Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Kikosi cha Simba sports kimeondoka siku ya Jumannne kuelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.
Mchezo huo ambao utapigwa siku ya tarehe 12 Ijumaa, Simba anaingia kwenye mchezo bila nyota wake wanne, wachezaji hao ni Erasto Nyoni, John Bocco, David Kameta na Perfect Chikwende.
Nyoni na Bocco watakosa mchezo huo kufuatia kuwa majeruhi ambapo mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni Januari 6 kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Aidha David Kameta hakuwa miongoni mwa waliondoka na kikosi cha Simba kuelekea DR Congo kwakuwa ametajwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20) ambao wanatarajia kuelekea Mauritania kushiriki mashindano ya Kombe la mataifa ya Afrika chini ya miaka 20.
Huku Perfect Chikwende akiukosa mchezo huo kufuatia kanuni za mashindano hayo kwakuwa tayari alishiriki akiwa na FC Platinum ya Zimbabwe.
Kwa upande wa mahasimu wao kwenye mchezo huo, Vita Club inashika nafasi ya 3 katika Msimamo wa Ligi kuu DRC ikiwa imecheza michezo 14 na haijapoteza mchezo wowote.
Kama ilivyo kwa Simba sc, Vita imebadilika sana katika kikosi chao. Wachezaji wengi wameondoka na kuja wengine.
2018 Vita ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco.