Simba kukosa nyota wanne kwenye mchezo dhidi ya AS Vita

Simba kukosa nyota wanne kwenye mchezo dhidi ya AS Vita

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
20210211_142900.jpg

Kikosi cha Simba sports kimeondoka siku ya Jumannne kuelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.

Mchezo huo ambao utapigwa siku ya tarehe 12 Ijumaa, Simba anaingia kwenye mchezo bila nyota wake wanne, wachezaji hao ni Erasto Nyoni, John Bocco, David Kameta na Perfect Chikwende.

Nyoni na Bocco watakosa mchezo huo kufuatia kuwa majeruhi ambapo mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni Januari 6 kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Aidha David Kameta hakuwa miongoni mwa waliondoka na kikosi cha Simba kuelekea DR Congo kwakuwa ametajwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20) ambao wanatarajia kuelekea Mauritania kushiriki mashindano ya Kombe la mataifa ya Afrika chini ya miaka 20.

Huku Perfect Chikwende akiukosa mchezo huo kufuatia kanuni za mashindano hayo kwakuwa tayari alishiriki akiwa na FC Platinum ya Zimbabwe.

Kwa upande wa mahasimu wao kwenye mchezo huo, Vita Club inashika nafasi ya 3 katika Msimamo wa Ligi kuu DRC ikiwa imecheza michezo 14 na haijapoteza mchezo wowote.

Kama ilivyo kwa Simba sc, Vita imebadilika sana katika kikosi chao. Wachezaji wengi wameondoka na kuja wengine.

2018 Vita ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.
 
View attachment 1699849

Kikosi cha Simba sports kimeondoka siku ya Jumannne kuelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club....
Chikwende ilikuwa wazi kuwa hangeweza kushiriki kutokana na kanuni husika, Nyoni kwa muda mrefu hana namba katika kikosi cha Simba na huyo dogo ndio anapigania namba. Wachezaji uliotaja siyo pengo kivile na siyo sababu ya kufanya vibaya.
 
Hata first eleven hao wote huwa hawapo.

Msiposhinda mechi dhidi ya As Vita mtaambulia kutoka na alama sifuri.

 
...la chikwende si tuliwaambiaga hapa mkajifanya much know
 
1998 ndio Mara ya mwisho Yanga kushiriki hatua hii ya makundi ambayo Simba ipo. Ili kujua kuwa 1998 ni mbali au karibu ,hebu kumbuka ulikuwa level gani ya elimu au mwanao alikuwa level gani.
 
Utopolo walivyokomalia mechi ya simba na as vita utafikiri na wao wanashiriki hili kombe kumbe wanasubiri hisani ya simba ili mwakani wabwebwe
 
Back
Top Bottom