotei lipo linaonekana kabisa mkude hawezi kukaba hili kila siku linasemwa na linaonekana wazi kabisa.
Kwa okwi anacheza Deo kanda ambaye anajua sana kuchezea Moira na kupiga vichenga lakini output yake huwa ni mbovu lakini okwi anajua sana kuwatoka watu na kufunga.
 
Simba imekosa upgrade ya Okwi, Kotei na Niyonzima ndiyo maana imepoteana.

Okwi anajua kuforce mashambulizi, kufunga na kupiga pasi za mwisho.

Msimu uliopita watu magoli mengi ya hatua za Knockout stage Okwi alihusika.

Kingine Okwi alikuwa amekomaa kiakili na anaijua football culture ya simba vizuri kuliko Deo Kanda.
Deo kanda ni mchezaji machachari ila okwi ni mchezaji hatariiii
 
No Mo kazungukwa na watu ambao siyo wa football.

Kama anataka kufanikiwa pale Simba aajiri Football director au technical director waanzishe na scouting Department watafanya vizuri sana.

Kila siku najiuliza simba waliwezaje kumuona Tairone Dasilva wakashindwa kumuona Timothy Awany pale KCCA aliyemuweka benchi Murshid Juuko kwenye mashindano ya Afcon?

Waliwezaje kumuona Shiraf Shiboub na Gerson Fragha wakashindwa kumuona Allan Lwanga wa KCCA aliyekuwa akivaa Viatu vya Michael Azilla kwenye mashindano ya Afcon. Au hawakumuona Julius Mutyaba pale URA midfielder mwenye control nzuri kabisa kama walihitaji upgrade ya Kotei ?

Waliwezaje kumuona Kennedy Wilson wakashindwa kumuona Kijana mchanga kabisa pale Mbao Fc anayeitwa David Mwasa ?

Walihitaji backup ya Chama yes hawakumuona Bwana mdogo Tito Okello pale KCCA badala yake wakamnunua Ajibu tu ?
Simba niliwashangaa sana kumsajili Ajib na kumwacha Okwi kisa kadai pesa nyingi hivi Mo anapoongea kuwa anataka kushindana na Tp mazembe huwa anaota au anakurupuka kama Okwi kadai pesa nyingi aachane na kusajili wachezaji kama Ajibu na Hizo pesa ampe Okwi maana kazi yake tulikuwa tunaiona, wanamng'ang'aniaBoko wakati umri umeenda na ni majeruhi mara kwa mara wangemruhusu tu aende Porokwa na pesa za usajili wakaongeza kwa Okwi, unaacha beki kama Juuko unamwongezea mkataba wawa ambaye umri umeenda, mtu kama Ndemla unamwongezea mkataba wakatu humtumii kweli nimeamini wahindi mchezo wao ni kriketi sio mpira
 
Yawezekana kweli Deo kanda angeweza kuwa upgrade ya Niyonzima ila pengo la Okwi halizibiki kwa sasa .

Jana simba walilazimika kucheza 4,4,2 mfumo huu Nina miaka 3 sijawaona simba wakicheza nadhani walifanya hivi kwa kukosa options kwenye striking force kutokana na Bocco pamoja na Wilmer kuwa Majeruhi .
Deo kanda ni mchezaji machachari ila okwi ni mchezaji hatariiii
 
*BREAKING NEWS*

```Kutokana na sheria mpya za CAF , Yanga ikitolewa Champions ligi itaenda Shirikisho. Pia kutokana na sheria mpya za CUF ya Lipumba, Simba ikitolewa Champions Ligi itaenda mojakwamoja Nangwanda Sijaona kupambana na Ndanda.```
 
Back
Top Bottom