Simba kufika makundi haimaanishi ubora kuliko Yanga

Simba kufika makundi haimaanishi ubora kuliko Yanga

Ndio uone De agosto haipo hapo kuonyesha kuwa ni kitimu kibovu sana, simba iko hapo lakini inachapwa na Yanga mfululizo kuonyesha kuwa Simba iko hapo kimchongo (kimakosa). Kaka hujui hata kufikiria na kutafakari.
Kwa hiyo unakubali ninyi pia hampo hapo hivyo ni underdog mbele ya Simba?

Hivyo Al Hillal msingeiweza hata iweje? Sasa kama ngoma kumpiga mtu hiyo jeuri mmeitoa wapi?

Ninyi kucheza na sisi kwenu ndio kombe la Dunia wakati Simba ninyi anawaona kama vidagala tu.
 
Sisi Simba tunakubali tulipewa kibonde, na lazima ifike kipindi ninyi Yanga mtambue kuwa hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa hukutanisha timu kubwa dhidi ya vibonde, na kibonde huanzia kwake.

Esperance alipewa Plateu
Mamelodi alipewa La Passe
Raja alipewa Nigelec
Al Ahly akapewa Monastir
Simba tukapewa De Agosto
Al Hilal wakapewa Uto

Lengo ni kuhakikisha vibonde hawatoboi ili kuyapa hadhi mashindano
 
Je, De Agosto ya Simba ni bora kuliko Al-Hilal ya Yanga? Au zina ubora sawa?

Kama ukishindwa kutoa jibu sahihi kwenye maswali haya, basi Simba inaweza kuchapwa na Yanga tarehe 23 October bila kulazimika kumlaumu Mgunda. Na wala Nabi asilaumiwe kwa kutolewa na Al Hilal kwa kumlinganisha na Mgunda aliyeifikisha Simba makundi.

Kwenye mashindano yale, tatizo halikuwa ni Nabi bali wachezaji wenyewe.
Kwanza unapaswa kujua De 1°Agosto ni mabingwa wa Angola inapotokea Altetico Petro Luanda. Kwa hiyo jibu ni Ndiyo, Agosto ni bora kuliko Al Hilal.
Unapaswa pia kukumbuka hao Al Hilal walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya reserves wa Simba na wakaambulia goli 1 na pia Simba waliwatandika 4-1 hapo Mkapa Stadium.
Na kama tatizo lilikuwa wachezaji na siyo Nabi hebu tuambie Djuma amepungua unene au Aucho amepungua uzito? Kisinda ameanza kukimbia na mpira akiwa na malengo yanayoeleweka? Au unataka kusema Diara ameacha kuwa na wenge golini? Mwamnyeto je, hatamkaba Musa kwa macho anavyolipasua goli mara 3?
Mpaka sasa Mgunda ni bora kuliko Nabi. Kwenye mechi 5 za mwisho Mgunda kashinda zote na kuruhusu goli 1 tu wakati Nabi kashinda 3 tu na kiruhusu magoli 3.
 
Sisi Simba tunakubali tulipewa kibonde, na lazima ifike kipindi ninyi Yanga mtambue kuwa hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa hukutanisha timu kubwa dhidi ya vibonde, na kibonde huanzia kwake.

Esperance alipewa Plateu
Mamelodi alipewa La Passe
Raja alipewa Nigelec
Al Ahly akapewa Monastir
Simba tukapewa De Agosto
Al Hilal wakapewa Uto

Lengo ni kuhakikisha vibonde hawatoboi ili kuyapa hadhi mashindano
Simba ni kibonde kwa Yanga kwenye ligi,, ngao na championship. Hushangai tyuu?
 
Pia naongezea simba haijawah kuifunga timu yeyote ngumu kuelekea makundi.. ref; nkana, platinum, red arrows na Agosto
Taja timu alizozifunga yanga kuelekea makundi ambazo ni ngumu, pia taja timu ngumu zilizomfunga yanga kuelekea makundi
 
Si mpenzi wa timu yoyote lakini ni jiuliza Bora kipi kuwa na timu Bora kama yanga lakini haishindi au kuwa na hiyo mbovu kama Simba halafu inashinda
 
Si mpenzi wa timu yoyote lakini ni jiuliza Bora kipi kuwa na timu Bora kama yanga lakini haishindi au kuwa na hiyo mbovu kama Simba halafu inashinda
Issue ni inashindaje? Tuliona vitendo ambavyo ni unsporting kama kumulika vitochi na mijitochi wachezaji usoni, kuwasha moto viwanjani, watu kuhofia kuingia vyumba vya kubadilisha nguo kuogopa pulizapuliza na kununua waamuzi. Hivi ni vitendo ambayo Yanga ama wanaogopa au wanashindwa au hawataki kuvitumia kumanipulate mechi,
 
Umeonae, kuingia makundi haikumaanisha kuw simba Iko juu kuliko Yanga. Simba na Yanga ni mbwa na dog TU, Simba ni dog na Yanga ni mbwa. Lakini pia Simba ni mbwakoko na Yanga ni German shield..
 
Back
Top Bottom