Simba inaweza kufuzu Kombe la Dunia la Vilabu 2025 bila kuchukua ubingwa wa CAF

Baada ya ripoti ya FIFA kutoka kuhusiana na ushiriki wa Simba katika Kombe la Dunia la Vilabu 2025, kumezuka malumbano mbalimbali. Kuna upande umekuwa unasema Simba hawezi kwenda kushirki mashindano yale bila kuchukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Africa msimu huu na kwa mtazamo wao ana nafasi sawa na Yanga.

View attachment 2853423

Jana baada ya kushiba pilau langu la Krismasi, nikaangalia vizuri mkeka mzima wa FIFA nikaona Simba ana nafasi ya kwenda Kombe la Dunia bila kuwa bingwa wa CAF ndiyo maana hata wao katika chapisho lao wameonyesha Simba ni miongoni mwa timu zinazoweza kufuzu kwa points inazoendelea kujikusanyia. Hapa chini nitaenda kukuonyesha ni jinsi gani hilo linaweza kutokea.

Kwanza nianze kwa kusema, Simba mpaka sasa amejikusanyia point 48 na siyo 45 kama ilivyoainishwa na FIFA kwa sababu ile ripoti iliandaliwa kabla ya mechi ya mwisho ambayo Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Wydad.

Tukienda kimahesabu tu, Simba inaweza kufuzu bila kuchukua kombe la CAF Klabu Bingwa kama mambo 3 yatatimia:

1. Bingwa msimu huu awe Al Ahly au Mamelodi

2. Esperance apoteze mechi mbili zilizobaki za makundi na atolewe katika mashindano ya klabu bingwa

3. Simba ashinde mechi 2 zilizobaki za Makundi halafu ashinde mechi zote mbili za robo fainali, halafu ashinde zote mbili za nusu fainali na aingie fainali. Akiingia fainali, Simba haihitaji kushinda mechi hata moja ingawa akitoka sare angalau mechi moja itakuwa nzuri zaidi

Mambo yote matatu yakitimia, Simba atafikisha point 75 sawa na Esperance. Sijajua FIFA watatumia kigezo gani iwapo hali hii itatokea ya timu mbili kulingana point katika rank.

Tuishi humo.

Haki zote za bandiko hili zimehifadhiwa.
Ok je hkn kigezo cha "aliyewahi kuwa bingwa wa cafcl kuchukuliwa" kikatumika kuwachukua esperance?
 
Makolo acheni propaganda za kulazimisha furaha elekezeni nguvu kwenye kuijenga timu yenu
 
Maana yake ni kwamba wote hao watatu CRB, Esperence na Petro de Luanda wapoteze Simba ashinde umempa nini Mungu?
[emoji23][emoji23][emoji23] wejama umefurahisha kweli. . (Eti umempa nini Mungu?)
 
Kwa hawa wachezaji wa mchongo n ndoto labda mwakan tujipange na full gear
 
Baada ya ripoti ya FIFA kutoka kuhusiana na ushiriki wa Simba katika Kombe la Dunia la Vilabu 2025, kumezuka malumbano mbalimbali. Kuna upande umekuwa unasema Simba hawezi kwenda kushirki mashindano yale bila kuchukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Africa msimu huu na kwa mtazamo wao ana nafasi sawa na Yanga.

View attachment 2853423

Jana baada ya kushiba pilau langu la Krismasi, nikaangalia vizuri mkeka mzima wa FIFA nikaona Simba ana nafasi ya kwenda Kombe la Dunia bila kuwa bingwa wa CAF ndiyo maana hata wao katika chapisho lao wameonyesha Simba ni miongoni mwa timu zinazoweza kufuzu kwa points inazoendelea kujikusanyia. Hapa chini nitaenda kukuonyesha ni jinsi gani hilo linaweza kutokea.

Kwanza nianze kwa kusema, Simba mpaka sasa amejikusanyia point 48 na siyo 45 kama ilivyoainishwa na FIFA kwa sababu ile ripoti iliandaliwa kabla ya mechi ya mwisho ambayo Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Wydad.

Tukienda kimahesabu tu, Simba inaweza kufuzu bila kuchukua kombe la CAF Klabu Bingwa kama mambo 3 yatatimia:

1. Bingwa msimu huu awe Al Ahly au Mamelodi

2. Esperance apoteze mechi mbili zilizobaki za makundi na atolewe katika mashindano ya klabu bingwa

3. Simba ashinde mechi 2 zilizobaki za Makundi halafu ashinde mechi zote mbili za robo fainali, halafu ashinde zote mbili za nusu fainali na aingie fainali. Akiingia fainali, Simba haihitaji kushinda mechi hata moja ingawa akitoka sare angalau mechi moja itakuwa nzuri zaidi

Mambo yote matatu yakitimia, Simba atafikisha point 75 sawa na Esperance. Sijajua FIFA watatumia kigezo gani iwapo hali hii itatokea ya timu mbili kulingana point katika rank.

Tuishi humo.

Haki zote za bandiko hili zimehifadhiwa.
Kweli ulikuwa umevimbiwa pilau ulipokuwa unafanya hayo mahesabu.
 
Ukimaliza kupiga mahesabu ya Simba kumfikia Es Tunis, basi anza kupiga na mahesabu ya Belouizdad na Petro de luanda ambao wote hao ni bora kitakwimu na kiubora kuliko Simba.

Mimi ni shabiki wa Simba ila Njia pekee ya Simba kuingia Club word cup ni kushinda CAF hiyo miujiza mingine ya Point Tuondoe kichwani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukimaliza kupiga mahesabu ya Simba kumfikia Es Tunis, basi anza kupiga na mahesabu ya Belouizdad na Petro de luanda ambao wote hao ni bora kitakwimu na kiubora kuliko Simba.

Mimi ni shabiki wa Simba ila Njia pekee ya Simba kuingia Club word cup ni kushinda CAF hiyo miujiza mingine ya Point Tuondoe kichwani.
Toa mfano wa jinsi gani hayo mambo matatu niliyoyaorodhesha yatokee halafu bado CRB au Petro apate point nyingi kumzidi Simba
 
Back
Top Bottom