Viongozi wa Simba kuna wakati utafikiri wapo "serious" lakini ukiwafuatilia kwa makini hawapo "serious" kabisa. Ni kama vile marehemu Hanspope aliondoka na "password" ya usajili. Utaona picha kwenye vyombo vya habari bodi imekaa kuzungumzia usajili halafu msimu wa pili huu timu inapata shida kwenye kiungo mkabaji na mshambuliaji wa kati wakati madirisha mawili ya usajili yameshapita. Tangu Fraga na Lwanga waumie Simba haijatafuta kiungo mkabaji asili. Tangu Kagere na Magalu uwezo ushuke na Boko aandamwe na majeruhi Simba haijatafuta mshambuliaji hasa wa kati. Simba wana timu nzuri lakini hizi nafasi mbili zinakosa watu waliokamilika hasa na kuzimudu kwa ufasaha.
Na hata hili dirisha dogo kama sio kocha mpya kuwasanua viongozi wa Simba lilikuwa lipite hivi hivi bila kutafuta mshambuliaji asili wa kati. Sababu utaambiwa kuwa Sidoo yupo eti kwa sababu mechi ya kwanza tu kafunga goli tatu, Wanasahau kuwa umri wa Saidoo na Boko pamoja na uwezo mkubwa walionao bado wasingeweza kwenda sambamba na na mechi zilivyo karibu karibu ukizingatia Simba inashiriki mashindano matatu kwa mpigo. Na mbaya zaidi wote Saidoo na Boko ni watu wa pancha sana majeraha kwao jumlisha umri ingekuwa vigumu kutoa mchango wao mpaka mwisho wa msimu.