Simba kumtambulisha mchezaji mpya leo usiku

Simba kumtambulisha mchezaji mpya leo usiku

Achraf Hakimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2010
Posts
943
Reaction score
1,944
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah 'Try Again' ametuma ujumbe kwa mashabiki wa timu hiyo kupitia mitandao ya kijamii akiandika; "Wa mwisho kufurahi, hufurahi zaidi. Mtafurahi kwelikweli,"

Simba itatangaza mchezaji mwingine mpya leo saa 5 usiku zikisalia saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kesho Jumapili Januari 15 saa 5:59 usiku. Hadi sasa Simba imemtambulisha Saido Ntibazonkiza ambaye tayari ameshacheza mechi moja ya Ligi Kuu akiitumikia Simba na kufunga mabao 3.

#mwanaspoti
 
Manzoki navyo sikia ana majeraha, sidhani kama atasajiliwa

Wapo wadau wanaomuhusisha Feisal kwenye utambulisho wa baadae kwa kile alicho post kwenye page yake

Viongozi wa Simba this time msifanye makosa tuleteeni mtu wa maana
Feisal hawezi kutambulishwa Simba kwasababu tayari kuna sekeseke la kimkataba dhidi ya Yanga. Tetesi zinaonesha ni kiungo Ismael Sawadogo
 
Manzoki navyo sikia ana majeraha, sidhani kama atasajiliwa

Wapo wadau wanaomuhusisha Feisal kwenye utambulisho wa baadae kwa kile alicho post kwenye page yake

Viongozi wa Simba this time msifanye makosa tuleteeni mtu wa maana
Walete mchezaji wa kuanza kikosi cha kwanza sio wa kuketi benchi.
 
Jamaa yupi huyo mkuu?!
FB_IMG_16737135383129461.jpg

Jean Baleke
 
Viongozi wa Simba kuna wakati utafikiri wapo "serious" lakini ukiwafuatilia kwa makini hawapo "serious" kabisa. Ni kama vile marehemu Hanspope aliondoka na "password" ya usajili. Utaona picha kwenye vyombo vya habari bodi imekaa kuzungumzia usajili halafu msimu wa pili huu timu inapata shida kwenye kiungo mkabaji na mshambuliaji wa kati wakati madirisha mawili ya usajili yameshapita. Tangu Fraga na Lwanga waumie Simba haijatafuta kiungo mkabaji asili. Tangu Kagere na Magalu uwezo ushuke na Boko aandamwe na majeruhi Simba haijatafuta mshambuliaji hasa wa kati. Simba wana timu nzuri lakini hizi nafasi mbili zinakosa watu waliokamilika hasa na kuzimudu kwa ufasaha.

Na hata hili dirisha dogo kama sio kocha mpya kuwasanua viongozi wa Simba lilikuwa lipite hivi hivi bila kutafuta mshambuliaji asili wa kati. Sababu utaambiwa kuwa Sidoo yupo eti kwa sababu mechi ya kwanza tu kafunga goli tatu, Wanasahau kuwa umri wa Saidoo na Boko pamoja na uwezo mkubwa walionao bado wasingeweza kwenda sambamba na na mechi zilivyo karibu karibu ukizingatia Simba inashiriki mashindano matatu kwa mpigo. Na mbaya zaidi wote Saidoo na Boko ni watu wa pancha sana majeraha kwao jumlisha umri ingekuwa vigumu kutoa mchango wao mpaka mwisho wa msimu.
 
Back
Top Bottom