Simba kumtambulisha mchezaji mpya leo usiku

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah 'Try Again' ametuma ujumbe kwa mashabiki wa timu hiyo kupitia mitandao ya kijamii akiandika; "Wa mwisho kufurahi, hufurahi zaidi. Mtafurahi kwelikweli,"

Simba itatangaza mchezaji mwingine mpya leo saa 5 usiku zikisalia saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kesho Jumapili Januari 15 saa 5:59 usiku. Hadi sasa Simba imemtambulisha Saido Ntibazonkiza ambaye tayari ameshacheza mechi moja ya Ligi Kuu akiitumikia Simba na kufunga mabao 3.

#mwanaspoti
Hawa si walitutukana sana wananchi tulipokuwa tunatangaza wachezaji wetu usiku..!? Eti Bantu Lady , si unakumbuka? Haya, yamewakuta yepi?
 
Let's pray
1673764403762.jpg
 
Hebu tumia factor hiyo ya umri kuongelea kiwango cha Messi, Modric, pepe, Giroud n.k kwenye World Cup.
Acha kufaninisha kifo na usingizi. Hivi kambi, madaktari, wataalamu wa viungo, madaktari wa timu, wataalamu wa chakula, medical checkup, ratiba za mechi na mazoezi, miundo mbinu ya viwanja vya mazoezi na mechi, usafiri n.k. wa hao wazee wa ulaya uliwataja unataka ulinganishe na hawa wazee wa hapa kwetu. Hapa Tanzania na sehemu mkubwa ya Afrika wachezaji wengi wakishafikisha miaka 28 - 30 tayari ni veterani labda itokee mchezaji mmoja mmoja (mfano mmojawapo ni Madaraka Suleiman mzee wa kiminyio) kutokana na alivyojitunza awe yupo fiti kwa asilimia 100 kwenye umri mkubwa wakati ulaya wachezaji wenye umri huo ndio kwanza wachezaji wanakuwa kwenye "peak".

Huwezi kuwategemea Saidoo na Boko wacheze dakika 90 kila baada ya siku mbili/tatu kwenye NBC, AZAM na CAF champions halafu wawe na ufanisi wa asilimia 100 ndio maana hata kocha kawasanua viongozi kistaarabu kuwa anataka mshambuliaji mwingine. Maana yake pale Simba Kyombo ndio alipaswa kusaidia hili zoezi la "rotation" lakini ameonyesha kiwango kidogo. Suala la pancha/majeraha ya mara kwa mara kwa Boko na Saidoo ni kitu cha wazi kabisa kwa yeyote anayefuatilia ligi yetu kwa takribani miaka miwili/mitatu iliyopita. Duru la kwanza Boko alikuwa majeruhi mwishoni ndio karudi na ukumbuke mchezaji akitoka majeruhi mpaka gari liwake anachukua muda kwa hiyo timu inapaswa kuwa na mchezaji timamu kwenye benchi sio aina ya Kyombo.
 
Maelezo yote haya hata sikuelewi. Jikite kwenye hoja ya msingi kwa kutumia wachezaji niliowataja kisha ndio ulete wacbezaji wako unaotaka kuwapondea.
 
Back
Top Bottom